Sunday, April 23, 2017

Kanuni Moja MUHIMU, Kumtafuta Mungu Nyakati Hizi.

KUMTAFUTA MUNGU KATIKA NYAKATI HIZI

Kanuni MUHIMU,  Mimi naona ni muhimu sana, kwa kila mtu kuijua na kuiweka moyoni, na kuifanyia kazi.

Nianze na kusema, Mungu alisema kwa wana wa Israel "Mtanitafuta na 'kuniona', mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote" Ye

maana ya "kumtafuta kwa moyo wote" ukiipata, ndiyo mwanzo wa kuanza kumtafuta Mungu kama Mungu anavyotaka, na utakuwa ndiyo mwanzo wa kumpata.

NI KAMA HIVI...
Kijana mmoja akamfata mzee tajiri na kumwambia "nataka kuwa tajiri kama wewe", Yule tajiri akamwambia tuonane kesho saa nne asubuhi ufukweni mwa bahari.
kijana akashangaa " kuna uhusiano gani kati ya kutaka utajiri na kwenda ufukweni"
Tajiri akamsisitiza "unataka utajiri, kesho saa nne asubuhi njoo Ufukweni"
Kesho kijana akafika ufukwe wa bahari akiwa amevaa suti amependeza saa nne asubuhi, Tajiri akamwambia "anza kupiga hatua kuingia ndani ya bahari". Kijana akaanza kupiga hatua, maji yakafika magotini, Maji yakafika mabegani, yakafika mdomoni, tajiri anazidi kumwambia aende. Maji yalipofika puani, anashindwa kuhema, kijana akatoka haraka majini,  akasema "huyu mzee ana kichaa". Mzee akamfata kwa haraka na kumshika kichwa na kumzamisha kichwa ndani ya maji_ Kijana akaanza kuhangaika ajitoe,

maana alikuwa anashindwa kuhema. Tajiri akaendelea kumkandamiza ndani ya maji. kwa mda baada ya kijana kuhangaika sana, akamtoa. Kisha akamuuliza "Je! Unapokuwa ndani ya maji, nini hasa unataka?"
Kijana akajibu "nataka kuhema"
Tajiri akamjibu "Hadi utakapofika wakati wa kutaka utajiri kama unavyotaka kuhema, hapo utakuwa tajiri"

NINI MAANA YAKE...
Tuhamishe hii hadithi kwetu watu wenye fikra tofauti na ulimwengu,  sisi tumeagizwa kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na mengine tutazidishiwa.

neno hili liki-ingia moyoni mwako,  KUMTAKA MUNGU KAMA UNAVYOTAKA PUMZI"

kati ya kitu muhimu sana kwetu ni pumzi, na tunahakikisha hatuipotezi_ na ndiyo HITAJI NAMBA MOJA KWETU.
Unapokuwa ndani ya maji, huwezi kutazama simu, TV, mama, Wala kumsikiliza mjomba, wala mume, au mke ila ni moja tu KUPATA KUHEMA..
Sidhani kama utakumbuka kula, au kuchati, kama unataka unatafuta pumzi, bali unachohitaji ni PUMZI TU.
UKIFIKA kumtaka Mungu namna hiyo_ Kuacha vyote na kushughurika na kumtaka kama unavyohitaji pumzi...
UTAKUWA UMEFIKA KUMTAKA KWA MOYO WOTE.

KANUNI YA PILI: Sema KANUNI namba 1 hata mara saba zaidi, asubuhi na jioni, mpaka uone inajisema yenyewe moyoni, hapo itakuwa imechukua maisha yako yote.
Sema nami
NIKIMTAKA MUNGU SANA KAMA NINAVYOTAKA KUHEMA NITAMPATA ZAIDI.
Ukifika kumtafuta Mungu, na kuona huwezi ishi pasipo Yeye, ukarudia kusema hata ikafika moyoni, itachukua moyo wako wote.
Jina la Bwana Libarikiwe

Contact: 0718721848

2 comments: