Friday, February 12, 2016

MAANDARIZI KABLA YA KUSEMA "NDIYO..." Part 1

PREPARATION BEFORE YOU SAY I DO

Mwaka 2013, nimewahi kumpenda msichana fulani jina naliweka nyuma ya pazia, ila namwita Angel. Maisha yangu ya kutumia mda mwingi kumtafuta Mungu na kutafakari matendo yake, yalinipa kuwa na maisha ya tofauti na mtazamo tofauti kuhusu wasichana na hata ndoa. Nilikuwa wazi hata kusema siamini katika ndoa, siamini kuwa naweza kupenda au hata kuowa. Nilivutiwa sana na maisha ya Mtume Paulo na hata sasa navutiwa sana na maisha yake, hivyo niliwaza nije kuisha pasipo kuowa kama yeye.

Hivyo niliishi namna hiyo mpaka nafika chuo mwaka wa tatu, bado sikuwa nikiamini kuhusu kuowa au kuhusu kupenda. Tabasamu la Angel likanifanya kubadiri muelekeo wa maisha yangu. Nikajikuta kubadiri hata laini ya simu toka tigo na kutumia Airtel sababu tu ya kupata mawasiliano yake. Kwakuwa sikujua kukabiri maisha yale mapya niliyoyaanza, ilichukua mda kumwambia Angel tuanze uhusiano unaoitwa uchumba.

Ili ilichukua miezi mingi sana kuvumilia ile hari, wapendwa kupenda huku ukiogopa kusema kwa unayempenda ni mateso, na kumchukia mtu unayeogopa kumwambia unamchukui ni kifo cha moyo unaoishi. Kila nilipomuona huyu Angel nilisahau hata kuwa niliwahi weka malengo ya kutoowa.
Siku moja uvumilivu ukanishinda, ilikuwa ni siku ya jumaapili. Uzuri Angel tulikuwa tukisali kwenye Fellowship moja ya Casfeta hapo chuoni. Siku hiyo nikaweka moyoni mwangu, kuwa lazima nimwambiye Angel, nini nawaza juu yake. Nikaamka kitandani na kuchukua simu yangu, na kutafuta jina lake, nini kilitokea...

Ninapobonyeza batani ya simu kubonyeza nitume sms, nikasikia sauti ikiniuliza swali gumu na jepesi sana, ambalo kupitia swali hilo ndipo tunapata somo la leo
Nikaulizwa "Are you capable?" Yaani "Je una uwezo?". Nguvu zikaniisha mwilini, nikakosa hata uwezo wa kusimama kwa miguu yangu, nikaanguka kitandani, ubongo ukasimama kuwaza, na hata leo simuwazi tena huyo msichana, upendo ule wa muemko ukaishia pale, hadithi ya maisha yangu ikaanza tena. Kuna jambo natamani kukufundisha hapo.
Mungu aliniuliza "Je una uwezo?". Lilikuwa ni swali la msingi sana. Nilitumia mda wa miezi mingi sana hata kuelewa kuwa kuna somo Mungu alitamani vijana na hata wanandoa waelewe.

"Kufunga ndoa pasipo maandarizi ya ndani (tabia, fikra, mitazamo na akiri) ndiyo mwanzo wa kuvunjika ndoa hata kabla haijafungwa

No comments:

Post a Comment