Tuesday, November 17, 2015

SEHEMU YA TATU: BARAKA TANO ZA PETRO

SEHEMU YA TATU
BARAKA TANO ZA PETRO

JINSI PETRO ALIVYOTUMIA LEO.

Leo tuangalie kiundani kuhusu Petro na uhusika wake katika maisha ya Yesu akiwa duniani. Na pia tuone namna Petro alivyoweza kutumia leo yake aliyopewa na Mungu kwa neema. Na tuone namna alipotoka na namna alivyoweza kubadiri maisha yake na namna alivyoweza kuendana na baraka alizopewa hata zikaweza kutimia.

UHUSIKA WA PETRO

Petro alikuwa Ni mwanafunzi machachari na mchangamfu, nahisi alikuwa ni mtu muongeaji, mtu wa kucheka na tabasanu mda wote, mwenye siasa kidogo, mcheshi na muoga, mwenye silka kubwa ya uongozi, kiherehere, na mtu ambaye hutochoka kukaa naye, ila utachoka tu kumsikiliza maana anaonekana alikuwa ni bingwa wa kuongea.

Petro katika maisha yake anakuja kupewa baraka tano na Bwana Yesu, ila kuzifikia, kuna kazi ilimbidi afanye, alipitia maisha ya kupatia na kukosea.
Petro hakuwa mwanafunzi aliyekuwa namba moja kwa ukaribu na Kristo lakini alifanikiwa katika kupata baraka nyingi ukisoma vitabu vya injili. Hivyo anatupa fulsa sisi ya kumchambua na kutusaidia kujua tunawezaje kujifunza toka kwake.

MAMBO YA MSINGI KUJUA KUHUSA PETRO
1. Petro alikuwa ni mvuvi, masikini, mwenye dhambi, alikuwa chini ya ukoloni wa Kirumi, na maisha yake aliyatumia kuvua samaki na si kukaa na familia.

2. Petro alikuwa alikuwa ni mtu wa kutochoka kujaribu: mda mwingi alisema linalotoka moyoni kujibu maswali ya Yesu na kuchangia mada za Yesu, kuna wakati akapatia na kuna wakati alikosea, lakini hakuchoka kujaribu tena na tena hata alipozuiwa, hakuacha.

3. Alikuwa muoga, ila aliyejitahidi kuushinda uoga wake, hata wakati aliposhindwa alijaribu tena; aliogopa kusema kuwa yeye ni wa Yesu, kuogopa kupigwa kama Yesu, lakini Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo walipoleta taarifa ya kufufuka kwa Yesu, mitume wengine wakaona ni upuuzi yeye hakusita kuwa wakwanza kwenda kuona bila kujari kuwa alikuwa anaenda kwa mtu aliyemkana, siku waliposhukiwa na Roho Mtakatifu akawa wakwanza kusema kati ya wanafunzi 120 waliyobaki, siku zote alipambana na hofu yake, aibu, na woga wake.

4. Alikuwa tayari kufa kwaajili ya wengine, alikuwa tayari kufa ili tu injili iwafikie na wengine. Alikuwa tayari kupambana ili kumuokoa Kristo asiteswe na Wayahudi na kufa japo haikuwa sahihi kufanya hivyo. Alikuwa tayari kufika mpaka lango la behewa ya kuhani mkuu kuona Yesu anafanywa nini na makuhani.

5. Petro alikuwa ni mwenye njaa na kiu ya haki: alipoona Eliya na. Musa wanazungumza na Yesu akaona hapa ndipo pa kukaa, akamwambia Yesu "...Bwana Mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa na kimoja cha Eliya" hali hajui asemalo. Japo alikuwa hajui asemalo lakini alionesha kiu na ufalme wa Mungu, kiu na kukaa penye dirisha la mbinguni. Na kwa hapo Yesu akambariki.
Petro aliacha vyote na kumfata Yesu, hata alipofanywa kuwa kiongozi wa makanisa yote hapo Uyahudi bado alizidi kuifanya kazi ya Mungu na kuutafuta ufalme wake.

6. Alisimamia anachokiamini kwa gharama yeyote; hata walipomshawishi kuwa aache kulihubiri Jina la Yesu, bado alisimama pamoja na Yohana na kuwaambia "...ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe, maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Mdo 4:19-20

7. Alikuwa mtu wa kutazama leo; Petro hata wakati alipokosea, alichukua kuwa hilo ni kosa la jana, akawa analisahihisha na kusonga mbele, kiukweli Petro alikuwa ni mtu wa kukosea sana, ila alikuwa ni mtu mwenye kutumia sana fulsa. Petro alipoambiwa na Yesu "rudi nyuma ewe shetani" Yoh 18:10, ndiye huyo huyo anakuja kumwambia nipo "tayari kwenda na wewe gerezani" Luka 22:33, Yesu anamwambia utanikana mara tatu, Petro hakusita kwenda naye kwenye maombi, aliposinzia na kuamshwa mara kadhaa, hakusita kunyanyua upanga na kumkata sikio la kuume mtumwa mmoja wapo wa kuhani mkuu, Yesu anamsahihisha, hakukosa kwenda naye mpaka malangoni mwa behewa ya kuhani mkuu, na huko alipomsaliti, pia hakusita kuomba msamaha, na kuwa mwanafunzi wa kwanza kufika kaburini kuhakiki kufufuka kwa Yesu na kuonana na Yesu kati ya wale mitume 11 waliobaki. Siku zote alitazama “maadamu ni hai, naweza kusahihisha na nikafanya kitu chema, kikafuta baya la jana na kunifanya kuwa mtu wa muhimu, mafanikio na mwenye kibari”.

8. Petro aliwaza chanya siku zote; siku zote alipoona fulsa imetokea, akaishinda hasi na kuweka chanya, alipoona Yesu amesema, ikawa ni fulsa, akaamini inawezekana, alipoambiwa kavue samaki wa kwanza atatoa pesa, japo hakuwahi ona kitendo hiko toka azaliwe, akaamini akaenda, alipoambiwa habari za wokovu kwa mataifa katika maono, Wayahudi wengine ilichukua miaka na miaka, lakini yeye aliamini saa hiyo hiyo alipoambiwa na Mungu, aliwaza chanya siku zote, hakutamani kubakiwa na hasi, aliiweka hasi ya jana, na kuwaza positive.

9. Petro aliamini anapohusika Mungu yote yanawezekana: Petro alipoambiwa shusha nyavu, hakuuliza mara mbiri "...kwa neno lako nitashusha nyavu" akashusha, alipoambiwa kavue samaki utapata pesa, haraka akaenda, Roho Mtakatifu alipowashukia, saa hiyo hiyo akaanza kuzungumza kwa ujasiri watu watubu, alipomuona kirema akiomba omba, hakutaka kuambiwa sasa unaweza kuponya, akafanya muujiza.

10. Alikuwa na roho kubwa ya uongozi. Petro alikuwa na roho ya kuongoza, najua kuwa kila mtu ana silka ya uongozi ila Petro alikuwa na roho ya uongozi, hii roho kila mtu huzaliwa nayo, ila ni jukumu la mtu binafsi kuifanya hii roho ichipuke na kufanya kazi. Petro alitamani kila kitu awe kiongozi, kila kitu afanye yeye, kila kitu kiwe sawa, kila kitu kiende inavyohitajika. Na hivyo Yesu akamfanya kuwa kiongozi. Kiongozi ni yule mtu ambaye yuko tayari kujitolea katika mambo yote, na hapa ndipo sehemu kubwa pekee inayomuwezesha mtu kuichipua roho ya uongozi.

11. Petro alikuwa mtu wa mahesabu na mfanya kwa faida. Wakati wote waliponyamaza kuhusu kumfata Yesu, Petro hakukaa kimya akaona aulize. "...tazama tumeacha vyote tukakufata; tutapata nini basi?" Petro hakutaka kufanya kitu kwa kujitoa kisichokuwa na matokeo ya maganikio yanayoitwa faida mbere.

NINI TUNAJIFUNZA...
1. Unaweza toka chini kabisa mpaka kuwa juu kabisa.
2. Usichoke kujaribu uonapo fulsa
3. Kila binaadamu anazaliwa na woga, shinda woga wako.
“Tunashinda woga kwa kufanya tunachokiogopa kufanya”
4. Kubari kufa kwaajili ya wengine, kuiponya nafsi yako ni kuwa tayari kuiuwa nafsi yako kwaajiri ya Kristo na watu wengine
“Unataka uijue siku ya kuanza kufanikiwa KiMungu, ni siku utakayoanza kufikiri kwa habari ya wengine”

5. Alitafuta kwanza ufalme wa Mungu, na mengine akazidishiwa; alifanya sehemu yake na kumuacha Mungu afanye sehemu yake.
6. Kama unachokimini kiko sawa, simama ulipo, usiyumbe wala kuyimbishwa. "The strongest man is a one who stand alone" Karl Max
Akimaanisha “mwanaume shujaa ni yule mwenye uwezo wa kusimama peke yake”

7. Usisumbue mda wako kutazama jana, tazama fulsa za leo, usitazame kushindwa au mafanikio yako ya jana, tazama fulsa za leo na uzitumie kwa nguvu ile ile iliyoko ndani yako, bila kuregea.
8. Hata wakati inahitajika uwaze hasi, au wengine wanawaza hasi, wewe waza chanya. Shinda mawazo hasi.
9. Amini wakati na mahari anapohusika Mungu yote yanawezekana.
10. Chipusha roho ya uongozi kwa kujitolea. Unapowapa watu vitu wanavyohitaji watakupa wewe zaidi ya unavyoviitaji.
11. Kuwa mtu wa mahesabu, hesabu hasara na faida. Unapotoa vyote kuanzisha biashara utapata nini basi, unapotumika usitumike kiuvivu, jitume ukijua faida yako ni kubwa toka kwa Yesu, umempa mtu mda wako kuonana naye, utapata nini basi, umeenda sehemu utapata nini basi. Chochote unachofanya lazima utazame utapata nini basi.

BARAKA TANO ZA PETRO
ngoja tuziorodheshe baraka hizo tano na ukurasa wa mbere tutaona namna alivyofanya kwa sehemu yake kwa uaminifu pasipo kuingilia nafasi ya Mungu, pasipo kumngoja Mungu aje afanye sehemu yake na Mungu akafanya sehemu yake kwa uaminifu na hivyo akafika alipoahidiwa na kutamani kufika.
1. Mvuvi wa watu—Luka 5:10B
2. Mwamba wa kanisa—Math 16:18
3. Mmiliki wa funguo za ufalme wa mbinguni—Math 16:19
4. Muimarishi wa wengine—Luka 22:32
5. Mlisha kondoo—Yoh 21:15

Zote hizi tutaziangalia kiundani na kuzichambua kiurahisi zaidi ili kila mtu afahamu.
Namna alivyozipata na namna zilivyomfikia na namna zilivyotimia kwake.
Ila kwanza tuangalie maana ya jana, leo na kesho kiundani na kimafunuo zaidi.


MAANA YA JANA, KESHO NA LEO

Mwaka wa 2009 nikiwa natoka shule ya sekondari ya Kigurunyembe nikiwa na marafiki zangu kadhaa, rafiki yangu mmoja akanyanyua kinywa na kutamka kwa huzuni iliyochanganyika na hasira na majuto kwa mbali, akasema "kama isingekuwa yule msichana nisingekuwa nimeferi" tukacheka sana,
Akanitazama kwa makini na kuniambia "unajua Ulenje nilikuwa na akiri zaidi hata yako", nikamjibu kwa kebeghi "ndiyo basi tena, neno ningelijua huja mwisho wa safari" alikasirika na kujaribu kunipiga ila hakuweza. Wakati huo mimi tulikuwa tukisubiri kuchaguliwa kwenda elimu ya kidato cha tano, sasa kati ya wanne tulikuwa tukitembea wakati ule ni mimi pekee niliyekuwa na matokeo ya kufauru. Yule rafiki hakuwa anajuta kuferi, ila alikuwa anajuta alichofanya wakati aliokuwa amepewa kusoma akautumia kufurahi na kula anasa na msichana.

MDA NI NINI...
Mda una maana nyingi ila huwezi kupinga hii.
Kifupi Mda ni maisha
Mda ni maisha yenye mwanzo na mwisho.
Mda si wa milele kama maisha ya milele, maisha ya milele hayana mda, huwezi kuyapima, yenyewe ni ya milele, yapo na yanaendelea kuwepo.
Unapotamka mda unazungumzia kipimo chenye mwanzo na mwisho. Unapotamka maisha niliyokaa shule, unatamka mda uliyokaa shule, ukihesabu kuna kipimo. Unapotamka nina miaka sabini unatamka mda uliyokaa duniani ni miaka sabini. Hivyo mda ni maisha, yana kipimo, yana mwisho.
Yesu anasema "imetupasa kufanya kazi zake yeye aliyenipeleka (nani?, Mungu) maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi"

"Yesu alipokuja alipewa mda wa kukaa ulimwenguni, na ilimradhimu kukimbizana nao: kwanini mda una kipimo”.
Ukipewa kazi ya kufanya kwa siku moja, maana yake yake ni masaa 12.
Moja ya huzuni ambayo huwa naisikia kwa wazee na watu wazima wenye miaka juu ya 50 wengi kila ninapopata mda wa kukaa nao, huwa wanasema "tulitamani kufanya mengi sana, tulipokuwa vijana kama ninyi, ila mambo yakawa mengi tukashindwa". Kwanini mda umeisha, kwa wao kufanya hayo, walipewa mda wakajisahau wakadhani wana umilele. Ila lipo tumaini toka kwenye kitabu hiki, kuwa hata kama una miaka 80 bado inawezekana.
Bado kwako unayesoma kitabu hiki, una miaka 20, 30, 35,  40, 45, 50, 55, 60, 65, 70, au yeyote ndani ya hiyo; jua kuna wakati utafika hayo unayoyafikiri hutoweza kuyafanya, na yataishia kwenye fikra zako tu.

MAISHA NI NINI...



Fatana nami tutenderea...
UBARIKIWE KWA KUSOMA.
By EV.ULENJE MWAIPUNGU

No comments:

Post a Comment