Wednesday, January 11, 2023

 DHANA HALISI ZA MAFANIKIO

(PRECEPTS TO SUCCEED)

The Original Concepts for Personal Success


Dhana ni wa wazo kuhusu jambo fulani.

Natamani tuone wazo halisi kuhusu Mafanikio. 

Na wazo halisi kuhusu mafanikio tunalipata kwa Mungu. Wazo halisi ni la muhimu sana sababu ndilo linakupa mafanikio halisi.

Mafanikio unaweza kuyapata kwa namna yoyote, na watu wakahisi umefanikiwa na kumbe ni mafanikio feki, tutakuja kuona ufupi wa furaha ya maisha yako na mwisho wako.

Mwaka huu mpya natamani twende kwenye mafanikio halisi, mafanikio ambayo yanatokana na baraka ya Bwana, ambayo haichanganyikani na majuto ndani yake. Binafsi leo naweka agano la kuzifata.

Kwanza naomba ijurikane sisi wana wa Mungu, ni watoto wa Mungu ni mawakili wa ufalme wa Mungu, hivyo tupo duniani kumuwakilisha Mungu, tupo duniani kuwavuta watu wa duniani waje kwenye ufalme wetu. 

Na njia kuu ya kufanya hivyo, ni kutumia kanuni zetu za mafanikio kw usahihi na bidii ili watu wa ulimwengu huu wakiona, watamani kufata kanuni zetu na kuingia kwenye ufalme wetu. Lakini kama tutafanikiwa kwa njia zao, basi hatutakuwa na sababu yoyote ya kuwavuta wao kwetu.


Tunapomaliza mwaka 2022 kuingia mwaka 2023 dalili zimeonekana wazi kwa Tanzania na dunia kuwa uchumi unazidi kushuka, hata Oxford Economics yenye jopo la wachumi 300 wamefanyia utafiti nchi zaidi ya 200 na kuona uchumi unashuka toka pato la 3% mpaka 1.3%. kwa namna hii tunahitaji kanuni za Mungu ili kuwa salama


Jiandae kutembea na kanuni za Mungu ambazo hazitashindwa.


1.   MFANO WA MUNGU 

   ðŸ‘‰ ILI KUTAWARA

Biblia inasema katika 

Mwa 1:26 na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyaa, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho chini ya nchi 

na Sura ya 27 inaweka wazi kuwa Mungu akaumba mtu kwa mfano wake. 

Mungu alimpa mwanadamu cha kwanza ni mfano wake na sura yake, ndipo akasema wakatawale. 

Kutawala ndiyo siraha ya kwanza mwanadamu kufanikiwa, kama ukitawala katika huduma umefanikiwa, ukitawala katika biashara umefanikiwa, ukitawala kazini umefanikiwa. Kwa sababu ili ufanikiwe lazima watu wakujie, na ukitawala maana yake watu wanakujia kupokea bidhaa yako au huduma yako, hapo umefanikiwa


Lakini ili upate utawala wa kweli, sifa ya kwanza ni lazima ufanane na Mungu. Kufanana na Mungu ni katika nia ya ndani, katika nia ya matendo yake, na namna ya kuishi binafsi na watu wengine. Na hasa aliongelea utu wa ndani.

Paulo anasema katika 

Efeso 2:10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Tuliumbwa katika Kristo, sababu kule kuumbwa kwa kwanza kwa lile kosa la adui kulitufanya kuharibika. Siyo muonekano wa nje, bali ndani. Na anaonyesha kuna matendo Mungu aliyaweka tangu awali, ambayo sababu ya anguko mwanadamu akawa hawezi tena kuyafanya.

Yesu anasema zamani haikuwa hivi, ila sababu ya ugumu wa mioyo yenu.

Ukisoma 

Efeso 4:24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. 

Ukisoma tena Kolosai 3:10 Paulo anasema mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.

Kama tunataka kufanikiwa katika uchumi, dhana ya kwanza kabisa ni kuwa watawara, kutawala katika mauzo ya biashara zetu, kutawala kazini, kutawala katika huduma. 

Mwa 17:1-5 Mungu anamwambia Ibrahimu, Mimi ni Mungu mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. Abramu akanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.  

Mungu alipomwambia awe mkamilifu alimaanisha awe afanane na yeye, awe tofauti na wanadamu. Na Ibrahim alipoanguka kifudifudi ishara kukubali, Mungu akwambia sasa nitafanya agano la kukupa kutawara.

Na Yesu anatuamuru tuwe tofauti na watu wengine katika Math 5:48 ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu


2.   PUMZI YA UHAI.

  👉 HAPO UTAWEZA FANYA CHOCHOTE.


Biblia inasema 

Mwa 2:7 Bwana akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Neno la msingi hapo ni mwanadamu akawa nafsi hai. Maana yake ile pumzi ya uhai ndiyo ikamfanya kuwa nafsi hai. Mtu asiye hai hawezi kufanya chochote. Adamu alipokufa kiroho ndipo mahangaiko ya mwanadamu yalianza. 

Lakini inaonyesha uhai wa mwanadamu unatoka kwa Mungu, mwanadamu hawezi chochote pasipo Mungu, mwanadamu pasipo Mungu kinachofata ni mahangaiko tu. 

Utaona mwanadamu alipopewa pumzi ya uhai akawa nafsi hai ndipo Bwana anampa kazi sasa ya kufanya. Kazi ni jukumu la kukuletea pesa, kukuletea mafanikio lakini huwezi fanya kazi pasipo ile pumzi ya uhai, mwisho wake ni mahangaiko,  

Kinachofanya wengi wasipate mafanikio ni kwa sababu wanahangaika na kazi, wanaacha walichopewa ili kufanikisha kazi. Na wengine wanapata mafanikio feki ambayo mwisho wake ni mauti.

Ibrahimu baada ya kutembea sana kuendea nchi ambayo Bwana atamuaonyesha. Mwanzo 12:7 Bwana anamwambia uzao wako nitawapa nchi hii. Kabla hata ya kuanza kuilima wala kujenga hema, akamjengea Madhabahu BWANA aliyemtokea, mstari wa 8 unasema ...akaliitia jina la BWANA.

Hii ilimaanisha Ibrahimu alijua, sawa Mungu amenipa sehemu ila lazima nimtake Yeye kwanza ambaye ndiye pumzi ya uhai ili nifanikiwe katika hii nchi...

Yesu amekaa miaka 30 bila kuanza kazi aliyoijia mpaka aliposhukiwa na Roho mtakatifu Luka 3:22-23. Neno la Bwana linamjia Zakaria kwa Zerubabeli Zekaria 4:6 kusema Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.

Wakati kanuni za dunia zimeshindwa, na umezijaribu sana, 2023 kaa chini na Roho Mtakatifu kwanza muulize nini nifanye, pili mshirikishe katika kila unalofanya. Ufanye 2023 siyo mwaka wa kujaribu bali wa kufanya. Baada ya Israel kuzunguka miaka 40 mlima Seiri, sauti ya Bwana ikamjia Musa peteni njia hii (Kumb 2:1-3). 

Weka mkazo sana katika kumtaka Bwana 2023 zaidi ya miaka yote, taka sana ufalme wake na haki yake, yale ambayo wengine wanayasumbukia hawayapati au wanatumia njia ya udhalimu kuyapata, wewe Mungu atakupa kibali na kukuweka katika nafasi ya kuyapata.


3.   BARAKA ZA BWANA.

 ðŸ‘‰ ILI UONGEZEKE


Baada tu ya mwanadamu kuwa nafsi hai, Mungu akambariki. 

Mwanzo 1:28 Biblia inasema Mungu akawabarikiwa, Mungu akawaambia Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Nikwambie tu wazi unahitaji baraka za Bwana kuliko unavyoweza ukafikiri. 

Watu wengi wanapenda kuongezeka, wanapenda kuzaa vitu, kuanzisha biashara, kampuni na wanataka waende dunia nzima pasipo baraka za Bwana. 

Baraka ni uwezesho wa Mungu ndani ya mtu wa kufanikiwa. Baraka ni kibali cha Mungu, ni neema.

Mtu aliyebarikiwa, ile baraka inampa kufanikiwa katika kila analogusa. Haina maana hatokutana na changamoto, ila ile baraka inampa ulinzi na kushinda.

Biblia inaweka wazi mtu aliyebarikiwa atakuwa tajiri, Mith 10:22 inasema Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo. 

Katika agano jipya 

Efeso 1:3, 4, Paulo anasema Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo. Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo

Hilo neno kama na neno ili tuwe linaunganisha kuonyesha Kumbe kuwa mtakatifu, kuwa mtu usie na hatia mbele zake inaambatana kabisa na baraka zetu kutenda kazi, ndiyo maana hata Adamu utakatifu ndiyo ulilinda baraka yake.  

Ndiyo maana utaona baada ya Bwana kumaliza kumuumba mtu, na kumpatia baraka zote akampa Discipline. Adabu, akamwambia utaishi ndani ya bustani lakini kwa mipaka, kula miti yote lakini miti fulani usile. 

2023 jiandae kuishi kwa mipaka, ishi maisha ukifanya unayopaswa kufanya, achana na yale ambayo yanakuondoa kwenye reli, kwa maana yaliyofanya mpaka sasa una struggle ni kutoishi kwa mipaka.

Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477 827 

FOLLOW ME KWA; 

Tiktok, Facebook, Youtube, Instagram 

Kama Pastor Ulenje.


 



No comments:

Post a Comment