Tuesday, January 10, 2023

UHUSIANO WA ROHO MTAKATIFU NA NENO LA MUNGU

 UHUSIANO WA ROHO MTAKATIFU NA NENO LA MUNGU


1.    Roho ndiye analishuhudia neno ndani yetu.


Yoh 15:26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia

1 Yoh 5:7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli

Tena kuhusu kuokoka Yoh 3:5 Yesu anasema Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, maana yake siyo neno peke yake, Roho lazima awepo ili neno kumuokoa mtu.


2.    Roho ndiye analisema neno la Mungu midomoni mwetu.


Yesu anasema Marko 13;11 msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu

Kwenye Mathayo 10:20 anasema kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu

Siri ya kufikia hapa ni kujaa Roho Mtakatifu, Biblia inasema kwenye Mdo 4:8 Petro akijaa Roho Mtakatifu, alipoongea wazee wakashangaa mbona hawa watu hawajasoma wametoa wapi ujasiri huu.


3.    Roho ndiye anayekupa uwezo wa kuisikia sauti ya Mungu.


Ufu 1:10 Yohana anasema Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu

Ukisoma Eze 2:2 Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami. 

Kumbe muda wote alikuwa hamsikii Yeye aliyesema naye.

Ukisoma Efeso 3:1-6

1 Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa;

2 ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;

3 ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.

4 Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.

5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;

6 ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo 


4.    Roho ndiye anayetupa kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.


Ukisoma 1 Kor 2:9-12 

9 lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.

12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

Kumbe yapo ambayo Mungu amekuandalia lakini kuyapata ni lazima Roho apate kukufunulia, la sivyo utaendelea kuteseka ikiwa uliyokirimiwa yapo.

Na siri kubwa ili Roho akufunulie ni kuwa mtu wa Rohoni, anasema katika mstari wa mwanadamu wa tabia ya asili yaani tabia ya mwilini hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, kwake ataona ni upuuzi, kwanini kwa sababu yanatambulikana kwa jinsi ya Rohoni.


5.    Roho ndiye anatusaidia kulishika Neno


Eze 36:27 anasema Nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu,nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 

Ni baada ya Mungu kuona mwanadamu ameshindwa kuenenda katika sheria zake wala kushika hukumu zake wala kuzitenda, ndipo akaweka roho yake ndani yako.

Ukisoma Warumi 7:23-25 Paulo anaonyesha wazi akipambana kuushinda mwili, lakini jibu anasema ni Roho mtakatifu ndiye anaweza kumuweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.


6.    Roho ndiye analithibitisha neno linapofika wakati wake.


Kila ahadi ya Mungu inapofika wakati wa kutimia unaona Roho anatokea kwenye tukio. Kuzaliwa kwa Yesu unaona mariamu anashika ujauzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Luka 1:35.

Ukisoma Mdo 13:2 Paulo anaitwa kuwa mtume wa mataifa, lakini anakaa miaka 11 Antiokia bila kufanya wito mpaka Roho anashuka na kusema sasa ndiyo wakati Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi niliyowaitia.

Siri kubwa waliingia kufunga na kumsifu Mungu, waliingia rohoni, kama wasingeingia rohoni wakati ungewapita. Acha kujichelewesha kwa kupenda sana kuwa ubize, tenga muda wa kuwa rohoni huu ndiyo wakati wa kupiga hatua uliyoisubiri.


7.    Roho ndiye anathibitisha Neno kwa Ishara na Nguvu.


Watu walipoona Yesu anafanya ishara nyingi wakasema akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote... Math 8:16, 

Lakini Yeye anakuja anasema kwenye Sura ya 12 hiyo Math 12:28 Lakini nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu. Kumbe wao waliona neno lake pekee, kumbe neno lake lilichanganyika na Roho Mtakatifu.

Mdo 13:9 Inasema Sauli, ambaye ndiye Paulo akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule mchawi akamwambia angalia mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu. Ikawa, kwanini kwa sababu neno lake lilichanganyika na nguvu za Roho.

Ndipo anasema kwenye 1 Thes 1:5 Injili haikuwafikia katika maneno tu, bali katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu.

Kama unataka neno lako liwe na nguvu unapotamka katika maombi, siri ni Roho Mtakatifu, Unataka Neno litokee kwenye maisha yako, Roho ndiye anafanya neno litokee kwako pale unapolitenda.


Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477827 

Follow me 

Tiktok, Facebook, Youtube, Instagram kama Pastor Ulenje... hakika Utabarikiwa



No comments:

Post a Comment