Monday, February 29, 2016

Part 4: MAANDARIZI KABLA YA KUSEMA NDIYO....

~ MAANDARIZI 15 KABLA YA KUSEMA NDIYO..."

Karibu sehemu ya nne ya somo letu...
Soma kila swali kwa umakini, kumbuka kujibu ndani ya moyo wako ukiwa peke yako.

Nianze kwa kusema: pindi unaposema ndiyo, kuna vitu vitabadirika kwenye maisha yako.

A. Ndiyo! yako hukuradhimu kubadiri tabia.
     Ili kuendana na furaha ya huyo umwambiaye ndiyo, kumbuka uwe tayari kuwa yeye anavyotaka. Na hivyo kuna vitu unafanya itakuradhimu vibadirike hata kama ulivipenda.

B. Kupungua kwa uhuru
     Kumbuka hutotakiwa kuendelea kuwa na uhuru kama uliokuwa nao, itakuradhimu umpe mwenzi wako sehemu ya uhuru.

C. Misimamo inabadirika
     Kumbuka unayekutana naye ana misimamo, na ili mfurahi lazima uwe tayari kubadiri baadhi ya misimamo yako.
E. Marafiki wanabadirika
F. Matumizi ya simu yanabadirika
G. Mda wa kulala unabadirika

Neno "Nimekubali..." Ambalo mara nyingi hutamkwa na wanawake, ni dogo sana ila ndiyo chanzo cha mabadiriko ya maisha ya wengi. Na hii ndiyo siri, ni wale tu ambao wako tayari kuendana na mabadiriko yanayotokana na neno nimekubali hufaidi furaha ya Ndiyo yao.

"Wale tu ambao wako tayari kukubaliana na mabadiriko yatokanayo na Ndiyo yao, ndiyo hupata furaha ya mahusiano yao"

Tuanze sasa, leo tutajadiri maswali kadhaa na Part ijayo tutamalizia maswali mengine. Kumbuka ni maswali 15.

Sw 1. Je Unaweza Kuzikabiri Hisia Zako?

Mtu yeyote hata kama mlikuwa marafiki kaka na dada hapo mwanzo, mnapoingia kwenye uhusiano mvutano wa miili yenu unaumbika na hivyo kuwaletea hisia tofauti na hapo mwanzo.
Hivyo kabla ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, ili kujizuia kutenda dhambi ya uasherati, lazima kwanza ujiulize kama una uwezo wa kukabiri macho yako na nguvu ya mwili wako kwa binti. Huna uwezo wa kukemea tamaa iondoke, bali una uwezo wa kuzuia kuyachokoza mapenzi.
Wengi husimama wakiwa single na hupotea pale wanapoanza mahusiano.

"Kabla ya kusema ndiyo, jiulize je una uwezo wa kutunza heshima yako mpaka Ndoa"

Turudi kwenye stori yetu kuhusu Angel: siku moja nikitoka kupata ibada yenye nguvu ya Casfeta- chuo kikuu cha UDSM, nakumbuka dada mmoja aliniambia "Ulenje sikuoni siku hizi kwenye ulimwengu wa roho". Nilishangaa lakini nikakumbuka Mungu amewahi kunionesha namna ninavyojiweka mbali naye. Usisahau wakati huo nilikuwa nahubiri madhabahu za ndani na majukwaani, naombea na watu wanapona.
Nakumbuka siku moja nikihubiri kanisa fulani, Mungu alijitukuza wakati wa maombezi, mpaka watu walianza kuitana mitaani na kuja kuombewa. Lakini nikirudi nyumbani Mungu ananionesha niko mbali naye.
Sikuwahi anzisha uhusiano na Angel, siku nilipogundua "bado sina uwezo,
Basi nilisubiri, mpaka namaliza chuo nikaendelea kusubiri, haikuwa dhambi, sikutaka kuwa mbali na Mungu"

Jifunze jambo hapo, ni kwa namna gani mpenzi wako anakuweka mbali na Mungu, kwa njia ya simu yako, au mnapokutana.
Kabla hujasema ndiyo kwa huyo umpendaye, Je una uwezo wa kuongoza hisia zako, na kuishi pasipo kumkosea Mungu. Najua baadhi watapinga, lakini wanaopenda roho zao, na kuwa tayari kukana nafsi zao kwaajili ya Bwana basi watapokea na kufanyia kazi ujumbe huu.

Sw 2. Je Unajua Unaenda Kufanya Nini?

Nilimuuliza binti fulani swali kama hilo, akajibu nitafua, nitaosha vyombo, na kumpikia chakula kizuri kila siku.

"Watu wawili hawawezi kwenda pamoja, kama wasipopatana"

Sina mengi ya kusema katika hili, soma mwanzo 2:20 Biblia inasema "lakini hakuona wa kufanana naye"

Hivyo Mungu uheshimu wa kufanana naye, japo Mungu alizungumzia wasichana wote, maana hakutoa ulinganifu wa msichana na msichana, bali ni msichana na wanyama, na kuona kiumbe msichana ndiye anafaa; ila alionesha jambo la msingi "kuwa anaheshimu sana mfanano"

Kila msichana ni mzuri, ila ni vema wa kufanana na wewe.

Swali letu ni "Je unajua unaenda kufanya nini?. Ni swali dogo, ila kufanana siyo shida, shida huyo unayefanana naye anajua anaenda kufanya nini mtakapokuwa pamoja"

Unashangaa, unapokaa chini na wachumba au wanandoa, na kuwaeleza tatizo ni "mnafanana ila hamfanyi mnayopaswa kufanya" wanacheka, na wengi husema "kwanini mtumishi: sikujua hayo hapo mwanzo?, mwingine aliniambia "tatizo ni kutokujua mtumishi"

"Kanuni ni ndogo, ukijua na kufanya unachopaswa kufanya uhusiano utaenda, usipojua cha kufanya na Ukafanya usichotakiwa kufanya uhusiano hautaenda"
Ev. Ulenje

Nakusihi katika Jina lake Bwana Yesu, tumia mda kusikiliza mafundisho ya watumishi wanaoaminika, soma neno la Mungu, Biblia imejaa stori za kila aina ya ndoa, soma vitabu vya waandishi wa kiroho wanaoaminika, sikiliza watumishi.
Kubwa kabisa muombe Bwana akufundishe njia zake. Na utambua nini unahitajika kufanya wakati wa ndoa, kisha kuwa na amani ya kusema ndiyo, achana na mambo ya umri na miemuko ya mwili, Mungu anatazama uwezo wa ndani na Ndoa pia inategemea sana uwezo wako wa ndani, si miemuko
Ya mwili wako, au umri wako.

"Mungu huwaepusha baadhi ya wasichana kukutana na waume zao, kwasababu ya kuwaepusha wanaume hao na maumivu" Dr Myles Munroe

Kuolewa si umri, umaarufu, karama, huduma au msisimko wa mwili ni uwezo wa ndani.

Fikiria hili, hata kwa wanaume pia.

SW 3. Je Unajua Kutambua

1 Wakorintho 13:9-12
Soma kwa makini mstari huo, ila naomba niandike sehemu muhimu.
Biblia inasema "Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;....nilipokuwa mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga...wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu, wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana"

Hakuna siri kubwa katika kuwa na ndoa nzuri kama "kuwa na uwezo wa kufahamu yaliyojificha nyuma ya neno "nakupenda" unalolisikia.

Natamani kuishia hapa; ila ngoja niendelee: wengi wanalia kwenye mahusiano si kwamba hawakuambiwa "nakupenda" na wapenzi wao, bali walishindwa kutambua nini kipo nyuma ya neno "nakupenda" walilolisikia.

Watu wawili wanasema "nakupenda" je una uwezo wa kutambua "nakupenda ipi ni ya kweli na imetoka kwa Mungu" na ipi ni ya kibinaadamu.

Mwanaume una uwezo wa kufahamu "ndiyo" unayoipokea na nini kipo nyuma yake: je ni Mungu au shetani, je ni hatima nzuri au mbaya. Na kwa wasichana pia, je unatambua nyuma ya hiyo nakupenda; je ni Mungu, Shetani, Hatima nzuri au mbaya.

Kama huna uwezo huo, basi ni bora ukaacha kujenga nyumba, Yesu anasema usije ukajenga msingi, ukashindwa kumalizia na wenzio wakakucheka. Ni bora ukaomba poooo....mapema kabla ya huyo mwanaume au mwanamke hajaja.

Ninayo mengi ya kusema katika hili, ila Roho mtakatifu akufundishe zaidi. Wengi wanalia. Wamejikuta wameng'ang'ania sehemu ambayo wenye uwezo wa kutambua walimwambia hapana, yeye akalazimisha "ndiyo" sasa analia.

Je una uwezo wa kutambua..."nakupenda unayoisikia" au "Ndiyo" unayoisikia. Maana tunafahamu kwa sehemu, na wakati wa utoto tunafahamu kama watoto, kama bado una babaika kujibu "je ni Mungu au ni hisia zangu" ni heri ukaomba poooooo!!!! Mapema, na "ukajifunza kuongeza uwezo wako wa KiMungu wa ndani" wa Utambuzi wa utu uzima"

Nitaendelea maandalizi ya nne siku tati Zijazo....
Usikose....

Kwa msaada wa Roho Mtakatifu somo limeandikwa na
Ulenje Mwaipungu

1 comment:

  1. Good in deed, may the grace of God expand ur bolding capasity, u lead me some where may God bless u bro

    ReplyDelete