Saturday, November 12, 2022

LAZIMA UWE NA SHAHUKU YA KUKUA NA KUONGEZEKA

Bila shahuku ya kukua hakuna mtu aliyewahi kukua.

Shika sana hili_ Wewe ni zaidi ya jinsi ulivyo na unaweza kuwa zaidi ya ulivyo leo.

📌 Kwa Mungu inatakiwa tukue, na Mungu anategemea tukue. Eph 4:13,14

Mungu ametupa nguvu ndani yatu, ikiwa na kazi ya kutufanya tukue. Kuna vitu Mungu hawezi kukupa, ijapokuwa ni vyako, mpaka ukue. Galatia 4:1-7.

Hata chakula, mafanikio, karama, vipawa, nafasi, fulsa na cheo, ambacho Mungu anakupa, kinatokana na ukuaji wako.


MAENEO MUHIMU UNAHITAJI KUKUA NA KUONGEZEKA.


1. Kua kwenye Kuomba

Math 26:40_ Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja.

Yesu alitaka wanafunzi wake wakue katika muda na stamina yao ya kuvumilia usingizi na kuomba.


2. Kukua kwenye kufunga

Math 9:15

Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.

Yesu alimaanisha, siku atakayopaa basi lazima tuanze kuutisha mwili kuacha chakula kwa ajili ya Bwana kwa muda fulani.


3. Kukua kwenye imani

Math 17:16, 19-21

Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.

Yesu alitegemea kwa muda aliokaa na wanafunzi wake, unatosha kukua imani, wakamvunja moyo alipoona kumbe bado wana mashaka hata kutoa pepo. Yesu anategemea kwa muda huo ulio kaa kwenye wokovu, uwe tayari una imani ya kutoa pepo na zaidi.


4. Kukua kwenye Neno.

Ebr 5:12

Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 

Kolosai 1:10 anasema "mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu"

Muda huu inatakiwa uwe tayari unaweza kufundisha siyo tena hata maziwa hujui, weka bidii kusoma neno ili ukue katika maarifa ya Mungu. 


5. Kukua katika kumtumikia Mungu.

Luka 5:10

Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu. 

Mungu anataka ufike hatua ya kuanza kuvua watu.

Yoh 15:16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Mengine yote ni mema, ila kusudi moja la kuokolewa ni ili ukazae matunda, uokoe wengine. "Mungu ametutuma kila sekta ili kuokoa watu kila sekta" huu ndiyo msemo wangu naupenda.


6. Kukua kwenye kiasi.

1 Thes 5:6-8

Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. 

Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 

Chochote fanya kwa kiasi, fanya kwa ratiba, ili ufanye kingine pia.


Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477827 

MOROGORO. TZ.

1 comment: