Monday, June 27, 2016

NGUVU NA MAMLAKA YA IMANI



NGUVU YA IMANI
                                                                                                                                                               
“hakuna kinachoshindikana kwa wale ambao bado wanaamini”
Mathayo 19:26
                                                                                               

Nguvu ni uwezo wa kitu kimoja kukifanya kitu kingine kufanya kitu pasipo kujali utayari wake. Imani ina nguvu ya kuamuru kitu chochote pasipo kujali wa hiko kitu. Imani ina nguvu ya kufanya chochote ambacho fikra za kibinaadamu hakiwezi kikawa kinawezekana, hata kama hiko kitu hakipo tayari. Yesu aliweza kufanya yote yaliyoshindikana na wanadamu, akayaamuru yatokee hata kama hayakutaka, hakuweza kufanya kitu pasipo imani. Je unataka kufanya makubwa zaidi ya aliyofanya Yesu, ni imani pekee inaweza kukufikisha huko. Nathubutu kusema kunena kwa lugha pasipo imani, hakuna litakalo tokea, kuomba kwa sauti au taratibu haisaidii, maana maneno ya kibinaadamu hayawezi kumfanya Yesu afanye lolote. Mungu ameipa nguvu imani tu pekee kuruhusu nguvu zake kutenda kazi.
“Ni Imani pekee ndiyo ina nguvu ya kuamuru kisichowezekana kiwezekane”
Nitoe mifano michache, Nguvu ya imani ndani ya Akida wa Kirumi (Luka 7:1-10), ijapokuwa hakuwa Myahudi wala hakuwa mtu wa dini ya aina yoyote ya Kiyahudi. Lakini imani yake ikaruhusu muuijiza juu yake. Mkumbuke yule mwanamke aliyetokwa na damu miaka 12, nguvu ya imani ndani yake ikaruhusu muujiza wake (Marko 5:25-34). Jambo la kushangaza hapo ni kiwango cha nguvu ya imani ndani yao. Mkuu wa Sinagogi Yairo ndiye alikuwa wa kwanza kumfata Yesu kuwa mwanae anaumwa hawezi yu karibu na kufa (Marko 5:2124), lakini mwanamke ndiye alikuwa wakwanza kupokea muujiza kabla hata ya Yairo. Kwanini kiwango cha imani ndani yetu. Yairo alikuwa na imani mwanae atapona akiguswa na Yesu, mwanamke akaenda mbali zaidi, akaamini kuwa akigusa tu, hata kama Yesu hajatamka neno, hata kama hatojua basi atapona, kumbuka aliwaza kugusa pindo na ni kweli aligusa pindo, yaani aliamini hata Yesu asipojua, ili mradi akigusa pindo la vazi lake tu. Je una imani namna gani?
“kiwango cha imani ndani yako ndiyo kinaamua kiwango cha muujiza unataka kupokea”
Imani ni kitu kisichoonekana lakini kina uhai na kina nguvu, ambayo hata mwanadamu hana. Imani ina nguvu zaidi hata ya nguvu za Mmarekani, Barack Obama alipomuua Osama Bin Laden alifikiri amemaliza kazi, lakini huwezi kuishinda imani kwa mtutu au kumuua kiongozi, sasa tunashuhudia kutokea kwa vikundi vya kigaidi zaidi na Al-kaida bado ipo. Kusambaratisha vyama pinzani kwa kutumia polisi bado hakuwezi kuishinda imani ndani ya vijana dhidi ya chama pinzani. Wengine wanajiripua na mabomu sababu ya kusimamia wanachokiamini. Karibu kila vita duniani chanzo chake ni imani, kama siyo imani ya dini basi ni imani ya kisiasa. Imani ina nguvu hatari sana na isiyozuirika. Kama kitu unachopaswa kuwa nacho ili kufanya yote ambao unaona yapo juu ya uwezo wako basi kuwa na imani.

No comments:

Post a Comment