Friday, November 20, 2015

SEHEMU YA NNE: BARAKA TANO ZA PETRO (KANUNI ZA KUTUMIA LEO YAKO)

MAISHA NI NINI

Hili ni zaidi ya swali, kila mtu anayeweza kupata mda wa kufikiri maisha yake (experience) atapata kusema kuhusu maisha.
Maisha ni neno gumu kujua.

“Unaweza kuwa na maana nyingi kuhusu maisha, ila mapito yatakwambia ukweli”

Hii ni sehemu ya nne ya somo letu, leo tutaangalia sana kuhusu maana ya leo, leo ni nini, pia tutaangalia fikra tofauti za watu na namna inavyoathiri kutumia leo yao.


Maisha ni mda, ni mda uliopimwa au usiopimwa, maisha hupimwa na mda. Na kama ni mda usiyoweza kuhesabika hayo ni maisha ya milele, na kama ni mda unaohesabika basi hiyo ni miaka ya kuishi.

Huwezi taja miaka ya Mungu, ila unaweza taja miaka yako, huwezi taja miaka ya mtu anayeishi milele.

Mda wa kuhesabu miaka ni ule unaokuwepo hapa duniani pekee, ukishaondoka na kufa basi sasa unaelekea kwenye maisha ya umilele, huwezi huko tena kuhesabu miaka. Maisha ya hapa duniani ya yanahesabika na kila mtu kapewa kwa kipimo maalumu

“Maisha ya hapa duniani ni mtihani wa kuona uwezo wetu wa kuishi milele”

Jinsi unavyotumia mda wako duniani, utavuna baada ya kufa” Hakimu wa Haki Yesu hatoangalia umeishi miaka mingapi, ataangalia umeishi vipi.

"Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe" Ayubu anazungumzia maisha ya mwanadamu kuwa siku zake zimeamriwa yaani zina kikomo na kikomo kimeshapangwa/kimeamriwa na tayari na kipo mikononi mwake.  "mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu, naye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa, hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe" Ayubu 14:1-2,5.

Nimetamani ujue kuwa siku zetu za kuishi hapa duniani zimepimwa, na zimeamriwa, zina mwanzo na zina mwisho.

Mwandishi wa Zaburi anamuomba Mungu "basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie hekima" Zaburi 90:12, alianza kusema "Bwana, unijulishe mwisho wangu, na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani; nijue jinsi nilivyo dhaifu" Zaburi 39:4.

Hii yote yatuonesha maisha ya hapa duniani ni mda na kama mda una kipimo basi maisha yako yana kipimo na ipo siku yatafika mwisho,

Swali unaendaje na wakati huo uliopimwa, na unataka uwe umefanya nini ndani ya masaa hayo.

Nakuthibitishia kuwa wakati wako ukifika mwisho utaondoka tu hapa duniani
Usiwe kama Mfalme Hezekia, wakati wake ulipofika Mungu akamfata na kumwambia “atengeneze mambo ya nyumba yake, lakini Hezekia akatafsiri tofauti, Mungu hakuwa anamlaani bali anamtaarifu kiwa katika ugonjwa huo bado itakufa. Lakini alipoomba sana, Mungu ni msikivu akamsikia. Lakini kwa kuongeza siku hizo chache, Kwanza siku Hezekia akakosea, Biblia inasema baada ya kupona, hakumpa Mungu utukufu, akawaonesha wageni milki yote ya nyumba ya Israel, Sasa hezekia aliyeomba kuongezewa mda, unajua nini kilitokea tena, Hezekia akautumia ule mda kumzaa mtoto Manase, Manase akawa mfalme mbaya kuliko wafalme wote waliopita na waliyokuja katika israel.

Tumia mda wako vizuri...

“Nioneshe sababu nyingi za kushindwa maisha, mimi nitakuonesha moja, ni kughairisha.

Acha kughairi ghairi, kila siku nitafanya nitafanya. Sulemani anauliza E mvivu utaamka lini?
Anza kufanya leo jambo unaliona bado. Kuna wakati utafika hutoweza kufanya.

Usitumie mda wako mwingi kutaka kumpendeza kila mtu. Usitumie mda wako kujaribu kufanya kila kitu, jitambue wewe ni nani, umezaliwa kufanya nini na nini unapata hamasa kubwa unapofanya, pesa zitakufata mbele.
Kumbuka hadithi ya Martha na Mariamu. Martha akaanza kuhangaika hangaika akitaka kumpikia Kristo na kufanya kila jambo, Martha akatulia miguuni pa Yesu akimsikiliza; akaacha mengi na kushughulika na moja tu: Ufalme wa Mungu.

“Nioneshe sababu bilioni za mwanadamu kutotimiza kusudi lake, nitakuonesha moja tu, kujaribu kutaka kufanya kila kitu”

Tumia nusu ya miaka yako hapa duniani kufanyika mtu halisi uliyezaliwa kuwa, na tumia mda wako wa mwisho kufanya ulichozaliwa kuwa.

Andrew Carnegie baada ya kufa, walipoenda kwenye nyumba yake, wakapata karatasi ndogo. Mr Carnegie aliandika akiwa na miaka 20 “Nitatumia mda wangu wa mwanzo kuwa milionea, nitatumia nusu ya pili kugawa zote”.
Mr Carnegie alikusanya Dola za kimarekanj zaidi ya milioni 450 na anapokufa akawa amegawa zote.
Inaleta raha.

Usipoteze mda muhimu katika mambo yasiyo muhimu. Heshimu mda wako, watu wengi wanaotazama TV sana huwa hawaji kuonekana kwenye TV, wakoonekana si kwa mema.

Jim Rohn amewahi kumuuliza mtu, gharama ya TV, yule mtu akajibu $12 akamwambia hapana, gharama ya TV ni $12,000 kwa mwaka. Kwanini, watu wengi wanahesabau gharama ya kununua TV na siyo ya kutazama TV. Rafiki yangu kila kitu unachokipa mda, usisahau unakipa sehemu ya maisha yako. Maana mda ni maisha.

Twende pamoja, heshimu mda wako,  kwa maana ndogo kuheshimu dakika moja ni kuheshimu sehemu ya maisha yako.

Maisha yamegawanyika katika Jana, Leo na Kesho.

Lazima tuiheshimu jana, najua umefundishwa kutotazama jana. Lakini kutazama jana ni vema: tazama jana kwa namba ulizoongeza kwenye akaunti yako, thamani yako iliyoongezeka kwa Mungu na kwa jamii, tazama umefanya nini mpaka sasa, narudia tazama umefanya nini mpaka sasa?.

Kuna kanuni inasema utavuna ulichopanda. Kutazama jana inakusaidia kujua uliponda nini jana na ulipandaje na ulikuzaje; na maana ulivyo leo ni mavuno ya ulichopanda jana.

Tazama jana na ugeuze yote yaliyotokea kwako na yote uliyokosea na kupatia na kuyageuza kuwa falsafa na mbinu mpya ya mafanikio.

Yaliyotokea jana na uliyokosea jana yanaweza kufanywa na kuwa mbinu ya mafanikio ya leo. Unataka uthibitisho: jaribu.

Leo ni siku ya baraka: hakuna zawadi nzuri kama leo.

“Mtu anauliza, Je naweza kubarika, jibu rahisi; Ndiyo unaweza,
Anauliza lini sasa jibu rahisi siku utakayoamua kubadirika

Yaweza kuwa kesho; No! Mwambiye siku yoyote inayoitwa Leo.

Kesho ni ajabu; inaweza kuwa njema, inaleta tumaini, inaleta furaha.
Kwanini ukate tamaa wakati huijui kesho.

Tufatane pamoja ili tujue maana ya siku zote tatu: Jana, Leo na Kesho.

A. JANA
Jana ni sehemu ya mda ambao mtu ameutumia ndani ya kipimo cha maisha yake.
Jana ni marighafi au nguvu isiyoweza kurudi wala kuzalishwa tena. Jana ni sehemu ndogo sana ya mda uliyopewa na Mungu kuishi na kutimiza kusudi lake hapa duniani.
Wanafunzi wa chuo kikuu kimoja  cha hapa Tanzania, walijikuta kwenye wakati wa kununua moja ya vinywaji maarufu na vya gharama duniani kwa gharama ya kutupa, kwa bei ya hasara, kwanini zile bidhaa zilikuwa zinaelekea kuisha mda wake wa kuishi (expire date), baada ya mwezi mmoja zingekuwa zimeshaharibika. Jinsi bidhaa inavyokaa dukani ndivyo inavyozidi kutumia mda wake wa kuharibika na kutumika.

Jinsi binaadamu anavyotumia masaa 12 ya siku na kuingia masaa 12 ya siku nyingine ndivyo anavyozidi kuupunguza ule mda aliyowekewa au kuamriwa tayari na Mungu kama muandishi wa Zaburi alivyothibitisha, na ndivyo kweli.
Hivyo kama ulipewa siku 1000, 000 za kuishi hapa duniani, jana ulipoitumia sasa una 999,999, bila ubishi.

MAMBO YA MSINGI KUHUSU JANA
1. Huwezi kuigusa tena jana
2. Huwezi kufanya chochote ndani ya jana
3. Huwezi kusahihisha ulichofanya jana
5. Una nafasi ya kurekebisha matokeo ya uliyofanya jana pekee na si kufuta ulichofanya.
6. Jana ni historia, si hatima ya maisha yako.
7. Wakati wa msiba wako hawatakumbuka ulichotaka kufanya jana watakumbuka ulichofanya pekee.
8. Ulivyo leo ni matokeo ya uliyofanya jana
9. Kukumbuka na kuhuzunika ya jana ni kupoteza wakati, hekima ni kutazama nini unacho na unaweza fanya leo.
10. Jana inapaswa kutumika kama elimu tu ya leo, ulikosea wapi, ulikoseaje, na namna ya kurekebisha
11. Waliyokufanyia jana; unaweza kuyarekebisha leo
12. Leo ina nguvu zaidi ya jana.
13. Huwezi kuipata tena jana. Imepita

INAWEZEKANA...
Ndugu mpendwa inawezekana jana ulikuwa ni masikini sana, au hata leo, inawezeka jana umetenda dhambi, ninaposema jana nasema kwa wakati uliyopita iwe ni robo saa iliyopita au miaka kumi au hamsini iliyopita au sekunde moja iliyopita, inawezekana umekuwa mtumwa wa pesa, au inawezekana umekuwa ni yatima wazazi wamekufa, au una maisha hayo kwasababu ni mjane hivyo upo hivyo kwasabau ya uliyotebdewa jana, inawezeka upo hivyo kwasababu ya waliyokufanyia jana.
Inawezekana kampuni yako imeshuka kutoka na waliyokufanyia watu jana, washirika wa kampuni yako wamekusaliti, umepata hasara, umefanya uzembe fulani. Au namna yeyote ile.
Na sasa kuna maisha unayoishi, au kuna hari kampuni yako inapitia, lakini hiyo ni jana, tuzungumzie leo, itakusaidia kutoka maisha ya chini kuelekea maisha ya juu zaidi.

Usitazame jana, maadamu umeamka. Jifunze tu kanuni za kutumia leo yako vema.

Jifunze kanuni kuhusu leo.

Jana imepita achana nayo, jifunze tu ulikiseaje kupanda mbegu zako, au ulipanda mbegu gani. Panda mbegu njema sasa na uitunze na kuilinda mpaka iote na linda mazao mpaka uvune.

FIKRA TOFAUTI KUHUSU JANA


Karibu tena Siku sehemu inayofata, tutaona fikra tofauti kuhusu jana na kuenderea na somo letu.

Asante kwa kusoma
Mungu akubariki.
Ev.Ulenje.

No comments:

Post a Comment