Thursday, December 31, 2015

2016 BWANA ANAKUWAZIA MEMA, WEWE JE?

WEKA ALAMA, JENGA JINA JEMA KATIKA UFALME WA MUNGU.

2016 ndiyo hii,
Mengi twaweza kuyafikiri kuyafanya, katika mwaka ujao.
Jambo la kufikiri, mwaka unapoisha, utakuwa umefanya jambo watu watazame au utakuwa unatazama watu waliyofanya.

Maana kuna watu hupokea mwaka kwa kufurahi kuongeza umri na wengine hutazama nini wamefanya.

Mfano: mtu mmoja alienda kwenye duka wanalouza ubongo. Muuzaji akamwambia kuna aina nne za ubongo. Akaanza kumuonesha aina:
Akamuonesha aina ya kwanza, ni bongo waliyofanikiwa kugundua Satelite, ndege, na magari, akamuonesha aina ya pili, ni wale waliyofanikiwa kugundua radio, simu, na television, akamuonesha aina ya tatu waliyofanikiwa kugundua kutengeneza majumba ya kufahari, madaraja na hoteri za kisasa, akamuonesha ubongo aina ya nne, ambao wao hawajafanikiwa kugundua chochote, wao hata kujenga vyoo vy ikulu huwaita watu toka nje kuwajengea
Mnunuzi akauliza bei, na kuambiwa bongo za kwanza mpaka namba tatu ni bei rahisi sana, ila ubongo wa mwisho ni aghari sana huwezi kununua, mnunuzi akashangaa inawezekanaje ubongo ambao hawajafanya chochote kuwa aghari zaidi ya bongo waliyofanya vitu vikubwa.
Akamwambia huu ubongo una uwezo mkubwa ndani yake, ambao bado haujatumika.

Mwanzo wa somo:
Dr Myles Munroe aliwahi sema, mari na utajiri haupo kwenye migodi, wala haupo kwenye visima vya mafuta.
Bali utajiri upo karibu na nyumba yako, utajiri upo kwenye makaburi.
Mungu akiyatazama makaburi anahuzunika, maana anaona nyimbo ambazo hazitoweza kuimbwa tena, anaona mahubiri hayatoweza kuhubiriwa tena, anaona vitabu havitaweza kuandikwa tena, anaona sadaka zilizo bank hazitoweza jenga makanisa tena, anaona vipawa havitaweza kutumika tena, anaona karama hazitaweza kutumiwa tena.
Hamu ya Mungu ni kuona kila mtu aliyemuumba na kumuokoa anafanya kazi aliyomuumba kuifanya.
Na ufahari wa Mungu ni pale mtu aliyemuumba na kumuokoa anafanya kazi aliyomuumba kuifanya.
Fahari ya Toyota inapofanya kazi kwa mtengeneza toyota, na toyota inakuwa na jina jema inapofanya kazi iliyoumbiwa kuifanya.
Vivyo hivyo na fahari ya simu inapofanya kazi, ni kwa mtengeneza simu, na simu hujenga jina jema pale inapofanya kazi iliyotengenezwa kuifanya.
Fahari ya Mungu ni pale bidhaa aliyoitengeneza inafanya kazi, aliyoiumba kufanya. Na jina jema hutengenezwa na mtu pale anapofanya kazi aliyoumbiwa kuifanya.

Mithari 22:1
Mhubiri 7:1
Sulemani anasema ni heri siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
Watu wanaogopa hasa siku ya kufa. Na siku ya kuzaliwa huwa ni siku ya sherehe kwa kila mtu, watu hufurahi na kufanya na sherehe, lakini Suremani anasema hiyo siku si heri. Siku ya msiba watu wanalia na kuomboleza, Sulemani anasema hiyo siku ndiyo heri. Hapa kuna kitu Sulemani anajua sisi hatujui.
Paulo alipofika wakati wa kufa kwake, akasema vita nimevipiga mwendo nimeumaliza na imani nimeilinda, anasema mwendo ameumaliza. Hakuogopa kufa kwasababu alijua mwendo ameumaliza: kazi ameimaliza.
Yesu hakuogopa kufa, hata akasema imekwisha, kwanini hakuogopa kufa, sababu alijua kazi yake ameimaliza.
Ukiona kazi umeimaliza, kufa inakuwa ni sawa na kuingia ndani ya chumba, unahamia sehemu nyingine.

Kitu cha kwanza kwa mtoto kukishika ni jina lake, hata kama atakuwa hajui kuona au kuongea, hata kutambaa, mama atamrazimisha alijue jina lake, kwa kumuita kila wakati.
Hata akifika shule, ni ufahari kwa walimu na wazazi wanapoona mtoto wao anajua kuandika jina lake. Hii inanipa kukua kuwa jina lina umuhimu sana.
Nilipokuwa utotoni nilidhani maana ya jina ni herufi, kama I. M. A. N. U. E. L na kujua kuwa ni kutoka na jina lilipotokea mfano Mungu pamoja nasi kwa jina la Imanuel, ila baada ya kusoma vitabu, Biblia, kusikiliza mahubiri na maisha binafsi nikaja kugundua maana ya jina ni zaidi ya nilivyofikiri.
Kuna watu wenye majina mazuri kama John, Jane, Petro, Happy, Precious, Michael, wanakosa kazi na watu wenye majina kama Mwantumu, Mboneghe, Nailejileji, wanapata kazi.
Nikagundua maana ya jina inatokana na alama uliyoweka.

Kwanini watu wanapenda majina kama Mathayo, Petro, Yohana, Daudi, Sarah, prisca, Rahabu, au Mary.

Kwanini wasiwape watoto wao majina kama Goliath, Ahabu, Yezebeli, Nebukadreza, Pilato, Herode, Iddi Amini, Senokarebu au Mabutu
Kutokana na alama waliyoweka.

Mtu aliyeweza kufanikiwa kutumia kiasi kikubwa cha ubongo kuliko wanadamu wote Albert Eastern aliwahi sema "Jaribu kuwa siyo mtu wa mafanikio, bali mtu wa thamani...maisha yanayo ishi kwa ajili ya wengine ndiyo maisha ya thamani"

Matendo na utumishi wa mtu ndiyo hujenga alama, na alama inajenga jina.
Kwahiyo; alama ya mtu inajengwa kutokana na matendo aliyofanya na utumishi aliyotumika.

Mfano Luka 7:1-5.
Akida Mrumi, aliyepatwa na tatizo la mtumwa wake kuumwa. Alipowatuma wazee kwenda kumuomba Yesu amponye mtumwa wake, wale wazee wakamwambia Yesu, "amestahili mtu huyu kutendewa jambo hili, maana analipenda taifa letu, ametujengea na hekalu".

NAMNA YA KUWEKA ALAMA, ILI KUJENGA JINA JEMA KATIKA UFALME WA MUNGU.
Ziko njia nyingi, ila leo tuongelee utumishi.
1. Tambua maono ya kanisa, na ujiunganishe nayo.
Maono ni kuona mbere kwa hekima. Nini kanisa au mchungaji anatamani kufika, au anatamani kanisa lifike. Kuna maono ya mda mfupi na ya mda mrefu, jiunganishe nayo kuhakikisha yanatimia.
Usipotambua maono ya kanisa utajitafutia mambo yako mwenyewe, utatumika, na kuishia kufanya mambo yanayoonekana hayana maana.

2. Tambua wewe ni nani, Kwanini uko hapo, na Unaweza kufanya nini.
Usipojua wewe ni nani utajitumia vibaya. Utafanya yasiyo yako.
Usipojua kwanini uko hapo; utapoteza mda na usifanye ulichopaswa kufanya, na hautofurahia maisha ya kuwa hapo.
Usipojua unaweza kufanya nini; utajaribu kufanya kila kitu, na kujikuta mpaka siku yako yako ya kufa, bado hujafanya chochote.

3. Kuwa chanzo cha mabadiriko:
Kuna watu kanisani ni waanzisha mabadiriko, na wengine washangaa mabadiriko.
Wanaoshangaa mabadiriko hawatengenezi jina, wanaosababisha mabadiriko, huweka alama na kujenga jina jema.

4. Kuwa sababu ya suruhisho la matatizo kanisani.
Kuna watu kanisani husababisha matatizo, hujenga jina baya na wengine ni suruhisho la matatizo; hujenga jina jema.
Kumbuka kushindwa kutoa suruhisho na wewe unakuwa tatizo.
Kama tatizo ni keyboard kanisani na washirika hawawi suruhisho la kupatikana na wao wanakuwa tatizo. Wataitwa washirika wasiyotoa michango. Wanakuwa tatizo kwa mchungaji, akijiuliza awafanyaje ili watoe.

5. Jitoe sadaka: kuwa wa kujitolea
Wakisema tunahitaji mtu, usiwe mtu wa kurudi nyuma, songa mbele, wanaosonga mbele hujenga majina mema, wanaorudi nyuma hawajengi majina.
Filipi 1:23.

6. Ishi kwa ajili ya wengine: Jitoe kwa ajili ya wengine.
Fanya kuona wengine wananufaika
2 Timotheo 2:10
Kuwa sababu ya wengine kufurahia ibada.

7. Usisubiri fanya (Just Do It)
Kampuni ya Nike mwaka wa 1988 January ilikuwa na utajiri wa dola milioni 177 lakini kwa kuanzisha neno la Just Do It ikawafanya mwenzi December kuwa na utajiri wa dola bilioni 9.2 sawa na tilioni 18.4 za kitanzania.
Kuna siri ndani ya neno; fanya usisubiri.
Wale wanaoona kitu na kufanya bila kusubiri wengine watafanya hujenga majina mema, ila wale wanaosema fulani atafanya hujenga majina mabaya.

8. Tafuta sehemu sahihi na ujenge jina hapo.
Kama ni kusafisha kanisa, kutoa, kufuta viti, kumtumza mchungaji, kutembelea watu, injili au kufundisha.

9. Kuwa mtu wa maono
Mtu wa maono ni mtu anayewafanya wengine kuona. Wakati wengine wanasema haiwezekani, yeye husema hebu tujaribu hivi, inawezekana.

10. Jenga tabia njema
Tabia ni wewe halisi, ni wewe nje ya ibada, nje ya madhabahu. Unafanya nini unapokuwa peke yako, unafanya nini ukifanikiwa au tukikupa cheo.
Tabia ina nguvu kuliko kipawa chako, kuliko karama au huduma.

11. Kuwa mtu wa kusadiki.
Mtu anayesadiki ni mtu anayeamini kitu kinawezekana na kushikiria kitu mpaka kinafanikiwa. Ni mtu anayeweza kuhangaikia maono ya kanisa zaidi hata ya mchungaji.

12. Tengeneza uhusiano mzuri na wengine
Tuwe furaha kwa watu wengine katika utendaji kazi.
Kuna baadhi ya kazi na maono ya kanisa huonekana ni magumu, si kwamba ni maono au kazi ngumu bali kuna tu fulani yupo.

13. Kuwa mtendaji kazi na si mfanyakazi.
Kuna mtumishi na anayetumika
Mtumishi yeye utumishi na utenda kazi upo moyoni.
Mtumishi anapotumika hufanya kwa moyo, na ni mtii hata kama mchungaji hayupo, hata kama hajatumwa, hata kama hakuna ujira, hakuna sifa alizopewa, hatazami aliyoyafanya, bali hutazama nini anapaswa kufanya.
Mfanyakazi: yeye kazi haipo moyoni, hufanya ili apate sifa, ujira au zawadi, hukwazika asiposifiwa, hukwazika akifanya peke yake, hukwazika akitoka kufanya kazi moja na kuambiwa afanye nyingine, hukwazika akikwazwa kazini, hupenda kuonekana afanyapo, si mti kiongozi asipokuwepo.

FAIDA ZA KUWEKA JINA JEMA.
1. Jina jema ni zaidi ya pesa na mali nyingi.
Maana pesa na mali huwa na kikomo, lakini jina jema hufungua milango na fulsa zaidi.

2. Jina jema hufungua mlango na kukupa kibari.
Kibari ni mlango uliyofunguka na kupitisha baraka.
Kibari huwavuta watu wa thamani kwako, kibari huvuta mafanikio na kuongeza thamani yako.
Mfano Yusuph na Daudi walipata kibari.

3. Hukupa ulinzi
Jina jema linakulinda, kila mtu atakuwa ni shahidi yako, kila mtu atapenda usishindwe na kanisa litahangaika unaposhindwa. Utakuwa kidonda kwa mchungaji, atakuita mwanae.

4. Hutakufa hakika.
Mtu mwenye jina jema kama Paulo hawezi kufa, huwezi kuhubiri injili na ujumbe uka kamilika pasipo kuchukua toka kwenye injili ya Paulo.

5. Kufanikiwa katika utumishi mdogo hukupa kufanikiwa katika utumishi mkubwa.
Hata leo unapowaona watumishi wakubwa, walianza kufanikiwa katika utumishi mdogo.

Kuna mifano ya watu waliyotumika na hawakuwa na vyeo kwenye kanisa la kwanza, maana kuna watu huamini kuwa kutumika mpaka uwe na cheo.

1. Epafra (mtu niliyempenda sana)
Huyu anapatikana kwenye kutabu cha Kolosai 4:12
Nimemuweka namba moja, kwasababu aliwabebea wenzake, na hakuna aliyemuona wakati huo, ila Paulo akaitambua huduma yake, na kuona wengine walistahimili na kuimarika kwa sababu yake.

2. Prisca na Akila.
Luka aliwandika kama Priscila na Akila kwenye kitabu cha matendo. Hawa walikuwa wakitumia pesa zao kusaidia huduma ya Paulo, walitumia nyumba zao kufundisha watu  Kristo, pale Paulo alipoenda kuhubiri injili. Na ndiyo wakiyotumiwa na na Paulo kuuza mahema aliyokuwa akiyatengeneza.

3. Luka tabibu. Huyu alitembea na Paulo popote alipoenda akiandika nini kinatukia na nini Paulo anasema.

4. Sira: aliyetembea na Paulo sehemu nyingi hata kukubali kufunga na Paulo.

5. Timotheo: kijana aliyekutwa Listra, Paulo na Sira walipo ona utumishi wake japo kuwa alikuwa ni kijana mdogo sana na baba yake hakuwa Myahudi, alikuwa na Myunani, Paulo akampenda, wazee wakamwekea mikono, akamtahiri kuogopa Wayahudi, na kuanza kutembea naye katika huduma.

6. Kreske, Tito, Tikiko, Karpo, Erasto, Trofimo, Eubulo, Pude, Lino, Klaudia: wengi kati ya hawa Paulo aliwa anzishia makanisa baaye.

7. Marko: paulo alisema kuwa anamfa sana.

NB: BADO WEWE... Chukua hatua, Inuka, Tumika, weka alama, Jenga jina jema.

MWISHO: Moja ya vitu ambavyo wapendwa wengi waliyofanikiwa kuwepo miaka ya 70 na 80, huwa vinawasikitisha ni mabadiriko ya kanisa.
Kanisa limebadirika
• tupo katika zama ambazo mabadiriko hatari yametokea kanisani
• utumishi umekuwa mtaji wa maisha
• karama za roho mtakatifu nyingi hazionekani
• huduma zimekuwa ni biashara
• sasa makanisani kuna utumishi wa matajiri na masikini. Mtu akishafanikiwa kuna baadhi ya kazi kanisani hafanyi tena.
• watu wanajenga majumba yao zaidi ya moja, na kuacha nyumba ya Bwana katika aibu.
• maombi yamekuwa ni ya watu fulani kanisani hasa wazee na wenye shida.
• mrundikano wa vijana kulima shamba la kanisa haupo tena, sasa  wachungaji ndiyo watumishi wa kazi zote.
• sadaka imekuwa ni ibada ya ziada.
• watu wanataka kuonekana na si kutumika.

Kama bahari inaweza kuhamisha vitu vyote ila si jiwe. Ni vyema wakati kanisa linabadirika, wewe usimame imara, kuweka alama na kujenga jina jema katika ufalme wa Mungu.

Kwa msaada wa Roho mtakatifu somo limeandaliwa na
ULENJE (Emanuel) MWAIPUNGU.

No comments:

Post a Comment