Saturday, November 19, 2022

MAANA HALISI YA MAOMBI 01.

Mpaka tumejua maombi ni ‘serious task’ kwetu tulio-amini, Hapo tutaanza kuomba. 


 Yesu anasema tukiomba tusipayuke-payuke.

Kupayuka si maneno mengi, kupayuka ni kurusha maneno pasipo shabaha. haikuwa na maana ya kukataa kuomba kwa sauti, ila usifanye hivyo kwa kuamini kuwa sauti huleta ufanisi wa maombi au ndiyo maombi yanakuwa na matokeo. 

Sauti haileti matokea, sauti ni sauti tu. Bali kuomba bila shabaha, bila imani, bali kutamka maneno mengi tu ukifikiri ndiyo kupata majibu, hiyo ndiyo kupayuka. Bali maombi lazima yawe na shabaha, yawe na matarajio. 

Pasipo matarajio hakuna uhakika, pasipo uhakika hakuna imani, pasipo imani hakuna majibu ya maombi, pasipo majibu ya maombi, maana yake bado hujaomba. 

 Swali kwanini Yesu alisema tusipayuke? 

Yesu alitamani tuombe kwa shabaha. Na hii ndiyo siri ya kuombea jambo la mda mrefu, ng’ang’anizi, lililokufata mda mrefu. Unapoingia kuomba ni muhimu kujua kuwa, hitaji lako Yesu alilijua kabla hata ya hitaji kukufikia (Math 6:8, Zab 139: 16), maana Yeye ndiye aliyeziamuru siku kabla hata hazijaja bado. Ndiyo maana akasema “...Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba”

 Mjumuisho wa maneno yote ya mwanzo ndipo tunapata maana ya maombi. Maombi yana nguvu sana kama yakiombwa kwa shabaha. Yaani kuomba ukiwa na matarajio ya kitu fulani kitokee, na ukaomba mpaka kitokee. 

Majibu ya Mungu ni kama bahari, cha kushangaza wengine wanaenda na vijiko, nenda kwa Mungu na matarajio makubwa, matarajio yasiyo na kizuizi cha kutazama uwezo wako bali uwezo wa Mungu usio na kipimo.

 MAANA YA MAOMBI

Kama Yesu anasema Baba Yetu anajua haja zetu kabla hata hatujaomba, kwanini hayashuki TU!?

 Yesu akasema “Basi ninyi salini hivi; Baba Yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Math 6:9-10). 

 Hivyo tunapoingia kwenye maombi tunaingia kwenye very serious business of God’s Kingdom, kushusha mapenzi ya Mungu ambayo yalishakuwa tayari mbinguni hata kabla siku hizi hazijafika, Mungu alikuwa anakusubiri wewe uyashushe duniani (Muhimu 1Kor 2:9). 

Yesu anawaambia wanafunzi wasalipo, wamwambie MUNGU mapenzi yake yatimizwe, kwanini wakati Mungu si mwanadamu hata a-amuriwe na mtu. 

Hapana “Mungu pasipo mtu hafanyi, na Mtu pasipo Mungu hawezi”. 

Usipotamka nini kitokee duniani Mungu hafanyi bali anasubiri mtu mmoja/wawili/zaidi “aliyeitwa kwa jina lake, ajinyenyekeshe na kuomba, na kumtafuta uso, na kuziacha njia mbaya; basi atasikia toka mbinguni na kuwaamehe dhambi yao, na kuponya nchi yao” (2 Nya 7:14) 

Hivyo; Maombi ni kumruhusu Mungu kuingilia jambo duniani 

Kifupi: Maombi ni kushusha mapenzi ya Mungu duniani.

Usikose Sehemu ya pili ya Somo hili kwenye Blog hii ya ulenje.blogspot.com. 

Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477827

Morogoro, TZ.


No comments:

Post a Comment