Saturday, December 5, 2015

SEHEMU YA TANO: BARAKA TANO ZA PETRO FIKRA TOFAUTI KUHUSU JANA

FIKRA TOFAUTI KUHUSU JANA

Unaweza kubadiri jana yako na ukawa tajiri wa kesho.
Fanya hivi

"Tendo unachopaswa kutenda, usitende usichopaswa kutenda"

FIKRA NNE TOFAUTI KUHUSU JANA

A. Kundi la Watu ambao Huamini wanaweza kufuta makosa ya jana kwa kufanya zaidi leo.
Jim Rohn anakutana na binti akiuza maandazi ya aina tofauti, binti anamuonesha tabasamu zuri na kutangaza maandazi yake, Jim anapenda sana tabasamu la yule binti, na kwasababu alikuwa ni mpenzi sana wa maandazi ya aina ile, na tabasamu la binti akajikuta anavutiwa kununua.

“Huwezi kufanya usichoweza kufanya, kama hukujiandaa kufanya, wenye maandarizi bora ndiyo pekee wanaweza kufanya kwa ubora”

Jim akauliza bei, binti akamjibu kwa dharau akijua ni kiasi kidogo sana cha pesa "yapo maandazi ya rangi tofauti, na yote nayauza Dola $2 pekee”
Jim pia akakubaliana na binti pia kuwa ni kiasi kidogo sana, lakini kilichomkwamisha, akajitazama mfukoni hana kiasi hiko kidogo. Ndiyo ni kiasi kidogo ila ndiyo hana, Jim akafikiri "ni mtu mzima, ana familia, ana mtoto, anaishi Amerika, kwa aibu akalazimika kumdanganya, ili tu afiche aibu, akajibu kwa ujasiri wa kutengeneza "Nina maandazi mengi tu nimenunua, yanatosha kwa familia yangu"

“Tatizo laweza kuendelea kuwa tatizo, kama halitashughulikiwa kama tatizo”

Ficha tatizo ila si kwa wote, maana unahitaji Mungu, Fikra chanya, Maono, Ndoto, Kuona mbali na Watu ili ufanikiwe”

Binti alipotazama ujasiri wa Jim akaamini, akaondoka.
Lakini baada ya binti kuondoka, Jim anaingia ndani na ghafla akiri zinamjia, na kufikiri “Siwezi kuendelea kuishi namna hii”

Tukio moja likabadirisha maisha ya Jim Rohn, Jim Rohn akanyanyuka siku na kuwa milionea, mwalimu mhamasishi (Motivation Speaker), akazunguka karibu dunia yote akifundisha namna ya kufanikiwa na kuongeza ubora wao, Kila mtu alipenda kusikia japo neno lake moja, na katika maisha yake alipenda kusema"

"Usitamani iwe rahisi, tamani uwe bora”

Haikuwa rahisi, ila aliponyanyuka siku hiyo akaongeza ubora wa fahamu zake kuhusu kesho yake, na kusema SIWEZI KUENDELEA KUISHI MAISHA HAYA.
Maisha yake yakabadirika.

“Namna unavyoiona kesho, Ndivyo utakavyokuwa”

SWALI: nini kinakutia hasira leo, ni tukio gani linakupa hasira leo, ni dharau ipo inakupa hasira, nani kakunyima kazi, nani kakufukuza kazi, nani kakuibia, nani amezina mafanikio yako. Jibu lipo...

"Kisasi kizuri ni kuwa na mafanikio makubwa"

TAARIFA MUHIMU
Dunia imejaa matajiri ambao ni masikini wa jana. Na KESHO dunia itajaa matajiri ambao ni masikini wa leo" kama hauamini, Omba uhai, utaona. Lakini nakuombea uje kuwa wewe.

Nikupe siri kabla ya kusonga mbele: Kutafuta mafanikio ni kazi ngumu, ila kuwa masikini ni kazi ngumu zaidi"

Dunia imejawa na watu wenye furaha ya maisha, ndoa, kazi, wamejawa na maisha wanayopenda kuyaishi, lakini jana walikuwa wanaishi katika maisha wasiyoweza hata kuyahadithia. Yamejawa na aibu na matukio ya huzuni.
Pamoja na shuhuda za watu hawa ambao walikuwa masikini jana leo ni matajiri lakini nashangaa  bado bilioni ya watu duniani wanaishi maisha yao ya jana na kuiabudu leo hata kukata tamaa na kesho yao.

Jibu ni dogo... Kwanini unakata tamaa, kwani una hofu kama utafika, kwanini unaanza na kuanguka, unainuka na kuanguka...

JE WAJUA
1. Historia nyingi za watu waliofanikiwa zipo kwenye vitabu, na namna walivyofanikiwa, Cha ajabu matajiri ndiyo wanaosoma vitabu na vipeperushi, masikini hawasomi, na wengine wamebakia vile vile, walivyo jana ndivyo walivyo leo, kwanini?

2. Fikra za masikini kuwa jana yao ni matokeo ya mambo waliyofanyiwa na wengine, matokeo ya jinsi walivyo; "sina akiri, mimi ni kilema, mimi ni kipofu, mimi ni yatima, nilikosea kuowa, nilikosea kuchagua elimu hii, nilikosea kuchagua mtu wa kufanya naye biashara, serikari ilikuwa mbovu". Kundi hili huwa halikosi sababu.
Watalaumu serikari, wazazi walikuwa masikini, sina elimu, walimu walikuwa hawafundishi, wazazi hawakunipa mtaji, ndugu hawakunijari, uchaguzi haukuwa huru na haki, barabara mbovu.

Na hii huwafanya kutofikiri nini wanaweza kufanya leo.

3. Matajiri na watu waliofanikiwa hutumia semina na makongamano kufundisha masikini namna walivyofanikiwa. Cha ajabu hawaendi, ni matajiri tu ndiyo huenda.
"Unaweza kuifanya kesho yako kuwa njema, kama utaamua kuitumia leo yako vema.
Petro alitumia kila fulsa ya kuongea aliyoipata kutengeneza kesho yake njema.
Jibu la swali ni rahisi
Tajiri ana kuwa tajiri na masikini masikini, kwasababu tajiri ameamua kuwa tajiri na kujenga tabia ya kuwa tajiri.
Kutumia mda vizuri, kujifunza mbinu za kufanikiwa, kuona leo kama siku iliyipita na jana kama historia.
Wanatumia mda wao vema, wako smart.

B. Kundi la Watu ambao bado wanaishi Jana Yao.
Kundi la pili ni...
Kuna watu wengine wapo kwenye kundi lapili, wao wapo  dunia ya leo lakini bado wanaishi dunia ya jana. Bila kujari kipato ulicho nacho, hata kama ni tajiri ila kama bado unawaza yaliyotokea jana na kukufanya kuona leo huwezi fanya kitu basi bado unaishi jana, una fikra za masikini.
Kundi la watu wachache na waliofanikiwa, wanaoitwa matajiri,

"Hivi unadhani naweza kuwa mtakatifu? Huyu ni kijana anayejiuliza. Watu wengi bado wanaishi kwenye makosa waliyofanya jana, bado wanaishi kwa  kukumbuka waliyofanyiwa jana. Bado wanakumbuka yaliyotokea jana.
Na fikra hii huzaa maisha ya tabu, wanashindwa kufanya kitu chochote,  wanashindwa kutafuta fulsa, na hata zinapotokea wanashindwa kuzitumia, kwanini, bado wanawaza jana.
Asingeniibia fedha ningekuwa tajiri, haya ni mawazo ya kijana wa miaka 24-30, "mimi ni kijana mwema, nasari, natoa zaka, nasaidia masikini, nafanya kazi kwa bidii, lakini ni masikini. Muulize kwanini? Anajibu: "ndugu zangu hawanisaidii, baba yangu alikuwa masikini.
Haya yote ni mawazo ya jana. Badirika.
Acha kuwaza sababu toka nje, mafanikio yako ni kazi yako.

"Usisubiri wengine, fanya nafasi yako, na muache Mungu afanye nafasi yake"

Siku moja nimewahi kukutana na tajiri mmoja Mr. Mwacha nikapata fulsa ya kumshirikisha habari ya kumaliza chuo,  "mzee natafuta kazi ila kazi nyingi mshahara wake upo chini kweli" alinitazama, akacheka na kunijibu kwa ujasiri, neno lililobadirisha fikra yangu, akasema "hata ndege ili iruke lazima ianzie nyuma". Nikacheka ila nikaweka akirini. Baadae nikagundua, tajiri huwa anawaza jana alikuwa anarudi nyuma ili apae juu zaidi, huwa wao hawakati tamaa hata kama leo hana hata dola centi 25, bado anawaza kufanikiwa.

“Kufanikiwa ni kiwango unachoweza kwenda juu pale unapodondoka chini”

Masikini anawaza jana alirudi nyuma kwasababu yeye ni masikini, watu wanamuonea, jinsi alivyo: utaifa wake, rangi yake, ni kilema, ni Mwafrika mweusi, baba ni masikini.

C. Watu wengine Wao wanatazama tu serikari imefanya nini,
hawa ni watu wa takwimu na makabrasha, na mabingwa wa kusoma taarifa na si kanuni. Macho yao ni serikari ilifanya nini mpaka tupo hapa na haya yanatupata.

"Taarifa haiwezi kukuweka huru, kweli itakuweka huru"

Watu hawa Macho yao hutazama serikari ilitenda nini siyo wao walitenda nini. Petro hakuitwa Zelot kama Simoni, yeye hakutaka kupambana na Warumi, alihangaika kuongeza uwezo wake wa kuvua samaki, kuvua watu, kuhubiri injili, kufanya miujiza na mafanikio yakamfata. Haa walipopambana naye, hakupambana, alilinda tu Jina la Bwana.
Acha mambo ya kuifanya serikari mzazi; kutegemea ikurishe na kukupa maisha bora, kuwa mzazi wako binafsi na mhusika mkuu wa mafanikio yako.

"Hukumbukwa wale wanaotoa msaada kwa dunia, husahaulika wale wanaosaidiwa na dunia"

Martin Luther, Martin Luther King Jr, John Bunyan, Dr Living Stone, Abraham Lincolin, Mother Teresa, Albert Einstein, Musa, Yohana Mabatizaji, Paulo na Mkuu wa wote wa rohoni na wenye mwili Yesu Kristo:

Walipojitoa kuisaidia dunia hawakusahaulika. Acha kumlaumu mtu kushindwa kwako, angalia umekosea wapi, hata kama wamekutenda nini, bado unaweza kutumia hayo kwa mafanikio yako.

D. Kundi la Wafikiri Chanya.
Petro alifikiri chanya kila siku: akasema Bwana tujenge vibanda vitatu, kimoja chako, kingine cha Eliya na kingine cha Musa. Aliamini kuna kitu kitabadirika. Amini ukioata siku moja kukaa na Bwana kama Sulemani mambo yatabadirika.
Watu wa kundi hili ni watu watakaofanikiwa, kundi hili huwa wana amani na ni wakomboa mda saa zote, husahau waliyotenda jana na kutazama fulsa ya leo, na hutenda wakitazama nini wanapaswa kutenda leo.
Ni wachapa kazi wasiyopumzika, maana kwao jana hutosha kwa maovu yake, na faida zake, hata kama alifanya mambo makubwa ya kuushangaza ulimwengu, yeye anasahau na kutazama anayopaswa kuyatenda leo.
Hata kama jana alishindwa, yeye huamini leo ni SIKU MPYA NA FULSA MPYA. Wanatoka nje ya milango ya nyumba au geto zao na kwenda kutafuta fulsa, wanazitumia na kufanikiwa, hata kama watashindwa tena. Huendelea kuzitafuta fulsa zingine. Yaani wao hawakomi kutafuta na kuzitumia wanapozipata.

Mstari wa maisha: jana imeshapita, leo ni siku mpya na fulsa mpya, kesho yaweza kuwa nzuri zaidi ya jana.

FIKRA NZURI KUHUSU JANA
Nini kinatupa utofauti kuhusu jana, Tabia ndiyo inatupa utofauti wa fikra kuhusu jana. Fikra sahihi ni kufikiri:
1. Jifunze kutoka jana yako.
• Wapi ulikosea; usifanye tena
• Nini ulifanya kikakupa hasara: usifanye tena
• nini ulishindwa: ongeza uwezo na ufanye

“Usitamani ingekuwa rahisi, tamani uwe na uwezo" Jim Rohn.

2. Kubali ukweli
Kubali kuwa ulikosea, usipinge kila kitu, na ubadirike.

3. Usiruhusu jana kukuadhibu, itumie kwa faida yako.
Kwanini una huzunika, kwanini unasikitika, achana na hayo. Usiruhusu ikuadhibi, tumia mapito hayo kwa kufanya zaidi, hiyo ndiyo bora zaidi.

"Ana heri anaejari mwisho wake kuliko anayesumbuka na mwanzo wa shida”

4. Usihamishe uhusika wako kwa yeyote
Usiwaze kama ingekuwa hivi ningekuwa, waza kama ungekuwa hivi ingekuwa hivi. Usiseme baba angekuwa tajiri, ningekuwa tajiri, sema ningekuwa nina mipango na kusimamia mipango yangu ningekuwa tajiri. Petro hakusema Yesu bahari ni chafu hatujapata kitu, alisema Tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu, lakini kwa neno lako nitazisha nyavu.

5. Ongeza uwezo
Petro aliposema kwa neno lako nitashusha nyavu, alimaanisha kukubali uwezo wake wa ndani ulikuwa mdogo, na kukubali kuwa uwezo wa Yesu ulikuwa mkubwa, hivyo kwa neno lake anashusha nyavu.
Ni mara ngapi katika jana yako umefanya kazi ya kuchosha pasipo matokeo chanya, kwanini ulishindwa, UWEZO WAKO WA NDANI ULIKUWA MDOGO.
Soma vitabu, sikiliza mafundisho, hudhuria semina, jifunze  kwa waliofanikiwa na kwa walioshindwa, ongeza uwezo wako wa ndani, kaaa karibu na waliofanikiwa, omba msaada kwako, kwa nguvu zao utafanikiwa.
Kumbuka Yesu alimwambia nini Petro "nitakufanya kuwa mvuvi wa watu"
Yesu hakutaka kumwambia Petro tatizo ni serikari ya Rumi, tatizo ni upepo au uwepo wa Mafarisayo na Masadukayo, akamwambia tatizo ni wewe, tatizo ni uwezo wako wa ndani, Yesu akatumia miaka mitatu kumfundisha Petro na kuongeza uwezo wake wa ndani, na akawa mtume kiongozi. Siku nilipoiona nyumba ya Petro kwenye dokomentari kuhusu maisha yake nilishangaa.

"Usitamani jana ingekuwa rahisi, tamani ungekuwa bora" Jim Rohn.

Leo nimemtumia sana Jim Rohn kwasababu natamani ujifunze kwake, mtu aliyeweza kupatwa na hasira na maisha yake ya jana, na kuweka ahadi ya kuibadirisha.

Tutaenderea...

Unafikiri ufanye nini kasahihisha jana yako
"Tenda unachotakiwa kutenda, Usitende usichotakiwa kutenda"

Somo lijalo tutaangalia hasa maana ya kesho na namna watu wanavyoitazama kesho. Na mwisho tutaangalia kuhusu leo, ambayo ndiyo lengo hasa la somo hili.

Tutajifunza Kanuni nyingi za msingi za namna ya kutumia leo.

Asante kwa kusoma, Mungu akubariki kwa mda wako.
Naamini ROHO MTAKATIFU AMEKUSAIDIA KWA SEHEMU.

No comments:

Post a Comment