Sunday, February 21, 2016

Part 3: MAANDARIZI KABLA YA KUSEMA NDIYO...

MISINGI IKIHARIBIKA...

Tuchokoze jambo hili la msingi kisha Part 4 tuanze kujadiri "mambo ya msingi ya kufanya maandarizi" kabla ya kusema Ndiyo!

"Huwezi chora ramani ya nyumba, baada ya kujenga msingi

Zaburi 11:3
Mfalme Daudi yeye anauliza
        "Kama misingi ikiharibika,
          Mwenye haki atafanya nini?

Huwezi jenga ghorofa la ngazi 30 kwa kujenga msingi wenye uwezo wa kubeba ghorofa la ngazi tano. Utachekwa tu.

Daudi anasema "mwenye haki atafanya nini" hajasema mwenye dhambi.

Si peke yako, hata wengi hujiuliza "nafunga sana, namtumikia Mungu kwa moyo wote, natoa zaka na dhabihu, ni mchungaji, ni askofu, ni mshirika mwaminifu sana, nampenda mke wangu, ni mwaminifu wa ndoa yangu, ila mbona ndoa yangu inasumbua?

Daudi anasema mwenye haki atafanya nini? Unafanya yote yanayokufanya uwe mwenye haki, ila ndoa haijakaa vema. Haleluya, nasema haleluya!. Hapa lazima kuna jambo la ziada la ambalo Daudi analifahamu.

Maandarizi kabla ya kusema ndiyo, maandarizi kabla ya kuingia kwenye ndoa, ni wakati wa muhimu sana kuliko hata ndoa yenyewe.

Maana msingi wa nyumba ni muhimu sana kuliko hata nyumba yenyewe.

Kuna wengine husema hayo mengine hujijua huko huko, kwani nani kazaliwa anajua, jibu ni fupi tu, unapotaka kujenga ghorofa la ngazi 30, na umeshajenga msingi wa ghorofa ya ngazi 10,  huwezi kubadirisha ramani wakati wa kujenga  ngazi ya 9, na kusema nataka ghorofa ya ngazi 30 na si ngazi 10. Wote watakushangaa, la sivyo itakulazimu ubomoe ngazi ulizojenga zote, kisha ubomoe msingi wote na ndipo uuweke msingi na upya kwa jinsi unavyotaka kubadiri, ambapo gharama yake ni kubwa sana kuliko hata ungekuwa makini mwakati wa kujenga msingi.

Huwezi kubadiri ramani ya nyumba  katikati ya ujenzi. Hivyo nathubutu kusema ni vema kutazama tunaujenga vipi msingi wa ndoa tunayotaka kuingia, hata kabla ya ndoa yenyewe.

KUMB:
        "Kama misingi ikiharibika,
           Mwenye haki atafanya nini

Usikose sehemu ya Nne, kumbuka ndiyo kiini cha somo. TUTAJADIRI maandarizi ya kufanya moja baada ya lingine.
Asante kwa kusoma.

Utukufu kwa Bwana Mungu na Mwanaye Yesu Kristo

1 comment: