Wednesday, October 5, 2016

SIRI YA KUFIKIA MAFANIKIO HARAKA

SIRI YA KUFIKIA MAFANIKIO HARAKA.

Mungu hawezi kukupa kazi, au mafanikio makubwa na kukukabidhi mapenzi yake kwasababu bado unawaza kidunia (Misri).
Kama unataka kufanikiwa haraka  _pambana na fikra yako,

Jitahidi kufanana na Yesu unavyofikiri na kuamua (ondoka Misri). Jinsi unavyobaki kidunia basi Mungu anakuchukua katika safari ndefu. Anajua huwezi kukabiri vita vya Kanaani, bado unajiona panzi

Itazame dunia kama Yesu anavyoitazama "Utakuwa namna unavyotazama"

Watu waliozaliwa ndani ya wokovu. Shika sana imani ya wazazi wako. Vizazi vilipozidi na walipokaa sana Kanaani wakasahau agano ambalo Mungu alifanya na baba zao, wakaanza kuabudu miungu mingine.

Mungu aliwauwa kwasababu hawakutaka kufikiri kama Yeye Mungu anavyofikiri. Kuna namna nyingi za kumshusha utukufu Mungu, ila zote huanzia kwenye fikra. neno la Mungu. Mungu alitamani wawatazame majitu kama Yeye anavyowatazama.

Yesu ametuokoa kutoka ulimwenguni, kazi sasa kuishi  ulimwenguni kama watu wa mbinguni. Kanaani ni mbinguni: hapa katikati wale ambao bado wanawaza kama Misri tutawaacha jangwani.

Wewe hukuwa mtenda dhambi ulizaliwa mwenye dhambi, Yesu alituokoa na utumwa huo.

Umeandikwa na Ulenje
Asante Roho Mtakatifu.