Tuesday, November 22, 2022

UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KWA MKRISTO

 KWANINI TUNAMHITAJI ROHO MTAKATIFU?

Somo la Kwanza


Luka 24:45, Mdo 1:4-5

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasitoke mjini mpaka wapokee Roho mtakatifu, maana yake ni muhimu sana kwa Mkristo. Yesu alileta ufalme wa Mungu, na alitaka watu kuingia ndani ya ufalme huo. Wanafunzi walipotaka kujua lini atawaletea ufalme, Yesu anasema kuhusu Roho Mtakatifu.

Yesu anamaanisha ili mfanikiwa ndani ya huu ufalme muhimu sana ni Roho mtakatifu.

  • Utaona kabla Yesu hajafanya chochote kwanza alipata Roho mtakatifu

  • Pia utaona anaawaacha wanafunzi wake, pia anawaambia wasitoke mpaka wapokee Roho

  • Na wanafunzi wake, utaona katika mahubiri yao, cha kwanza kabisa mtu akiokoka ni Roho mtakatifu, na ishara yao kubwa kama mtu amepokelewa na Mungu basi ni kupokea Roho Mtakatifu. Mfano mzuri ni habari ya Kornelio


KWANINI TUNAMHITAJI ROHO MTAKATIFU/ UMUHIMU WA RMT

  • ROHO NI MUHIMU KATIKA WOKOVU WETU.

Tunaokoka kwa njia ya Roho mtakatifu.

  • Yoh 3:5-6 tunazaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho mtakatifu.

Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

  • Tito 3:5 Roho ndiye anayetufanya upya.

si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

Roho ndiye anashuhudia kuwa sisi tu watoto wa Mungu

  • Rum 8:16 ndiye anashuhudia pamoja na roho zetu

Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

Roho ndiye arabuni ya wokovu wetu

  • 2 Kor 1:22 Naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. Arabuni ni ishara ya kitu kijacho. Muhuri ni dhamana au uthibitisho.

naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.

Tunatunza yale mazuri Mungu aliyotupatia kwa Roho Mtakatifu

  • 2 Tim 1:14 Tunalinda ile amana nzuri kwa RMT. Amana ni akiba nzuri au ya thamani. Pasipo Roho utapoteza kila kitu.

Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

Tunamshinda adui kwa Roho Mtakatifu

  • Mdo 1:8 mtapokea nguvu akishawajilia juu yenu RMT. Mfano wa Skewa Mdo 19:14-16. Hawa watu hawakuwa wameokoka, wakatamka jina la Yesu wakijaribu lakini hawakuwa na nguvu.

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

  • Mdo 8:5-7, 5:3-5. Filipo kwa sababu alijaa Roho mtakatifu akashinda nguvu zote za giza, mpaka mganga akasalimu amri.

Tunashinda tamaa za dunia na za mwili kwa RMT

  • Rum 8:13 

kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

Tunakuwa imara katika wokovu kwa sababu ya Roho Mtakatifu

  • Mdo 4:8, 13 walipotikiswa Roho akawapa hekima ya kujibu kwa ujasiri mpaka mafarisayo wenyewe wakashangaa.

Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,

Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Pastor Ulenje

+255 683 477827

MOROGORO, TZ.

No comments:

Post a Comment