Tuesday, May 2, 2017

SHETENI HANA HARAKA

SHETENI HANA HARAKA

Soma ni muhimu....
Mara nyingi watu husumbuliwa na baadhi ya tabia, au kuwa nazo kwa kujua au kutojua_ hasa ni Kiburi, Uvivu, Tamaa ya mwili, tamaa ya macho, Kupenda pesa, maneno mengi, na matumizi mabaya ya fedha... na kushinda katika kila jambo...na kushinda kupanda kiroho. 

Mara nyingi tunashughurika sana na kumurika Miguuni, tunasahau kuwa adui wa miguuni huanzia mbali, kabla ya kufika miguuni. Ukweli ni kwamba mengi yanayotusumbua leo ni matunda tu ya magugu ambayo ibilisi aliyapanda wakati tulipolala, na wakati anapanda ukweli, hakuwa na haraka_ alijua mbegu itaota, kama mwenye shamba asipoamka mapema.
Ulipokuwa unafanya baadhi ya vitu na ukiona ni kawaida, na wakati mwingine mama, ndugu, au rafiki walinyamaza kimya, au wewe mwenyewe uliona kuwa ni kawaida tu, ila leo mti umeota, matunda yanaonekana_ ndipo unashituka. 

siandiki kumsifu shetani, naandika ili kufichua mbinu kubwa ambayo shetani hutumia dhidi ya watumishi na wakristo wengi...hasa kutufanya tusifike mbali.

"Shetani hana haraka..." Ni neno lilibadiri muerekeo mkubwa wa maisha na matendo yangu. Mama yangu katika huduma (Mama Nyagawa) aliniambia, akinisisitiza kuwa **sasa sina kiburi ila napaswa kuwa makini, maana shetani hana haraka, hupanda kiburi leo, akitegemea kesho atavuna

nafikiri alimaanisha kama nilivyoelewa "kuwa napaswa kulinda adui asipande mbegu" ndipo nikakumbuka Yesu alivyosema "lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake" 

Napenda kutazama na kucheza, (mpira wa kikapu),  moja ya wachezaji wa NBA ninaowapenda sana ni Stephen Curry,  naamini ni mchezaji bora hajawahi tokea tangu wakati wa Michael Jordan. 
Siku moja Stephen Curry alifunga gori katikati ya wachezaji na wazuiaji waliobobea na hata kupewa tuzo kama Briant, lakini mchambuzi alipovuta picha kwa karibu akaona Curry amefunga lile gori akiwa amefumba macho, kila mtu alishangaa, kweli kudumbukiza kile kitundu cha kikapu ukiwa umefumba macho!!
Lakini_ Siku ya jana yake, Curry alifanya mazoezi kudumbukiza mpira kwenye kikapu, upande ule aliyotumia kufunga gori mara 77. Fikiri sasa!!
"Stephen Curry alitumia kumbukumbu ya misuri, hakuhitaji macho"

Unapofanya jambo mara kwa mara, mara kwa mara_ kwa kujua au kutokujua,  baadae inaingia kwenye mifupa_ na ikishaingia kwenye mifupa, TABU ndipo huanza. Mtu hujaribu kuacha na kubadirika, akipata matokeo madogo. wazungu huita "Addiction" na wengine hufanya wasijue_ kuwa wanakosea, hata kujihesabia haki, hata wakisikia injili,  mchana watafanya lile lile.
"Mambo mengi ambayo mtu hufanya katika nusu ya pili ya maisha yake, ni yale aliyopanda katika nusu yake ya kwanza"

BADO LIPO TUMAINI
Kama ilivyo jino kwa jino, jicho kwa jicho, Yesu amesema "Kesheni basi... 
Paulo amesema "msimpe ibilisi nafasi" Efeso 4:7
Hakikisha ni nini kinapandwa kwako...
JIBU NI MOJA: Muwahi shetani_ tuwe wajanja kama nyoka na wapole kama ua...Anza kupanda tabia unazotaka

ANZA KUPANDA TABIA UNAZOTAKA
Andika chini VIPI UNATAKA KUWA, Andika kwa peni, na anza Siku hiyo hiyo kufanya mazoezi ya hizo tabia...itachukua mda lakini nakwambia tena ndani ya siku 360 utanipa matokeo...ukifanya hivyo kwa mwaka itakuwa ni tabia yako.

"utapata shida mwanzo, ukifanya na kufanya na kufanya... ila baadae itaingia mifupani... na ikiingia mifupani tu, wewe ni mshindi...

Amka asubuhi saa 10...kuomba
Anza kuomba zaidi ya saa moja kabla ya kulala
Anza kusoma neno saa zaidi ya moja kila siku
Anza kuwa mfadhiri
anza kuhubiri injili kwa mmoja mmoja
anza kutoa sadaka, zaka na shukrani n.k

Anza kuwa unavyoitaka leo_ kama AMIRA inavyoenea taratibu ndani ya ngano na kuiteka ngano yote, ndivyo tabia njema itateka mwili wako wote.
NINI UNATAKA KUWA
Andika chini tabia nzuri zote unazotaka kuwa nazo, Anza leo kuzifanya, itakuaa shida, utaona kushindwa...ila songa mbele "unaposhindwa, usilie kuacha safari, lia kuendelea"

SIKIA NENO MUHIMU
"Haupo una-po-taka KUWA sababu haupo una-vyo-taka KUWA"
Anza kujenga unavyotaka kuwa leo_ Ili baadae uwe unapovyotaka na unapotaka kuwa.
Shetani anapanda tabia kwa siri, sababu anajua wengi hupotea wanapofika juu na kukosa tabia za kuwatunza wabaki juu...
Usikose somo lijalo
Kwa msaada wa Roho mtakatifu 

Ev.Ulenje 
Director CWGM. 
Contact: 0718721848 , imaf2b@gmail.com .