Tuesday, October 20, 2015

SEHEMU YA PILI: BARAKA TANO ZA PETRO NA KANUNI KUMI ZA KUFIKIA MAFANIKIO YAKO.

Tunaendelea
Kwanza naomba amini maneno haya;

"Maadamu yu hai...
1. Unaweza songa mbere zaidi
2. Unaweza toka hapo ulipo
3. Unaweza kuwa mtu huru
4. Unaweza kuwa mtu uliyefikiri kuwa
5. Unaweza kuishi maisha ya mafanikio unayotaka kuishi
6. Unaweza kuacha historia nzuri katika ulimwengu huu
7. Unaweza kubadirika
8. Unaweza kubadiri tatizo lako kuwa neema
9. Unaweza kubadiri historia mbaya kuwa nzuri
10. Unaweza kuinua maono yako na kuyaanza tena na kuyatimiza.
11. Bado unaweza kuwa jasiri tena
12. Unaweza kuwa mtakatifu tena na mwenye haki
13. Unaweza kuwa mtumishi tena
14. Unaweza kufanya uliyowaza kuyafanya.

Bado unaweza....
Na "LEO" ndiyo siku pekee unayoweza kufanya maamuzi ya kufanya haya. Jana haikuwa siku sahihi, kesho haigusiki, na hatujui.


JANA IMEISHA, LEO NI SIKU MPYA,  KESHO YAWEZA NZURI ZAIDI YA LEO
Tangazo hili naomba liingie ndani yako. Soma mfululizo huu kwa umakini, soma kanuni kumi kwa umakini, baada ya kusoma vitabu vingi vya watu waliofanikiwa, na kuona, na kusikia wengi waliofanikiwa, kupitia Biblia na kusoma watu waliofanikiwa, na maisha yangu binafsi; nimekuja kugundua kanuni hufanya kazi kwa yeyote pasipo kujali kabila lake, dini yake, taifa lake, rangi yake, umri wake, nchi anayotoka, elimu yake, na wote waliofanikiwa waliishi maisha ya kushindwa kwanza, ila walipoamua kufata kanuni maisha yao yalibadirika, na nilichogundua hawakutumia miaka au miezi, walitumia siku moja kama dhahabu inayotoka kwa Mungu kwa neema, inaitwa leo.
Kanuni zikiheshimiwa huleta mafanikio, zikivunjwa huleta kushindwa, uamuzi ni wako, kazi ya karama ya mwandishi ni kupokea toka kwa Roho Mtakatifu na kuandika kwa utiifu wote bila kupunguza, kazi ya msomaji ni kusoma, kuamini na kutendea kazi.
Mimi naanza kufanya jukumu langu.

Wote tunakubali tunaishi kwenye dunia inayokubari mabadiriko, dunia inabadirishwa na wachache, dunia yenye wengi wanaoshangaa na kuhadithia mafanikio ya wengine, wachache ndiyo wamiliki wa mali za dunia, wengi ni watumishi na wateja wa hawa wachache, nani kazaliwa na kitu, hapana; wao wamevipata wapi? Hapa hapa duniani, na sisi twaweza kuvipata wapi? Hapa hapa duniani
Nianze kusema wote tumeumbwa ili tuwe wamiliki
Jambo la kwanza alilolifanya Mungu alipomuumba Adamu ni kumpa umiliki, akamwambia "ukataware" kutawara ni umiliki, huwezi kutawara vitu ambavyo havipo chini yako, soma mwanzo 9:2 Baada ya wanadamu kukosea na Mungu kuwaangamiza kwa Ghalika, Mungu anafanya agano jipya na Nuhu na neno la kwanza ni kummilikisha vitu vyote duniani, Mungu amekupa umiliki, lakini ni kumiliki kwa niaba yake, Yeye bado atabaki Bwana yaani Adon kwa Kiebrania, yaani mmiliki kwa kiswahili, Yeye yupo juu ya vyote, ila amempa mwanadamu ataware kwa niaba yake
Swali kwanini humiliki, kwanini umekuwa mteja na mfanyakazi wa hili kundi dogo la mabepari,
Ipo kanuni ya kuondoka ulipo na kurudi namna ya Mungu alivyokuumba.

Wana wa Israel walifurahi kwenda Misri wakati nchi yao ilipokumbwa na njaa yaani Kanaani, Yusuph akawapokea, Mungu alikuwa ameshaagana na Ibrahimu kuwa atakipeleka kizazi chake Misri na kuwa watumwa kwa miaka 400 kisha atawaokoa na kuwarudisha kwenye nchi aliyomwahidi Ibrahimu.
Wana wa Israel moja ya vitu ambavyo hawawezi kusahau ni kuwa watumwa ndani ya Misri kwa mda wa zaidi ya miaka 400.

Mtumwa ni mtu ambaye hufanya kitu pasipo kutaka/ pasipo kuwa na matakwa yake. Mtumwa huenda asipotaka, hufanya kazi asiyotaka, hula chakula asichotaka, hulala mda asiyotaka, hupumzika mda asiyotaka, huishi maisha asiyotaka, hulala mahari asipotaka, huvaa nguo asizotaka; kuwa mtumwa ni heri ya kutozaliwa.

Wana wa Israel najua walifika wakati wakasema ni heri tusingezaliwa.
Mtu asiyekuwa katika kundi la wamiliki wa mali na uchumi wa dunia hii; yawezekana ukawa mmoja wa hao, atakula chakula asichokitaka, atavaa nguo asizozitaka, atafanya kazi mpaka mda asiyoutaka, atafanya kazi asiyoitaka, atalala mahari asipopataka, atanunua vitu asivyovitaka, atalala mahari asipopataka, ataishi maisha asiyoyataka, huu ni utumwa, wengine katika sayari hii wamekuwa ni mtumwa wa kiwango kidogo cha pesa walichonacho; "Pesa ndiyo jawabubla mambo yote"

Mara ngapi umeingia kwenye mtihani wa shule au chuo, umejiandaa kwa kusoma, kila kifaa unacho, peni, rula, na umevaa nguo za kupendeza: unaingia ndani ya chumba cha mtihani, unakaa vizuri kwenye kiti, unafunua karatasi ya mtihani, na kukuta kichwani una asilimia 30 ya yale yaliyoulizwa, kati ya maswali 20 unayajua maswali saba tu, ina maana asilimia 70 ya mtihani hujui. Wewe unadhani majibu hayapo ya maswali hayo, ukitaka kujua majibu yapo, tazama wa kulia kwako utamuona anajibu mtihani kwa tabasamu akionesha kuyajua yote;
"si kwamba pesa kama haijibu mambo yote unayoyahitaji kwamba imepoteza uwezo wake wa kujibu, ila ni kwamba unazo chache, umekusanya chache, umezipata chache.
Kushindwa kujibu maswali yote hakuna maana kichwa chako hakina uwezo wa kujibu; ila hayo saba ndiyo ambayo uliyasoma na kuyaweka kichwani, kichwa hakiwezi kujibu zaidi ya uliyoyaweka ndani yake wakati unajisomea, ukilazimisha utakosa tu.
Ndivyo pesa ilivyo; siyo kwamba haiwezi kujibu mambo yote unayotaka; tatizo ni kwamba hizo ndizo ulizotafuta, hizo ndizo ulizopata, hizo ndizo ulizonazo.
Kama wenzio wananunua vitu vya gharama ya Laki tano, ndizo walizokusanya, wewe nguo ya 3000 ndiyo uliyokusanya, na huwezi zidi hapo. Kanuni ndani ya kitabu hiki zinataka kuondoka na utumwa huu wa na kuwa mmiliki na uwe na pesa zenye jawabu la mambo yote.
Mungu amenipa kanuni hizi ili tu utoke ulipo na uwe na kesho yenye furaha na ushuhuda.

Mbali na hapo kuna watu ni watumwa wa hari zao za maisha, waweza kuwa tajiri lakini ni mtumwa wa ndoa, furaha, amani na huishi unavyotaka kuishi, huoni faida ya pesa yako katika maisha yako ya kawaida. Kanuni hizi zitagusa huko pia.
Na mfululizo huu ni maalumu kwa kila mtu, kama ni tajiri, mjasiliamari, muwejezaji, na yeyote, kama unayo leo, kitabu hiki kitakupa mwanga wa kufanya zaidi; kama unaishi bado waweza kufanya zaidi, soma mfululizo huu ili tumshinde adui wa kufanya zaidi ambaye ni mafanikio yako uliyonayo.

PART ONE
sehemu hii hasa tutaangalia msingi wa somo letu, maana ya siku tatu (leo, jana na kesho), pia tutaangalia watu tofauti jinsi walivyotumia leo yao, na tutazama makundi muhimu, hasa wale ambao leo yao, imesababishwa na historia, matukio au sababu fulani kama kukisa elimu, yatima, mjane, kilema, n.k

SEHEHEMU YA KWANZA
MSINGI WA NENO

KANUNI: kanuni ni imani na sheria ambazo mtu huziamini na kuzisimamia na kuzifanya mwongozo wa maisha yake.
Kanuni ni za asiri si za kubuni, kanuni zimefanikiwa kufanya kazi kila mahari kwasababu ni za asiri. Mwanadamu ameumbiwa, kuzifata si hiyari ni lazima, kanuni hazina jaji, usipofata zinakuhukumu zenyewe, hapa hapa duniani.
Yesu alisema, Mimi sitowahukumu ila maneno yangu ndiyo  yatakayowahukumu"
Nimewahi kuwa na rafiki yangu miaka ya 2005 mpaka 2008, alikuwa ni mtu anayefanya vizuri sana toka tukiwa shule ya msingi, tulipofika sekondari alifanya vema toka kidato cha kwanza mpaka cha pili na alikuwa mbere yangu kimasomo, nilishangaa kidato cha tatu akaanza kuwa nyuma yangu, nilipochunguza alikuwa amejenga mahusiano ya kimapenzi na binti fulani ambaye kwa pale shule alikuwa ana historia ya kutembea na wavulana wengi, nikamfata na kujaribu kumshauri lakini alinijibu kuwa "acha ushamba dogo" nilipomng'ang'aniza akanijibu kwa kebehi "niache, kwani haya si maisha yangu" nikamuacha ila siku ile ile nakumbuka hata mama yangu nilimshirikisha kuwa "rafiki yangu unayemjua amebadirika na sijui kama atafauru".

Ilikuwa ni rahisi kujua kuwa hawezi kufauru kidato cha nne hata kama si nabii, kwanini alienda kinyume na kanuni. Kanuni haziitaji hakimu wala jaji, bali zenyewe ni za asiri, unapovunja zinakuvunja.
Mfano usinywe sumu, usizini, usilewe, usinywe sumu, usiwe mvivu, hizi ni moja ya sheria za asiri, unapovunja haihitaji hakimu, zinakuvunja hapo hapo.
Kumbuka Yesu kasema, ni heri msingesikia, lakini sasa mmesikia hukumu i juu yenu.
Unapovunja kanuni, unatupa ruhusa ya kujua mwisho wako wa majuto, unapojitoa na kufata kanuni, unatupa furaha ya kujua mwisho wako mzuri.
Msingi wa kitabu hiki si kukupa mawazo, ila nataka upate kanuni.
Sihofu umesoma vitabu vingapi na ukabaki kama ulivyo, mimi najali kuwa, kwa kusoma mfululizo huu hutabaki kama ulivyo.
Na kwa waliofanikiwa naamini utafanya vizuri zaidi maadamu bado unayo leo.

Tuanze na mdano wa Mpakwa mafuta wa Bwana Mungu, kuwatoa Israel toka utumwani Misri kwenda Kanaani.
Anatoka kutoka maisha ya anasa ndani ya ikulu ya Farao mpaka kuwa masihi wa Bwana. Na kuandika vitabu vitano muhimu kwenye Biblia, Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na KumbuKumbu la Torati.

KUTOKA14:13-14
"Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. 14. Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

Maneno ya msingi ya kuyakumbuka kila unaposoma mfululizo wa somo hili ni:
• msiogope simameni tu
• mkaone wokovu
• Bwana atakaowafanyia
• Wamisri mliowaona leo
• hamtawaona Wamisri tena milele
• mtanyamaza kimya

Toka hapa tunapata maneno ya msingi;
Mafanikio hutokana na...
• uhusika wa Mungu (atawapigania)
• uhusika wetu (simameni)
• waleta utumwa (wamisri)
• utumwa (kutofanya unayopenda)
• mafanikio ni vita (atawapigania)
• kusonga mbere hata kama umetoka utumwani/umefanikiwa
• no retreat no surrender/ hakuna kurudi nyuma wala kunyosha mikono juu ya kushindwa.
• maisha yanahitaji kukubari kwa imani ya wengine juu yako na juu ya unachokifanya,. Musa ilimradhimu kuwashawishi kwa maneno ya imani wana wa Israel ili tu wakubali jambo analotaka kulifanya.
• Watu ndiyo wa muhimu sana katika jambo lolote unalotaka kulifanya. Ishi na watu vizuri, sema nao vema, chukuliana nao vizuri, ishi nao kwa hekima, uhakikishe unapata wengi wa kukuunga mkono,
 “ni ngumu kukupenda wote, ila tu unawahitaji watu sahihi”.
• muache Mungu afanye sehemu yake, na usingoje afanye sehemu yako.
• usimuingilie Mungu sehemu yake na usingoje aingilie sehemu yako.
• Mungu akisema 'nenda' wewe nenda.
• ukianza safari usifikiri kurudi nyuma/ ukiaga kwenu usirudi.

Pia tunajifunza namna ya kutumia tatizo na kulifanya kuwa baraka na siyo tatizo;
Huwa napenda kuwaambia INAWEZEKANA... watu walipita kwenye sehemu ya mkwamo wa kusonga mbere kufanya jambo ambalo kwa mda huo li juu ya uwezo wao (impossible).
Rafiki yangu wa karibu nikiwa mtoto Mama mmoja, siwezi kumsahau, mume wake alipomuacha, na kumuachia mtoto mchanga na kwenda kuowa msichana mwingine, mda mwingi nilimuona na tabasamu na mwenye maneno ya kufariji na si mwenye uhitaji wa faraja, ukienda kumfarini utaishia kufarijiwa wewe, alikuwa ni mtu aliyeumba kichwa chake kuwa tayari kujifariji na kukabiri haiwezekani kuwa inawezekana, sasa yupo Kenya ana maisha mazuri.

Tunajifunza nini toka kwa Musa aliibadiri "haiwezekani kuwa inawezekana” ndani ya fikra yake na ya team yake yaani wana wa Israel, na imani iliyochipuka ikaungana na nguvu za Mungu na bahari ikagawanyika.

“Imani ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na nguvu za Mungu”

1. Tambua tatizo mpaka hapo ulipo: Wamisri

2. Tambua kikwazo cha kufika unapotaka kufika: Bahari

3. Weka akiri zaidi kupata uhitaji, na uache kupoteza akiri kwenye tatizo, bali nini unataka; Musa alifikiri kuvuka ng'ambo si kurudi Misri.

4. Badiri fikra: ondoa hofu weka ujasiri

5. Tambua fikra za team yako na kuzishughulika: woga

6. Peleka akiri pa kupata usaidizi: Mungu

7. Tambua ushiriki wako, katika kuliondoa tatizo, ushiriki wa Mungu na wa timu yako: piga fimbo

8. Yakusanye matatizo yote na uyajue yote : Wamisri, Bahari, hofu yake na ya Waisrael, jangwa, hawana msaada.

9. Yatenge kwa utofauti wake na uyatatue kwa upekee wake: akaanza na Wana wa Israel kisha akaja Wamisri, akamalizia bahari, wakavuka.

10. Tengeneza mpango na mbinu nzuri ya kuyamaliza: Mungu akamtoa malaika aliyekuwa mbere yao na kumuweka nyuma, akaweza kiza kati ya Wamisri na mwanga kwa Israel ili kuwatenganisha.

11. Tembea katika imani huku ukimtazama Mungu; Musa alimwita Mungu na si mtu wa karibu, si Haruni wala Miriam, wala hakuanza kulia na kumueleza kila mtu.

12. Matatizo yasikufanye ukapunguza juhudi yako ya kusonga mbere: Musa hakupunguza munkari wa kwenda Kanaani, akaamnini Mungu atafanya lolote, saa yeyote.

13. Amini Fulsa, na jawabu inaweza kutokea saa yeyote na kwa namna yeyote: hawakufikiri kupasuka kwa bahari

14. Amini unaweza songa mbere zaidi: waliposikia wakapata moyo na nia, bahari ilipopasuka wakasonga mbere zaidi

15. Amini Mungu anaweza tokea mda wowote na kwa namna yeyote.

Alifanya kwa namna isiyoweza kufikilika kama angefanya vile, unaweza waza angeleta mtu alete maboti, au meri, au awauwe wa Wamisri kwa moto, hapana akawafanyia wasichofikiri.
Leo atafanya kwako. Kwa Jina la Yesu Kristo.

16. Weka suruhisho na siyo kukazana na ukubwa wa tatizo: Mungu alinishangaza hakuanza kuwakazia macho Wamisri, bali alikazia macho wao kusonga mbere, alikazia macho nini kinahitajika, na nini kifanyike wasonge mbele, hakutazama Wamisri.
Mungu akawapasulia njia, ndipo akawauwa Wamisri, kwa haraka utafikiri kwanini asingewauwa Wamisri, lakini alijua sasa akiwauwa, “enhee kwa wingi wao, wangepita wapi.
Leo hii Wamisri wanafananisha na utumwa wa pesa waliyokuwa nao wengi, na matatizo na changamoto nyingi ulizonazo.
Na kupasuka kuna maana ya usisimame ukaona umefika, bado hujammaliza adui, songa mbere, uhai wako, fulsa na nguvu ni kwamba bado unaweza songa mbere; shinda ugomvi wako na mafanikio uliyonayo ambayo yanakufanya usisonge mbere.

17: nini unahitaji kumaliza tatizo: Musa alihitaji fimbo ya kupiga maji yagawanyike. Na usiangalie mbali kwanza kupata kitu cha kumaliza tatizo, tazama kwanza nini unacho mkononi, nini unacho, kama ni kipawa, karama, au fedha kidogo, ndugu au rafiki wa karibu au watu sahihi. Tumia ulichonacho kwanza, na hivyo ulivyonavyo vitaleta unavyovihitaji kumaliza tatizo lako.
"Nyoka hatuanzi kummulika mbali, tunaanzia miguuni"

Tuendelee tena siku nyingine...
Karibu na ufurahie ufunuo wa siri za mbinguni kwa msaada wote wa Roho Mtakatifu.
Mungu awe nawe...

NAAMINI UMEBARIKIWA.
Bado tunaendelea
Fatana nami zaidi...

No comments:

Post a Comment