Monday, December 7, 2015

KUFIKIA UKAMILIFU WA YESU KRISTO

KUFIKIA UKAMILIFU WA KRISTO


Utofauti wa Mungu na wanadamu katika kuona vitu,
1. Mwanadamu anaona mwanzo kisha mwisho, Mungu anaona mwisho kisha anarudi mwanzo na kupanga namna ya kufika mwisho

2. Mwanadamu anaona nje na kuweka hitimisho, Mungu anatazama ndani kwanza kisha anafanya cha ndani kuonekana nje.

3. Mwanadamu anatazama kitu, Mungu anatazama matokeo ya kitu

4. Mwanadamu anatazama mwisho wa kitu Mungu anatazama baada ya mwisho.

5. Siku zote Mwisho wa mwanadamu ndiyo mwanzo wa Mungu

6. Ana heri yule ajuaye mawazo ya Mungu kuliko yule ajuaye matendo, ishara na miujuza ya Mungu
I.e ana heri yule amjuaye Mungu kuliko yule anayejua matendo ya Mungu.

7. Kila anayetaka kuwa hodari wa imani kwanza lazima ajue mawazo ya Mungu na Mungu mwenyewe

8. Imani huonekana tu mahari ambapo hapana majibu
Kama sehemu ina majibu hapo siyo imani

9. Imani ni kuamini kitu ambacho hujawai kuona kutokea.
Mfano wa Martha

10. Kufikia ukamilifu wa Kristo ni kufikia kwenye imani ya Kristo

11. Imani ni kufika wakati wa ulichosoma kwenye neno na kuhubiliwa unakuta ni tofauti kwenye maisha halisi

12. Mungu hufanya na huruhusu kila kitu kwa kusudi lake.

13. Mungu unayemtumikia hayupo kukuepusha usipate matatizo, mjaribu, kushindwa, udhaifu, na majaribu bali yupo ili akupitishe katika hayo kwaajili ya utukufu wake.

14. Unapombiwa utukufu wa Mungu huonekana mwisho, si mwisho wa Mwanadamu, ni mwisho alioupanga Mungu, ambapo ni baada ya mwisho wa mwanadamu.

Usiogope unapopitia hayo, maana ni Mungu wako amekupitisha.
Kama ukitaka kuwa na Mungu anayekuepusha na majaribu basi 80% ya Biblia ilipaswa tuitoe, maana asilimia zaidi ya asilimia 80 ya Biblia ni hadithi za watu waliopitia mateso na majaribu, kuanzia mwanzo mpaka ufunuo
Na kipimo cha wewe kuwekwa kwenye Biblia ni kupitishwa kwenye majaribu, mateso na udhaifu
Ibrahimu hazai
Mussa hajuo kuongea
Yakobo mwongo, mwizi
Esau mwoga wa njaa
Gideoni mwoga
Samson mdhaifu kwa wanawake
.......................

Yoh 16:33

Mara nyingi ndani ya ibada na makongamano mengi ya watu waliookoka tumekuwa tukifundishwa imani ya matendo ya Mungu
Yeye atafanya njia
Yeye atakuwa nawe
Yeye atakutetea
Ataponya nyumba yako
Hakuna uchawi wala uganga nyumba ya Israel
Atakuwa nawe daima
N.k

Lakini wengi tumeshangaa kuona tulichoamini na tunachokiona ni tofauti
Tulichosoma kwenye Biblia na kinachotokea kwenye maisha halisi ni tofauti
Tulichohubiliwa na tunachokiona ni tofauti

Unafika wakati
Familia uliyoamini inafunikwa na Mungu; mke anasumbua, mume anasumbua, mtoto anakuletea mimba
Ulivyoamini kuwa hatutakopa tutakopesha, unakuta ni tofauti, una madeni na mengine yanaongezeka

Uliamini hakuna uchawi juu ya Israel wala magonjwa ya kutisha, unashangaa anatoka kuumwa mume anakuja mtoto, usiku vita vya kichawi haviishi

Uliamini kutawara si kutawalia, unajikuta unatawaliwa na kuhama chini ya utawara wa bosi huyu na bosi huyu.

Uliamini kwa mikutano na kushuhudia na kulitangaza Jina la Yesu watu watajaa maelfu kwa maelfu kanisani unakuta katika maisha halisi hata mtoto haokoki na hata mtoto wako pia hajaokoka.

Leo tunaongelea imani ambayo unafika wakati hata neno uliloliamini halitokei
Mungu aliyemwamini humuoni
Mahubiri uliyoamini hayatokei

Maombi unaomba tena kwa kufanya kwa kujidhiki na kushirikisha na wengine lakini ndiyo kwanza mambo yanaongezeka kuwa magumu na majibu kutoonekana

Unaomba kwa ushahidi wa vifungu, lakini hakuna majibu

Imani wakati ambapo nini unaamini ni tofauti na unachoona katika maisha halisi.
..............................


Yesu anapowaaga wanafunzi wake,
Anaamua kuweka hitimisho/conclusion ya maisha yake yote toka anazaliwa mpaka anaenda kuteswa mpaka anapaa mbinguni, kwa kutumia sentensi moja tu

"Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu"

Luka 2:52 anamtambulisha Yesu tofauti na yeye anavyosema
Si kwamba alikosea Luka anamtambulisha Yesu wakati ana miaka 1-30

Luka anasema "naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu"

Katika umri wa miaka 1-30 Yesu akafurahia maisha yale, akaona ulimwengu huu mwema sana.

Hivyo ndivyo kwa wengi wetu, tulipozaliwa, wakati wa utoto tuliitazama dunia katika uwema sana, ukiamka asubuhi baba ameshaacha pesa ya kula shule nyumbani
Kitu kikiisha unasema tu mama au baba analeta
Ukaishi pasipo kujua ulimwengu halisi aliouongelea Yesu kwenye Yohana 16:33

Tambua kuna kuwa
1. NJE YA ULIMWENGU
2. Na kuwa NDANI YA ULIMWENGU

Wakati ule ulikuwa nje ya ulimwengu, wala ulikuwa hujui kinachowapata wazazi wako ndani ya ulimwengu

Wazazi Wakija sebureni wanacheka, unaona yes ngoja nikue kumbe maisha ni furaha, ukiongezeka umri unafurahi sana maana unatamani kufikia ukubwa kama wao ili ujitegemee.

Unapanda darasa na kumaliza shule unafurahi sana, unaolewa na kupata kazi unafurahi

Sasa mchezo unaanza unapotoka nje ya ulimwengu na kuingia ndani yake, na kukuta maisha ya ndani ya ulimwengu ni tofauti na ulivyokuwa unafikiri ukiwa mtoto kwa wazazi (nje ya ulimwengu)

Ulikuwa unasikia maisha magumu, sasa una yaishi hayo maisha.
Ulihadisiwa kuna kupitia majaribu sasa unapitia
Ulihadisiwa sana kwa habari za matatizo ya ndoa ya fulani na fulani na kuna wakati ukawaona wazembe sasa unapitia
Ukamuona mtu anafukuzwa kazi, ukasema mzembe, sasa unapitia

Ukamuona mtu hana kazi yuko nyumbani sasa unapitia

Ulikuwa ukiona tu baba anamfukuza mpangaji ukaona mpangaji mzembe anakunyimia fedha ya shule, leo ndiyo unaishi maisha ya kushindwa kulipa kodi

Hooooo
Unachanganyikiwa
Na kusema waoooh! This is the world

Yesu alipopitia maisha ya kukubaliwa, akawa akifurahi na kucheka na mama yake, na kuuliza je mkate si bora kuliko neno litokalo kwa Bwana?
Anakutana na Wakuu wa hekelu na kujadiri nao neno la Mungu akiwauliza maswali na wakimsifu sana.
Anafurahi kujenge meza na vitu na makochi akiwa seremara

Anafika miaka 30 na kuingia ndani ya ulimwenguni.

Anaona wao this is a world my mumy live?

Anaona walimu alioshiriki nao neno la Mungu hekaluni ndiyo hao hao anafika hekaluni wanamkataa

Watu walioona akiponya na kuwafanyia ishara na miujiza mbele yao ndiyo hao wanasema asurubiwe

Akaona waaooo! Kumbe nje ya ulimwengu ni tofauti na ndani ya ulimwengu.

Rafiki zako wa utotoni uliohisi watakutetea ndiyo hao watakusaidia mahakamani ndiyo hao wanasema afungwe, watu uliowahi hata kuwasaidia walipokuwa na shida leo kwako wanasema afungwe, watu walioona wema wako, leo wanasema mwongo mwizi huyo.

watu uliofikiri watakuwa ndiyo washirika wa kwanza kwenye kanisa ulilolianzisha, ndiyo hao wanakuwa wa kwanza kusema hukuitwa

Watu uliotegemea kukusaidia kutoka kimaisha leo wanasema hatuwezi, hata hawataki kuwa karibu na wewe.

Yesu anaona wanafunzi wake waliompenda sana na kumuita rabi, mfalme, na Mungu akawatambulisha ni mwanangu mpendwa, na kuwa naye mpaka kwenye dhiki na kuwafanyia miujiza baharini
Ndiyo hao hao wengine wanamsaliti, na wengine wanakimbia hawataki hata kuona anavyosurubiwa

Wanafunzi wengine waliomfata zaidi ya 15000 na kula mikate na samaki wa miujiza, hao ndiyo wa kwanza kupiga kerere msurubishe

Hii inatisha

Yesu anashangaa Baba yake yaani MUNGU BABA ambaye alipata kibari kwake na hata mara kadhaa akasema kuwa "Huyu Ni Mwanangu Mpendwa Msikilizeni Yeye" ambaye Yeye huwa tunategemea huonekana wakati wa mateso, hasa wakati ambapo tumechoka hatuna jibu, Yeye huleta jibu, huyo naye anafika katika hatima ya mwisho ya angalau kupata tumaini kwake au hata neno la kufariji, huyo naye anamuacha, Yesu akaseme "Eloi Eloi Lama Sabaktani"

"Ukifika wakati wa kukomazwa kiroho na Mungu, kuna wakati anakaa kimya ili kukufundisha imani ya kumtumaini na kumpenda Yeye na si vitu akupavyo"

Yesu anafika msalabani, hakuna tumaini tena ni kifo tu kinamngoja, anatazama kulia na kushoto haoni msaada zaidi ya mama yake tu analia, anaona kama hawa wameniacha sawa, anaamua kumtazama Baba yake juu

My God!!!!!!
Anaona afadhari hata ya hawa ambao wamejificha lakini angalau wanamuangalia, anamuona Baba yake amegeuza shingo hataki hata kumuangalia

Na kumbuka Yoh 16:31-32

Huyo ndiye Baba ambaye alijidai kwa wanafunzi wake na kuamini wakimuacha wao, Yeye  atakuwa naye

Huu ndiyo wakati wa kuonesha imani

Yesu anafikiwa Na wamama wanampa maji huku wakilia, Yesu anawatazama,

Tazama sasa baada ya Yeye kujionea huruma anawaonea huruma wao
WHY? Anatazama ikiwa Yeye Mungu na mwana wa Mungu na dunia imemuonesha dhiki namna ile, itakuwaje kwa mti mkavu. Twende pamoja usichukuzwe.

Yesu anawaambia msinililie mimi, mimi ndiyo naelekea mwisho na nikitoka mwisho naelekea upande wa pili wa ushindi na kuitwa mfalme wa wafalme
Jililieni ninyi na watoto wenu, ikiwa dunia wamenitenda mimi mti mbichi itakuwaje kwenu

Kwa maana nyingine Yesu anawaambia ndiyo mmenifata lakini kuna wakati mtaona mlichosikia na kuamini viko tofauti, mtaona dhiki, umasikini, uadui na kukataliwa

Yesu akiwa msalabani kwa machozi anaita Eloi Eloi Lama sabaktani, Mungu wangu mbona umeniacha

Yesu anafika wakati haoni jibu, anapanga kete na kupanga, weka mawazo na kuweka, panga na kupangua
Omba na machozi ya damu
Anatazama msaada wa wanafunzi wake haoni jibu, wote wamelala
Kuna wakati miimili ya kukusaidi watalala, watakuacha peke yako
Anarudi kuomba Mungu haji,

Luka 22:43-44 anasema akiwa katika dhiki, malaika akaja kumtia nguvu
Lakini baada ya uchungu kupotea, ndiyo kwanza unaongezeka baada ya machozi ya maji sasa machozi ya damu, anaomba na kuomba Baba amuepushie kikombe kile inashindikana, panga na kupangua

Alafu ebu fikiri, Yesu alikuwa anaomba kikombe kimuepuke, badala ya Mungu Baba kuepusha kikombe, eti anamtuma malaika aje kumtia nguvu. Lile halikuwa jibu Yesu aliloenda kuomba mwanzo, alitaka kikombe kimuepuke, malaika anakuja kumtia nguvu.

"Kuna wakati Mungu atataka upite jangwana ili akufundishe kitu, wakati huo hutohitaji kutoka, utahitaji kutiwa moyo, lengo ni umalize somo"

Yesu akasema "ikiwa ni mapenzi yako" wakati huo utahitaji kutiwa moyo na mapenzi ya Mungu lazima kutimia"

Je umewahi pitia jaribu, unaomba na kuomba Mungu alifanyie hata wepesi, unafika hata kufunga tatu mpaka nne kavu lakini wapi bora ungekula tu....
Ita na watu wanakusaidia kufunga, wanakushauri lakini wapi ndiyo kwanza linazidi come on... Machozi ya maji yanabadirika sasa unaamia kilio cha kwikwi moyo wako umekata tamaa

Unapanga kete hazipangiki, unapanga hazipangingi, shauriwa na kushauliwa kama wanakuchelewesha tu
Ita mke, marafiki, wachungaji hakuna msaada.

Hapo ndipo imani ninayoongelea hapa inatumika

Wakati ambapo Biblia inasema nitafanya mlango wa kutokea alafu ndiyo unaona hata dirisha dogo ulilokuwa unatazamia kupenya hapo nalo limefunga
Haleluya

Yesu alipoona hii ngoma nzito
Akaamua anyoshe mikono juu
Akasema kwa imani "Ee Baba ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu bali ni mapenzi yako yatendeka"

Nenda hapa utanielewa

Yoh 11:4
Yesu analetewa habari ya Lazaro kutoka kwa maumbu yake yaani Mariamu na Martha, Yesu anajibu tofauti na matarajio ya mwanadamu awaye yeyote duniani

Anawaambia "naye Yesu aliposikia, alisema Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwaajili ya utukufu wa Mungu, ili mwana wa Mungu atukuzwe"

Kumbuka Yesu ni mponyaji na Lazaro ni rafiki yake, na Lazaro anakujua kuwa Yesu ni mponyaji hivyo tu kujua kuwa ana taarifa ni faraja tosha.

lakini haendi

Cha kufurahisha hakuna aliyehoji, wala Martha hakuwatuma tena watu, wala hakuja mwenyewe
Lazaro rafiki yake Yesu aliyekuwa akishuudia Yesu akifufua wafu na kuponya viwete na kwa moyo wote akaamini

Leo Yesu anataka kumfundisha kumjua si kuona miujiza
Lazaro anaita msaada, lakini hauji mpaka anafika mwisho, anakufa

Najua umewahi kufika wakati, umemuita Bwana na kuona yu kimya hata unaoomba nao ukafika wakati ukawaambia Mungu amekaa kimya, pamoja na shutuma bado Mzee wa siku anakaa kimya
Nyumba unafukizwa, watoto wanarudi nyumbani, fedha ya kula tu ni tatizo, ada je
Unaomba sana, leo unazika huyu, kesho mwanao wa kike anakuletea mimba, na mtaa mzima wanajua ni mlokole na unajisifu kuhusu wokovu wa wanao
Yesu amekaa kimya

Nazungumzia imani ambayo hata wakati unaona mwisho wa mambo yote yenyewe bado inaamini, wewe siyo wa kwanza, kufika wakati kuchoka

Martha anafika wakati amechoka, Anamtazama Yesu, Yesu hatokei, anajipa moyo
Mwisho anaona ndugu yake hawezi kabisa na mwili unaacha roho, ohooo hapo ndipo anachoka na kuona sasa imekwisha

Najua umewahi fika wakati huo, wakati ambao unaamini na umesoma kwenye Biblia ndiyo wakati wa Bwana kutokea
Unaona ndiyo kwanza hata maombi hayana uwepo wake, ni makavu kama hujaokoka
Unajiona labda una dhambi, unaanza kutubu, yote pia ni kama unasema hewani
Hiyo ndiyo imani ninayoiongelea hapa

Lazaro amekufa, Martha anawaza Yesu atakuja kumfufua, mpaka wanazika haji
Come on, je bado unayo imani? Unapofika nyakati hizi.

Martha anakata tamaa, wanamzika Lazaro
Martha amekwisha, tatizo sasa ni basi
Yesu ndipo anatokea
Martha anamwambia Bwana umechelewa kuja mtoto ameshafukuzwa shule,

mke wako ndiyo amepinda tayari asikii wala haambiliki, amesharudi kwao tayari, hata kitanda kila mtu na chake
Anaumwa kabaki mifupa
Biashara na fremu tumesharudisha
Chumba na vyombo tulitoa nje hukuja, sasa na kuuza tumeuza vyote tumerudi kwa wazazi kuomba hifadhi, kama ni aibu tumeshaipata
Wakati alisema atatufichia aibu, ni masikini tayari, na huduma nimeshaacha, chuo nimesha Disco, sina ada; Yesu ndiyo unakuja, umeshachelewa.

Je umewahi pita wakati Yesu anakuja kujibu maombi yako too late (ameshachelewa) na ulivyotarajia.

Yesu anamwambia

"Sikukwambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu".

Naongelea imani ambayo, bado unaamini wakati uliyosoma kwenye Biblia ni tofauti na unavyoona kwenye maisha halisi

Yesu alikuwa anataka Martha asiishie kumpima Yesu kwa vilema na viwete na wafu waliokufa asubuhi mchana anawafufua, alitaka asimpime katika ufufuo wa wafu pekee katika siku ya mwisho, kuna kiwango cha imani alitaka kumpeleka.

Jiulize Kiwango gani Mungu anataka kukupeleka?

Ipo level ambayo unamwamini Mungu, mruhusu Mungu akuonesha anaweza fanya zaidi ya hapo ulipo, zaidi ya aliyowahi kukufanyia, muache akuoneshe anaweza zaidi ya ulivyoona zaidi ya ulivyoamini.

Alitaka ajue Utukufu wa Mungu ni mkuu sana pale ambapo hakuna majibu, pale ambapo akiri za mwanadamu haziwezi endelea mbele tena. Anachoka

"Lolote linafanyika kwako ni kwa utukufu wa Mungu, ambao huonekana baada ya kufika mwisho"

Lazaro anateseka, Martha analia, kumbe Mungu anajua mwisho wa jambo kabla hata ya mwanzo na ameweka kwa utukufu wake.

Yesu anapotazama, mateso na machozi yale anakumbuka kuwa Baba yake huwa anatenda mwisho wa akili za wanadamu.

"Unapombiwa utukufu wa Mungu huonekana mwisho, si mwisho wa Mwanadamu, ni mwisho alioupanga Mungu, ambapo ni baada ya mwisho wa mwanadamu.

Yesu ananyosha mikono juu
Na kusema ikiwa ni mapenzi yako na yatendeke

Na hii ndiyo imani
Wakati ambao huna majibu ya mambo unayopitia,

kama kweli una imani na Mungu na si kanisa, si mchungaji
Unaona marafiki, washirika, ndugu na wote wamesimama kushoto wanakutaza na hawana msaada kwako wowote huo ndiyo wakati wa kuonesha imani yako
Wakati wa Kuacha Mapenzi ya Mungu na yatendeke

Biblia inasema katika
Ebrania 12:1-3

"Yesu kwajili ya furaha aliyowekewa mbele aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu"

Hivyo tunapoongelea ukamilifu wa Kristo tunaongelea pale mtu anapofika wakati hayatazami mateso yake, hatazami kushindwa, hatazami kukataliwa, bali anatazama furaha iliyoko mbele yake, furaha iliyo ndani ya jaribu hilo

Hivyo imani ni kutazama ya mbele na kuyafumbia macho ya sasa hata kama Mbele imefunikwa na kiza kinene, haionekani, inaona ulipo ndiyo mwisho
Uko tayari hata kufa hivyo hivyo ulivyo

"Imani ni kupika hatua pale ambapo huoni mwisho wa ngazi" Martin Luther King Jr

Na ukayafumbia macho na kutazama mbele, kwa kutokuitazama aibu ya sasa, hiyo ndiyo imani na ndiyo iliyokamilifu katika Kristo

1. Naongelea wakati ambao Yakobo amechoka, na Mbingu zinafunuka na kugundua kumbe pale alipo kuna Mungu
Wakati ambao katika hari ya kushindikana kabisa, na kuona Mungu amekuacha, unakuja kugundua kumbe Mungu yupo hapo ulipo

2. Wakati ambapo imani yako inagoma kuamini, na inakuradhimu kuanza kushindana na imani yako
1 Timothy 6:12
Imani yako inagoma kuamini, lakini wewe unashindana nayo na kuishinda mpaka inaamini

3. Wakati wa kutazama mwisho na kuona furaha uliyowekewa mbele kisha kurudi mwanzo na kuona unatokaje ulipo

4. Ni wakati wa kuwa na subira na saburi na kusubiri kuyaona mapenzi ya Baba wa Mbinguni
Huu ndiyo ukamilifu wa Kristo

Waooooo

Mungu alibariki neno lake
Kristo neema yako iwe nawe
Roho mtakatifu awe ushirika nawe unaposoma ujumbe huu
Mungu uwe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja nami katika kuandaa ujumbe huu, kuufundisha makanisa kadhaa na leo kuuandika kwako.


From the Holy Spirit
Written by Ev. Ulenje Mwaipungu.

No comments:

Post a Comment