Wednesday, December 9, 2015

SEHEMU YA SITA: BARAKA TANO ZA PETRO NA KUJENGA KESHO KWA HEKIMA

Asante kwa kusoma sehemu ya tano, kama bado nakuomba katika Jina la Bwana Yesu tenga mda na usome sehemu ya tano, sasa tuendelee... ulenje.blogspot.com

B. KESHO

Baada ya kujifunza kuhusu jana sasa ni vema tukajua zaidi kuhusu kesho na kuona namna Petro alivyoweza kutumia leo yake kutengeneza kesho yake.

Petro siku zote alifanya jambo pasipo kutazama jana, hakutazama makosa, kati ya wanafuzi 12 Petro alikuwa ndiye mwanafunzi aliyekaripiwa na Yesu mara nyingi na kukosolewa mara nyingi lakini ndiye aliyetumiwa na kuwekwa karibu sana na Yesu, si hivyo tu, baada ya Yesu kuondoka Petro ndiye maanafunzi aliyeachwa kuwa kiongozi kati ya watume, ndiye aliyeambiwa waimarishe wenzio, ndiye aliyeambiwa kisha kondoo wangu, unaona pamoja na makosa yake yote lakini Mungu aliyakusanya yote na kuyafanya mema kwa kutimiza kusudi lake duniani.

"Unataka kumjua mtu asiyekosea, mtafute mtu asiyetumia fulsa"

Unataka kumjua mtu anayekosea na kuibuka mshindi, mtafute Petro, anayeona fulsa na kuitumia, wakamuita kiherehere, wakamuita mnafki, wakamuita charismatic, wakamuita msariti, lakini ndiye huwezi taja maendereo ya kanisa la kwanza na kuacha jina lake, hata Paulo anajua hilo, hata wewe unayesoma unajua hilo.

Uanataka kuwa mtu wa mafanikio, jaribu sana, ukikosea umia tena umia sana ili usirudie kosa hilo, jisamehe jisamehe tena jisamehe sana, kisha jaribu tena, ukikosea jaribu tena usiache kujaribu, hata ukifika mbinguni, jaribu kuimba kila wimbo jaribu kila wimbo mpaka uwekwe kiongozi wa kuimba kama cheo hiko kipo, lakini kubwa usiache kujaribu.

Najua ungetamani leo iwe ya pili kuelezwa, lakini hapana, siku zote ni za muhimu lakini kwa mafanikio ya mwanadamu LEO ni kuu na muhimu kuliko zote.

Kesho ni mda wa mbere ambao bado haujafikiwa na kuanza kutumika"
Katika mda uliyopewa na Mungu, kesho ni mda ambao bado hujaufikia.
Yesu akasema "Basi msiyasumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe" Math 6:34. Yesu hapa alikuwa akizungumzia siku ya kesho, ambayo ipo mikononi mwako, ambayo katika mda uliyopewa kuishi, kesho ya kwako.
Mtu aliyekufa hana kesho, mtu aliye bado mzima ndiye pekee mwenye kesho. Hivyo kesho ni yako, ukiwa hujaamka kesho, ujue siku zako ziliisha.
Siku ya mkesha wa mwaka mpya wa mwaka 2014 mchungaji wa kanisa la CLC alitoa hadithi ya ajari ya mtu aliyegongwa na gari aina ya Toyota iliyotokea mda wa mchana wa tarehe 31/12/2013, siku moja kabla ya mwaka mpya wa mwaka huo, kisha akasema "fikiri kama tukirudisha dakika moja nyuma, wewe unadhani yule mtu atakuwa anawaza nini kichwani mwake?" Akajibu mwenyewe akasema "lazima atakuwa anawaza mipango ya kufanya baadae". Sijatoa hii hadithi kukwambia usipange ya kesho, nimetoa hii hadithi kukuonesha kuwa, kesho ni yako kama ukiifikia, usipoifikia si yako,

Hivyo kati ya siku tatu: jana, kesho na leo. Tunayoimiliki ni leo tu pekee, si jana wala si kesho. Na usiumize kichwa kwa habari ya kesho, panga tu kwa habari ya kesho, umiza kichwa kwa habari ya leo. Tukizungumzia leo, utanielewa.

"Weka mipango ya kesho na kuwa na dhamira dhabiti ya kuitimiza ila Usiumize kichwa kwa habari ya kesho, Wala usiwaze kwa habari ya jana, umiza kichwa nini unapaswa kufanya na usichopaswa kufanya Leo, maana leo ndiyo siku pekee tunayoimiliki"

Ndugu mpendwa leo ndiyo yenye nguvu kubwa ya kubadiri maisha yako, si jana, wala si kesho.

UTAENDA JEHANAMU SI KWA ULIYOFANYA JANA SI KWA UNAYOPANGA KUFANYA KESHO, ni kwa unayofanya LEO"

Kesho ni siku ndani ya mda tuliyopewa na Mungu ambayo hatujaifikia bado, tukiifikia inaitwa leo, hakuna mtu anayeimiliki kesho. Kama hatujui kuwa tutakufa lini ndivyo hatujui kuwa tuna kesho. Hivyo kesho ni miliki yetu ila ni milki hewa. Inaweza tokea au isitokee.
Kifupi ni kwamba: Mungu amempa kila mtu kusudi yaani kazi ya kufanya na kumpa mda ambao anajua hiyo kazi itakuwa imeisha, kuna wakati anaweza kuongeza, pia mwandamu anaweza kwa kuounguza mwenyewe, hasa pale mwanadamu anapotumia nguvu yake ya maamuzi kufanya jambo ambalo linaweza changia kuondoa uhai wake, Daudi alilia (paraphrase) "Bwana nipe kuzijua siku za kuishi kwangu ili tujue namna ya kuenenda"

1. Kesho ni siku mbere ya leo
2. Kesho ni siku ambayo bado haijatumika
3. Kila mwanadamu ni mjinga kuhusu kesho
4. Na ujinga huleta woga na hofu kwa kila mwanadamu kuhusu kesho.
5. Woga na hofu huleta watu kuisumbukia sana kesho.
6. Kesho ni makisio tu si kitu halisi.
7. Masikini wanahofu na kuacha ije inavyotaka, matajiri wanapanga wanavyotaka ije
8. Masikini wanaamini kutofika kesho, matajiri wanatumai kufika kesho bila kujari umri wao
9. Masikini wanajadiri kesho, matajiri wanawekeza kupata faida kesho.
10. Mabepari wanawekeza kesho kwa hofu ya watoto wao, wenye hekima wanawekeza kwa kizazi kijacho
11. Maisha unayoishi leo, ndiyo yatakuwa kesho yako; maisha ya kesho, yatakupa unachompa wewe leo.
12. Hakuna unachofanya leo, usivune kesho, na kile unachopanda leo, ndicho utakachovuna kesho
13. Maamuzi yako ya leo, ndiyo matokeo ya kesho.
14. Kesho hujaifika, iache siku itoshe kwa maovu yake
15. Usiseme nitafanya kesho hata mara moja, fanya sasa. Toa mchango sasa, panga mipango sasa, tekeleza sasa, kuwa muaminifu sasa, tenda mema sasa, jenga ndoa nzuri sasa, saidia watu sasa. Kuna watu wanatamani waume na wake zao wafufuke ili waweze kusema "nimekusamehe mume wangu, au nimekusamehe mke" ila haiwezi kutokea. Samehe leo, mpende mume au mke leo, fanya malenzi ya Mungu leo.

FIKRA TOFAUTI KUHUSU KESHO.
Tengeneza picha kwenye kichwa chako, wewe ndiyo Yusuph upo gerezani kwa kosa la kusingiziwa. Unapelekwa kufanya kazi za gerezani, unateswa na mijeredi, unakula chakula cha gerezani, miaka mitano inafika na huoni hata wa kuja kukuona au ndugu yako kujua kuwa mzima. Futa wazo kuwa unajua nini kiliendelea kwa Yusuph, fikiria haupo kwenye hadithi  na si hadithi, fikiria ni tukio la kweri kwako; hivi nini mawazo yatakuja kichwani mwako mfano; "nitatoka kweri?, nitatokaje?, itakuwaje wakiniuwa?, au nimkane Mungu wangu?, au nijifanye Mmisri?" Maswari mengi najua yalikuwa ndani ya Yusuph mpaka kufikia hatua ya kuwaambia wale wafanyakazi wa Farao waliopata fursa ya kutoka "msinisahau..." Kwanini alikuwa akitafuta njia ya kutoka, alikuwa hajui kesho yake. Ukweli wa hadithi ni kwamba anayeifahami hadithi anafahamu nini kinaendereana nini kitatokea, tofauti na yule asiyejua hadithi au yule ambaye anaipitia hadithi hiyo.
Yusuph alikuwa hajui nini kitatokea, wewe unajua nini kilimtokea, sasa kuielewa zaidi hadithi hii inatakiwa uivae hadithi hii ya Yusuph na iwe kama wewe, ndipo utajua kuwa mtu anayepitia hajui kesho.
Masikini kwao kesho ni kitendawili kisichokuwa na majibu. Kwao kesho siyo siku yao, ni siku ya wengine, kwao kesho kufika ni 0/100. Na hivyo hakuna anayewaza kesho. Anapopata pesa ya kula siku hiyo, anafurahi na kuona siku hiyo ni ya bahati sana, anafunga kazi na kupumzika. Anafungua pochi mda wa kula ukifika, akimaliza kula analala, akingoja kesho apate tena wapi ya kula. Maisha yote ni mkono na mdomo. Kwanini hawazi kwa habari ya kesho.
Matajiri hawawazi kwa habari ya kesho sana japo hofu yao kubwa kwa habari ya kesho, ni kushuka kiuchumi na kurudi kuwa kama jana yaani wanaogopa kurudi kuwa masikini. Hivyo kundi hili ni kundi lisilojiamini na lenye hofu kubwa sana, kuhusu kesho, utofauti wao na masikini, wao hawawazi kutofika, bali wao wanawaza itakuwaje wakifika wakiwa wameshuka chini kiuchumi na kurudi kama jana. Na hii huwafanya kuwa watu waoga sana wanapokuwa katika siku ya leo. Uzuri wao ni watu wa kupanga sana kwa habari ya kesho. Mabepari wao kesho ni siku ya muhimu sana na hivyo hutumia pesa, nguvu na tekinolojia  kupanga kwa habari ya kesho, mabepari huwaza faida, huwaza masikini atabaki vipi kuwa masikini, siku zote anafikiri na kubashiri kinachowesa kutokea kesho.

Mabepari huwa ni watu wa kufikiri sana, nini kitatokea kesho: uchumi kushuka au kupanda, pesa kushuka au kupanda, biashara kushuka au kupanda. Siku zote wanawaza hayo ili wajue namna ya kushindana na soko.

Wajamaa, wao na serikari tu; mara zote hutumia mda kusoma magazeti na kutazama television kuona nini serikari imepanga kufanya kesho, huwa makini kujua mipango ya serikari ya mda mfupi na muda mrefu na hufatiria kama inatimia. Watu hawa hupatikana hata nchi za kibepari pia.
"Watu wajamaa huwa wanawaza sana serikari imefanya nini kuliko hata wao wamefanya nini"

Watu wa ufalme wa Mungu wao huwa hawakondi wala kukosa furaja kwasababu ya kesho. Wao hutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, kisha haki yao waliyonayo katika ufalme wa Mungu humfanya mfalme wao ambaye ni Mungu Baba kuwatengenezea fulsa. Soma vizuri kuwatengenezea fulsa, huwaandalia mazingira, huwapa kibari, huwapa hekima na maarifa zitakazowasaidia kufanikiwa. Kama ndege wa angani alivyokuwa hana shamba, hana ghara la kuifadhi chakula, wala hana duka ila Baba wa mbinguni humlisha.
Ukifanya uchunguzi wa ndege utagundua kuwa, yeye hutoka kiotani akiwa na matumaini kuna sehemu nitakuta chakula, nitakula na kupata chakula cha watoto wangu. Tazama maua ya kondoni, hayalimi wala hayavuni ila hata Sulemani na fahari yake hajapata kuvikwa kama maua hayo. Mauwa ili yaoate chakula, huwa yanaamini yakishusha mizizi yake na kuchanua maua yake wakati wa mchana yatapata chakuka na mwanga.

Jambo la msingi kuhusu ndege, anatoka kiotani kwenda kuchukua chakula alipowekewa na Baba wa mbinguni.

Maua huwa yanatoa mzizi na kuchanua ili yapate chakula na mwanga.

Nini cha kujifunza Yesu hakusema watu wa Ufalme wa Mungu wasifanye kazi au wasitoke mlangoni mwao na kutazama fulsa na kuzitumia, Kama Ndege anavyotoka kiotani na kwenda sehemu ambapo anaamini Mungu wake wa Mbinguni amemuandalia chakula, ndivyo nawe pia utoke mlangoni ukatazame fulsa pale ambapo Baba yake wa mbinguni amekuandalia.
Kama vile mauwa yanavyotoa miziz yake na majani yake yakiamini kwamba Baba wa Mbinguni amewaandalia maji na mwanga wa jua kwa chakula. Tafuta mtandao tafuta mawazo tafuta marafiki tafuta watu ukiamini kuwa Baba yako wa mbinguni kuna fulsa amekuandalia.

Jifunze katika mfano wa Yesu, kama Baba wa mbinguni anayalisha maua na ndege wa angani, itakuwaje wewe ambaye alikubali mpaka hata kufa kwaajili yako. Kuna fulsa nyingi amekuandalia toka mlangoni si kwa hofu, toka nje kwa imani, ukiamini kuna fulsa amekuandalia leo kufikia mafanikio yako.
Tuma tema barua ya maombi ya kazi, nenda tena kuomba kazi, fanya juhudi mpya maana Baba wa Mbinguni amekuandalia fulsa za kutosha.

Acha hofu na kesho, tafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine hayo Yesu amekuandalia, wewe tazama fulsa na usonge mbele.

Mfano; Mungu atatoa watu kutoka mashariki na magharibi ya mbali kukuletea fulsa. Mamajusi toka mashariki ya mbali ni uthibitisho tosha kuwa Bwana atafanya hilo.

Watu wa ufalme wa Mungu huwa hawana tatizo, kwasababu wao, wameamini Baba yao wa mbinguni anawajua wao, na anashughukika kuwa mema. Hivyo kwao kesho siyo kitendawili, bali Mungu wao ndiyo tumaini kuu na kati ya watu wanaowaza na kutumaini kesho njema ni watu wa kundi hili.

FIKRA HASI KUHUSU KESHO.
watu wengi wanaoishi maisha ya kushindwa huwa wanaangukia kwenye makundi haya mawili.
1. Wale wanaosema "nani anayajua ya kesho" hivyo wanaishi kama wanakufa usiku na wanaona kufika kesho ni asilimia 0, wanaona kesho ni kama makisio tu, ni kama siku isiyofikika. Cha ajabu wanajikuta wamefika, hawana hata pesa ya kuanzia, au hata sehemu ya kuanzia, wanatafuta pesa ya kula, wanakula wanalala huku wakiwa na asilimia 0 za kuamka, wanajikuta wanaamka. Maisha yao huwa ni ya kujaa taabu, utumwa, manung'uniko, kukosa tumaini, kuhangaika, hawana malengo, hawana akiba, wanakula wanalala na kuamka.

Nimewahi kuwa na rafiki yangu nikiwa O-Level: baba yake alikuwa ni mtu mwenye pesa, na kuwafanya kuishi sehemu za watu wenye pesa maarufu kama Kilakala kwa watu wanaotoka Morogoro. Baada ya baba yake kustaafu, maisha yao yalibadirika na kuwa maisha ya shida sana kipesa, siku moja alikosa fedha ya nauli ya kurudi nyumbani kwao kutokea na shule, akanifata na kuniomba nauli, kwa kicheko nikamjibu "tatizo baba zenu wanakumbuka kujenga kwa pesa za kustaafu, nyumba ikiisha na pesa zimekwisha mnakuwa masikini" siku ile hakunielewa lakini akisha kuwa mkubwa atanielewa.

Watu wengi wanatumia pesa zao za mshahara zote, na kuacha kupanga ya kesho, wakiona watakufa kesho, wanashangaa hawafi.
• Watu hawa hutafuta pesa za leo bila kupanga kuhusu kesho yao.
• Huwa hawafanyi majukumu yao, wakiamini kesho itawafanyia majukumu yao.
• hawana mipango
• hawana maono wala ndoto
 • hawana uwekezaji wowote
• hawasaidii watu wengine

2. Kundi la pili ni wale wanaoitafutia kesho maisha na siyo wao wenyewe".
Watu hawa huangaika na kuhangaika wakaiitafutia kesho chakula, mavazi, heshima na utukufu. Kumbuka nimesema "wakiitafautia kesho" siyo "wakijitafutia".

Kundi hili ni watu wenye hofu, mashaka, kuhangaika, na wengi huwa wanatumia mpaka njia ambazo si harari, njia hatarishi, dhuruma, ufisadi na rushwa, ili kutengeneza kesho yao. Watu hawa huishia kuitafutia kesho yao, na kusahau kujitafutia wenyewe maisha. Kuitafutia kesho haki na kusahau kujitafutia wewe haki, si mafanikio ni utumwa.
Mr Msofe alijitahidi kutafuta pesa kwa hari nyingi, aliuza bangi, madawa ya kulevya, akajiunga na rushwa za kuizurumu serikari na dhuruma nyingi akiihofu kesho yake, pesa nyingi alizopata aliweka akiba akiogopa kuteseka kesho yake; akajenga majumba na makampuni, alipomaliza kufanya yote sasa aanze kula faida, akavamiwa na majambazi wenzie akapigwa risasi akafa" Kesho inafaidika yeye ameenda na maji.

Patric the great kijana maarufu, akaenda kwa mganga ili apate utajiri, baada ya kupata utajiri, akaowa na kupata mtoto, baada ya miaka mitano akaumwa akafa, mke akapokonywa mari na ndugu wakatapanya mari zikaisha.

Mzee James ili kupata utajiri akaradhimika kuhudhuria kanisani siku ya jumaapili pekee na siku zingine alikataa kufunga duka lake ili aende kanisani, alipopata utajiri wa kuanza kufanya biashara nje ya nchi, akapata ajari akafa, ndugu wakatapanya mari na mke wake akaishi maisha ya shida.
Mr Tomson alipopata pesa zake za ajira yake ya kusafisha ofisi za watu, kufagia na kuzoa taka taka. Pesa alizopata aliziifadhi chini ya kitanda chake, akisema kesho nitazitumia katika uzee wangu. Siku moja akapata ajari ya gari kabla ya uzee wake, akafa. Hakuwa na ndugu maeneo yale, wakatangaza kwenye vyombo vya habari ili wapate ndugu zake, hakuna aliyejitokeza. Serikari ikachukua jukumu la kumzika. Walipoifungua nyumba yake, wakakuta Dola zaidi ya milioni kumi na tano. Mr Tomson aliishi maisha ya kimasikini sana, kila mtu aliyesikia habari ya kukutwa kwa pesa zile na maisha ya Tomson kila mtu alihuzunika. Kwanini alitafuta maisha ya kesho akasahau kuyatafutia maisha yake.
• Watu wa kundi hili hutumia pesa nyingi kuweka akiba na si kuzalisha pesa zingine
• watu hawa hutumia mda mwingi kujenga ya kesho kuliko kujenga maisha yao, wakihofu kushuka kiuchumi zaidi kuliko kushuka kwa maisha yao, wakihofu vipi fulani akinipita
• watu kama hao ni waoga sana kwa habari ya kesho. Huwa hawana amani siku zote. Wanahofu sana kuwa wasipotafuta leo kesho watateseka sana.
• watu kama hawa, huishi kama masikini wakihifadhi na kutafuta ya kesho. Husema moyoni mwao heri nilale njaa leo, kesho nitashiba na kusaza.
Robert Kiyosaki amewahi sema "haina maana kuishi masikini na kufa tajiri"

Watu wengi wanaishi kama masikini wakisema wanahifadhi, wanajikuta wanaishi masikini nankufa tajiri wakiwaacha watoto na ndugu zao kama Fisi wakigombea mari zao. Unahitaji kujipanga.

"Jenga ufalme wa mbinguni ambapo mwivi wala kutu haviwezi kuharibu"

Kesho ni mda wa mbere ambao Mungu ameundaa kwaajili yako. Na ana mpango na wewe, anachotaka ni wewe kutafuta ufalme wake na haki yake, kisha mengine utazidishiwa. Kwa maana ndogo fanya nafasi yako na umuache Mungu afanye nafasi yake.

FIKRA SAHIHI KUHUSU KESHO

Usikose sehemu ya sita tukizungumzi fikra sahihi kuhusu kesho.
Asante kwa kusoma naamini Roho mtakatifu hajakuangusha, neno hili ni ya hai na linaponya soma vema hata mara mbili ili uelewa
Uliza swali aunacha comment na share ili unisaidie somo hili kufika na kwa wengine.
MUNGU AKUBARIKI
From Holy Spiri

No comments:

Post a Comment