Sunday, January 15, 2023

SIKIA SAUTI YA MUNGU, KUINULIWA NA BWANA NI FUMBO

 SOMO LA TATU LA KUINULIWA


SIKIA KWA BWANA, KUINULIWA NI FUMBO.


Mith 25:2, 

Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.

1 Sam 8:30

Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.


Nikupe Mifano Miwili, Uone Kuwa Kuinuliwa na Mungu ni fumbo...


1) HAUJUI SEHEMU YA KUINULIWA KWAKO.

Yusufu angeweza kudhania au yawezekana aliwahi kudhania kuwa atainuliwa kupitia Potifa, au yawezekana aliamini pale ameshainuliwa. Kwa sababu Potifa alikuwa akida wa Farao na mkuu wa askari, na kama aliweza kumfunga Yusuph kwenye gereza la mfalme maana yake alikuwa mtu mwenye cheo. 

Lakini Mungu anamuinua Yusufu kutokea gerezani na siyo kwa Potifa.

Usikate tamaa kwa sababu hujui mbinu ambayo Mungu anataka kuitumia ili akuinue, kwa sababu hujui sehemu gani Mungu anataka kukuinua, unaweza fikiri anakupeleka gerezani kumbe ndiyo anakupeleka sehemu ya kukuinua, unaweza fikiri anakupeleka chini kumbe anakupeleka sehemu ya kuinuliwa kwako.


2) KUNA WAKATI VITA NDIYO SEHEMU YA KUINUKA KWAKO.

1 Sam 15, 17, 27 (8-9), 30.

Ukisoma hiyo mistari utaona maadui ambao aliwaacha Sauli ndiyo Daudi anawapiga, Lakini kumbuka hawa ndiyo waliomshusha Suali, leo wanakuja kama Maadui. Daudi anauliza niwafute. Mungu anamwambia nenda. 

Daudi alipokewa na Sauli vizuri, akapendwa na Yonathani kama anavyopenda roho yake, lakini haikuwa sehemu ya kuinuka kwake, bali viliinuka vita, akachomewa nyumba, na wake zake wakatekwa. Kumbe Mungu alileta maadui zake, ambao Sauli aliwaacha ukiwapiga ni sehemu ya kuinuka kwako. 

Kupitia Amaleki Yoshua aliinuka na kujulikana kuwa anafaa, leo Daudi anainuka kupiga maadui ambao Sauli aliwaacha. 

Lakini yatufundisha Sehemu ambapo wengine wanaacha wewe muulize Bwana kwanza, yawezekana hizo changamoto zinazofanya wengi waache ni Adui za Bwana, Bwana anataka ushinde ili akupe kuinuliwa.

Walichoshindwa wao ndiyo sehemu ya kuinuka kwako (I am your replacement) ukishindwa kuomba mimi naomba, ukishindwa wachawi mimi naondoa, ukishindwa kufunga mimi nafunga, wakati unalala mimi naomba…

NINI CHA KUFANYA ILI KUCHUNGUZA SIRI YA KUINULIWA


I. FUNGUA MOYO WAKO KWA ROHO MTAKATIFU

1 KOR 2:9-10

9 lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

Kama kuinuliwa ni fumbo, na Roho ndiye pekee anaweza kukujulisha siri hiyo, kwa sababu yeye anayajua mafumbo ya Mungu.

Katika siku yako, tenga angalau asilimia 10 ya masaa yako 24 ukae na Roho Mtakatifu, Yeye atakujulisha siri ya kuinuliwa kwako.

Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani. MWA 41:16

Yusuph alisaidiwa na Roho Mtakatifu kumtafsiria Farao ndoto, na ndiyo ikawa point yako ya kuinuliwa.

Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? MWA 41:38


II. TAZAMA ISHARA YA KUINULIWA

1 FAL 19:19, MWA 40:1-3

Mungu anapotaka akuinue, kwanza anatuma ishara, alipotaka kumuinua Musa, kwanza alimtumia ishara ya kijiti kikiwaka moto bila kuteketea.

Mungu alipotaka kumuinua Elisha, kwanza alimtumia ishara, Eliya akamfata na kumtupia vazi lake. Na Elisha alipoona akajua kabisa kuwa ni ishara ya kuchukua nafasi ya Eliya ya kuwa nabii wa kimataifa. Kwa sababu watumishi wa Mungu walipewa vazi maalumu na Mungu kama ishara ya nafasi zao.


III. OMBA UNAJISIKIA AU HAUJISKII

YER 33:3

Hatuombi kwa sababu tunajisikia, bali unajisikia aua haujisikii inatakiwa kuomba. Yesu hajasema mtakapojisikia kuomba, bali alisema ombeni.

Biblia inasema

Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Utakapoamua kumuita Mungu na kumuita zaidi, Mungu atakuonyesha makubwa na magumu usiyoyajua. Usiyoyajua ni sehemu ya fumbo la kuinuliwa kwako. Huwezi kuonyeshwa makubwa na Mungu alafu ukaishi maisha ya chini.


Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477 827 

pastorulenje@outlook.com 


Nifatirie zaidi katika mitandao ya kijamii kama...

Pastor Ulenje 


No comments:

Post a Comment