Sunday, January 15, 2023

MAANA YA KUINULIWA NA MUNGU

SOMO LA KWANZA LA KUINULIWA NA MUNGU.

MAANA YA KUINULIWA

 1. MTU ALIKUWA CHINI UNAMSIMAMISHA 

Mtu ambaye yupo chini  ni yule ambaye ni daraja la mwisho mbele ya wengine, katika uchumi, maisha yake, uzima wake au historia yake, au familia aliyotoka, Mungu anampeleka kiwango cha juu, anampa historia, anampa heshima na daraja la juu. 

Mfano mzuri ni Daudi alitoka kuchunga kondoo, akafika kuwa na jeshi la watu minne, akafika kuwa mfalme wa Yuda, akafika kuwa mfalme wa Israel, akakuwa kuwa baba wa mfalme wa wafalme na Mungu akamwambia jina lake litabaki milele katika Uflme wa Israel. 

Lakini Bwana alipomuita, aliinuka na kumpiga Goliathi, na BWANA AKAMUINUA.

Soma ____Zaburi 78:70-71.


2. MTU ALIKUWA CHINI SANA UNAMSIMAMISHA. 

Kuna watu wako chini sana kiwango ambacho hata aliye chini anamuona yuko chini, kiwango ambacho hata wewe mwenyewe unajikatia tamaa, hata Mungu akitaka kukuinua unamcheka kuwa hutoweza kuniinua kwa kiwango hiki cha chini, kisha Mungu anakuja anakuinua. 

Mungu anawasimamisha. Mfano mzuri ni Musa, kwa sababu alikuwa kiwango cha chini sana kiwango cha kwenda kufanya kazi kwa baba mkwe, mwanaume kufanya kazi kwa baba mkwe, ni kiwango ambacho hata masikini atakuona upo chini na atakudhalau, 

Ndiyo maana Mungu alipokuja kumuinua alikataa hata Mungu, ikamlazimu Mungu atumie ishara nyingi kumthibitishia lakini bado hakuamini, ila alipoinuka na kwenda Mungu aliposema, BWANA AKAMUINUA.

Soma ____Kutoka 3:14-15


3. MTU AMEDONDOKA UNAMSIMAMISHA. 

Mtu ambaye alikuwa amesimama, kila kitu kinaenda vema, na kila mtu anampa heshima na amekuwa mtu mkuu, kisha katika njia ya maisha anadondoka, watu wanamkatia tamaa, kisha Bwana anakuja anamuinua na kuwa na uwezo wake wa zamani.

Mfano mzuri ni Samsoni, alikuwa mtu mkuu katika nchi yake, ameuwa simba, kauwa majeshi ya wafilisti na nchi yake ikampa heshima kama mwamuzi wao, lakini akadondoka mpaka kuwa kiwango cha chini mpaka kuwa kipofu, ila alipoinuka na kuomba toba mbele za Mungu, BWANA AKAMUINUA.

Soma ___Waamuzi 16:28-29


3. WEWE MWENYEWE KUINUKA HUWEZI 

Kuna mtu yuko chini kiwango ambacho hawezi kuinuka pale anapopewa nafasi ya kuinuka, kwa sababu imefika ameshajihesabia kuwa yeye ni wa chini na wengine ni wa juu. 

Mfano ni yule mtu aliyekuwa kiwete toka tumboni, hajawahi kusimama kwenye maisha yake, alafu leo Petro anamwambia simama, naamini hakuamini_ mpaka Petro akaamua kumsaidia kuinuka, naamini kwako ambae unaona huwezi inuka, inuka kwa maneno haya na BWANA ATAKUINUA kwa sababu naamini amenituma kwa ujumbe huu uinuke.

Soma ____Mdo 3:1-8


4. MTU ALIYEKATA TAMAA KUINUKA ALAFU ANASIMAMISHWA. 

Kuna mtu amejaribu mara nyingi, mara nyingi na mara nyingi tena na tena kusimama na akashindwa, alafu Bwana anakuja kumuinua.

Mfano ni aliyekuwa hawezi katika birika la kwenye mlango wa kondoo, birika la Bethzatha, amejaribu kuinuka kwa miaka 38 ni miaka mingi sana, malaika anapokuja anajaribu kuinuka ajitupe kwenye birika hawezi, mpaka watu wamemkatia tamaa naye akajikatia tamaa kwa sababu amejaribu mara kwa mara, lakini Yesu anamwambi simama, jitwike godoro lako uende. Aliposimama, BWANA AKAMUINUA.

Soma ____Yoh 5:1-8


5. MAANA YAKE NI KUWA CHINI SIYO MWISHO WA MAISHA. 

Kama Mungu alimuinua Daudi aliyekatiwa tamaa na baba yake, kama Mungu alimuinua Musa aliyejikatia tamaa yeye mwenyewe, Samsoni ambaye taifa lilimkatia tamaa, mtu ambaye hata kuinuka mwenyewe hakuweza, mtu dhaifa kiwango cha kujaribu kuinuka miaka 38 asiweze, Sarah aliyekaa bila mtoto miaka 85 mpaka alipoambiwa utazaa akacheka__ LIPO TUMAINI KWAKO LA KUINUKA.

Lakini pia mwambie mtu yeyote “Usinikatie tamaa tafadhali, BWANA ANAWEZA KUNIINUA. Lakini pia na wewe jiambie “Usijikatie tamaa tafadhali, BWANA ANAWEZA KUNIINUA. Waambie watu wasikuandika MWISHO, Wala wewe Usijiandika MWISHO… Maadamu unaishi BWANA ANAKUINUA. 


KANUNI ZA MSINGI KUINULIWA 2023

1. Mkumbuke BWANA MUNGU wako. 
     Mh 12:1, Kumb 8:18 

2. Kuwa na imani ya KUINUKA. 
    Math 9:6-7 

Mimi ni Pastor Ulenje 
+255 683 477827 
pastorulenje@outlook.com 

Follow me kupitia 
Tiktok, Facebook, Youtube, Instagram kama Pastor Ulenje. 

No comments:

Post a Comment