NGUVU YA
IMANI
“hakuna
kinachoshindikana kwa wale ambao bado wanaamini”
Mathayo 19:26
Nguvu ni uwezo wa
kitu kimoja kukifanya kitu kingine kufanya kitu pasipo kujali utayari wake.
Imani ina nguvu ya kuamuru kitu chochote pasipo kujali wa hiko kitu. Imani ina
nguvu ya kufanya chochote ambacho fikra za kibinaadamu hakiwezi kikawa
kinawezekana, hata kama hiko kitu hakipo tayari. Yesu aliweza kufanya yote
yaliyoshindikana na wanadamu, akayaamuru yatokee hata kama hayakutaka, hakuweza
kufanya kitu pasipo imani. Je unataka kufanya makubwa zaidi ya aliyofanya Yesu,
ni imani pekee inaweza kukufikisha huko. Nathubutu kusema kunena kwa lugha
pasipo imani, hakuna litakalo tokea, kuomba kwa sauti au taratibu haisaidii,
maana maneno ya kibinaadamu hayawezi kumfanya Yesu afanye lolote. Mungu ameipa
nguvu imani tu pekee kuruhusu nguvu zake kutenda kazi.
“Ni
Imani pekee ndiyo ina nguvu ya kuamuru kisichowezekana kiwezekane”
Nitoe mifano
michache, Nguvu ya imani ndani ya Akida wa Kirumi (Luka 7:1-10), ijapokuwa
hakuwa Myahudi wala hakuwa mtu wa dini ya aina yoyote ya Kiyahudi. Lakini imani
yake ikaruhusu muuijiza juu yake. Mkumbuke yule mwanamke aliyetokwa na damu
miaka 12, nguvu ya imani ndani yake ikaruhusu muujiza wake (Marko 5:25-34).
Jambo la kushangaza hapo ni kiwango cha nguvu ya imani ndani yao. Mkuu wa
Sinagogi Yairo ndiye alikuwa wa kwanza kumfata Yesu kuwa mwanae anaumwa hawezi
yu karibu na kufa (Marko 5:2124), lakini mwanamke ndiye alikuwa wakwanza
kupokea muujiza kabla hata ya Yairo. Kwanini kiwango cha imani ndani yetu.
Yairo alikuwa na imani mwanae atapona akiguswa na Yesu, mwanamke akaenda mbali
zaidi, akaamini kuwa akigusa tu, hata kama Yesu hajatamka neno, hata kama
hatojua basi atapona, kumbuka aliwaza kugusa pindo na ni kweli aligusa pindo,
yaani aliamini hata Yesu asipojua, ili mradi akigusa pindo la vazi lake tu. Je
una imani namna gani?
“kiwango cha imani ndani yako ndiyo
kinaamua kiwango cha muujiza unataka kupokea”
Imani ni kitu
kisichoonekana lakini kina uhai na kina nguvu, ambayo hata mwanadamu hana.
Imani ina nguvu zaidi hata ya nguvu za Mmarekani, Barack Obama alipomuua Osama
Bin Laden alifikiri amemaliza kazi, lakini huwezi kuishinda imani kwa mtutu au
kumuua kiongozi, sasa tunashuhudia kutokea kwa vikundi vya kigaidi zaidi na
Al-kaida bado ipo. Kusambaratisha vyama pinzani kwa kutumia polisi bado
hakuwezi kuishinda imani ndani ya vijana dhidi ya chama pinzani. Wengine
wanajiripua na mabomu sababu ya kusimamia wanachokiamini. Karibu kila vita
duniani chanzo chake ni imani, kama siyo imani ya dini basi ni imani ya
kisiasa. Imani ina nguvu hatari sana na isiyozuirika. Kama kitu unachopaswa
kuwa nacho ili kufanya yote ambao unaona yapo juu ya uwezo wako basi kuwa na
imani.