Monday, February 15, 2016

Part 2. MAANDARIZI KABLA YA KUSEMA "NDIYO..."

Nianzie hapa...

" huwezi kutumia kitu vizuri kama hujui namna ya kukitumia"

Nazungumzia maandarizi kabla ya kusema "Ndiyo"

Yesu  anasema "maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumaliza?"

Na hii na ndiyo sababu ya ndoa nyingi kusumbua. Wengi tunaowa kwa miemko na kutazama umri, na si uwezo wetu wa ndani, na kutazama "kama una uwezo?" Ndoa si kuishi pamoja, kuna zaidi ya maana nyingi ya neno "kuishi pamoja".
Yesu analeta kesi mezani, anasema "Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema mtu huyu, alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza"

Siku hiyo niliishiwa nguvu, haikuwa na maana ya ugonjwa kuingia moyoni mwangu, "ilikuwa ni ishara ya kuwa sikuwa na nguvu za kujenga mnara unaitwa ndoa". Na haikuwa kesi ya umri, ilikuwa kesi ya uwezo wangu wa ndani wa kuwa na uhusiano wa uchumba. Kabla hujasema ndiyo, usiulize kama unampenda au kama anakupenda, ni swali dhaifu sana, usiulize umri wako ni swali dhaifu sana, kaa chumbank peke yako, jifanyie ukaguzi binafsi, ukiwa na Mungu wako, ikiwezekana muulize Mungu anayekujua zaidi, je una uwezo?. Kama huna kabla ya kusema "Ndiyo" chukua mda kuzingatia moyoni mwako, na ujenge uwezo kwanza. Alafu unajua nini cha ajabu, kuwa na uwezo haichukui mda, siku moja mpaka mbili kwa uwezo wa ndani, siku kadhaa kwa uwezo wa nje.
Twende pamoja...

Yesu ananifurahisha hapa anaposema "Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?

Hii ni siri kubwa katika maisha "mazingira siku zote si rafiki" ndoa siku zote hutaka kuwapeleka ninyi chini, mgombane na mchukiane, dunia na matukio ya kimaisha siku zote si rafiki. Hivyo "kabla ya kusema Ndiyo, swali la msingi, je unaweza kupambana na mazingira ya ndoa na changamoto zake" usiogope, hakuna mtaaramu wa maisha, wote tunatembea kwenye neema ya Mungu, wote tuna matatizo yetu tusiyotaka kuyasema yote, ila swali, kwanini wengine wanapotea kwenye matatizo, ambayo wengine wanasimama? Tofauti ni ule uwezo wa ndani.

Wote wana changamoto fulani za ndoa, hata kama wana miaka 25-50 ya ndoa, wana vitu hawawezi kusema, ila katika hayo waliyopitia wakashinda, kuna wengine walianguka. Unaanza kunielewa, nini shida; Ni uwezo wa ndani ya mtu wa kukabiri changamoto na kuzishinda.

Yesu anamaliza kusema "na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali"

Waooo!!! Kama ukiona huwezi kumtii mwanaume kama vile unavyomtii Kristo na kumfanya awe kichwa kwako kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa, basi omba pooo! Mwanaume akali mbali"

 kama ukiona "huwezi kuvumilia makosa na udhaifu wa mwanamke/msichana, hata pale anapoweza kukuumiza sana kama vile Kristo anavyolivumilia kanisa, na kukubari kufa ili alisafishe, basi omba pooo mwanamke akali mbali" waoooo!!!! Incredible.

Kama huyawezi haya aliyoandika mtume Paulo waefeso 5:22-25
Omba pooooo mapema kabla ya mke au mume hajaja kwenye maisha yako.

Ngoja tumalize kabisa Yesu aliyosema kwenye hii luka 14.
"Basi kadharika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu". Kama haupo tayari kuacha aina ya maisha unayoishi, mitizamo yako na misimamo yako, marafiki zako wa kike na wakiume na mengine ambayo unayeanza naye uhusiano hataki, au yanaweza kusababisha kutoenderea na upendo wake kwako, basi omba pooo! Akali mbali, usiwe mke wake, au mume wake.

Yesu anamalizia "Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?, haifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia. Na asikie. Waoooo! Ndoa ni kitu chema sana, ila kama kikiharibika itiwe nini hata ikolee, semina na semina zinafanyika, masomo na masomo yanaandikwa ila bado ndoa ni tatizo, kwanini? Hakuna maandarizi.

Swali "je unaweza kutumia kitu vizuri kama hujui namna ya kukitumia"

Tuendelee kuchana nyavu, sehu ya tatu ipo njiani

Mungu alibariki neno lake.
Kwa msaada wa Roho Mtakatifu Limeandikwa na Ev. Ulenje
0718721848.
imaf2b@gmail.com

No comments:

Post a Comment