Sunday, November 27, 2016

UNAONAJE?

KUFIKIA UKAMILIFU WA KRISTO


Utofauti wa Mungu na wanadamu katika kuona vitu,
1. Mwanadamu anaona mwanzo kisha mwisho, Mungu anaona mwisho kisha anarudi mwanzo na kupanga namna ya kufika mwisho

2. Mwanadamu anaona nje na kuweka hitimisho, Mungu anatazama ndani kwanza kisha anafanya cha ndani kuonekana nje.

3. Mwanadamu anatazama pito/jaribu, Mungu anatazama matokeo ya pito.

4. Mwanadamu anatazama mwisho wa kitu Mungu anatazama baada ya mwisho.

5. Siku zote Mwisho wa mwanadamu ndiyo mwanzo wa Mungu

6. Ana heri yule ajuaye mawazo ya Mungu kuliko yule ajuaye matendo ya Mungu, ishara na miujuza ya Mungu
I.e ana heri yule amjuaye Mungu kuliko yule anayejua matendo ya Mungu.

7. Kila anayetaka kuwa hodari wa imani kwanza lazima ajue mawazo ya Mungu na Mungu mwenyewe

8. Imani huonekana tu mahari ambapo hapana majibu
Kama sehemu ina majibu hapo siyo imani

9. Imani ni kuamini kitu ambacho hujawai kuona kutokea.
Mfano wa Martha, kuamini mtu wa siku nne kufufuka, hajawahi ona, lakini Yesu alipomwambia Yeye ndiyo huo ufunguo aliamini.

10. Kufikia ukamilifu wa Kristo ni kufikia kwenye imani ya Kristo

11. Imani ni kufika wakati wa ulichosoma kwenye neno na kuhubiliwa unakuta ni tofauti kwenye maisha halisi unayopitia, na ukazidi kuamini, ukiamini kuwa aliyeahidi ni mwaminifu.

12. Mungu hufanya na huruhusu kila kitu kwa kusudi lake.

13. Mungu unayemtumikia kuna wakati hayupo kukuepusha usipate matatizo, mjaribu, kushindwa, udhaifu, na majaribu bali yupo ili akupitishe katika hayo kwaajili ya utukufu wake.

14. Unapaombiwa utukufu wa Mungu huonekana mwisho, si mwisho wa Mwanadamu, ni mwisho alioupanga Mungu, ambapo ni baada ya mwisho wa mwanadamu.

Usiogope unapopitia hayo, maana ni Mungu wako amekupitisha.
Kama ukitaka kuwa na Mungu anayekuepusha na majaribu basi 80% ya Biblia ilipaswa tuitoe, maana asilimia zaidi ya asilimia 80 ya Biblia ni hadithi za watu waliopitia mateso na majaribu, kuanzia mwanzo mpaka ufunuo
Na kipimo cha wewe kuwekwa kwenye Biblia ni kupitishwa kwenye majaribu, mateso na udhaifu
Written by
Ev. Ulenje

No comments:

Post a Comment