Sunday, May 7, 2023

UMUHIMU WA KUNENA KWA LUGHA KWA MTU ALIYEOKOKA.

UMUHIMU WA KUNENA KWA LUGHA

Sababu Mungu ameweka kunena kwa lugha kwa kusudi, kila kitu Mungu anafanya kina kusudi, na kusudi zuri sana kwa mwanadamu.

Kunena kwa lugha ni namna ambavyo mwanadamu anaweza akawasiliana na Mungu kwa lugha inayowezeshwa na Roho Mtakatifu [inayojaliwa na Roho Mtakatifu].


- Mdo 2:1-4 - Unaona wanafunzi walinena kwa lugha kwa kujaliwa na Roho Mtakatifu.

- Kunena kwa lugha ni Roho Mtakatifu anaweka maneno kwenye roho ya mtu, na kisha mtu ananena hayo maneno kwenye kinywa chake. Aidha kwa mtu kuamua, au Roho kuweka msukumo wa mtu kuyatamka hayo maneno.

- Kunena kwa lugha ni Roho kutuombea kwa lugha ya mbinguni kupitia sisi wenyewe, hasa kupitia roho zetu - Rum 8:26, 27.

- Kunena kwa lugha ni kuruhusu roho zetu kuomba kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu - 1 Kor 14:14. au kuomba katika roho.

- Mtu anaponena kwa lugha mara nyingi haelewi anachokisema sababu ni maneno ambayo hayaeleweki kwa namna ya nyama [mwili] ni mpaka roho aamue kumjalia kufasiri - 1 Kor 14:2, 14

- Mtu atasema kwanini nisielewe, na naombaje sasa vitu nisivyoelewa - Maombi unaomba kwa Mungu hauombi kwako wewe mwenyewe, hivyo muhimu Mungu kuelewa siyo wewe [sina maana Mungu haelewi kiswahili, ila anapenda unene kwa lugha, sababu ndiyo njia pekee ya kuongea na wewe yaani roho yako kibinafsi bila wengine kuhusika, sababau wanakuwa hawaelewi] 

     - Hivyo lugha ya Mungu ni muhimu kuliko lugha yako. Ila Roho yako inaelewa ndiyo maana kuna wakati mtu ananena anasikia furaha, au kulia, sababu roho yako inakuwa imeelewa [roho yako pekee inaweza elewa mambo ya rohoni, na kukuletea kwenye ufahamu wako Roho Mtakatifu akitaka]


- Kunena kwa lugha ni muhimu sana kwa kila mkristo, haina maana mtu hatoenda mbinguni kwa kutonena kwa lugha, lakini kuna vitu vikubwa atavikosa.

- Wengi walio okoka hawaneni kwa lugha, moja ni kwa sababu hawajafundishwa umuhimu wa kunena kwa lugha wakaelewa, mbili ni kwa sababu hawajafika kujua umuhimu wake hata kunena kwa lugha. Siku wakijua watataka sana. 

       - Sababu nimeona watu wakijua, wanaanza kukesha mpaka kanisani wakitaka sana kujawa na Roho kiwango cha kunena kwa lugha.

- Isaya 28:11, 12 - Isaya alitabiri ya kuwa tutasema kwa lugha nyingine.

- Marko 16:17 - Yesu anasema kunena kwa lugha ni moja ya ishara ya mwamini.

- Mdo 2:4 - Unaona ishara ya kwanza ya mtu kujawa na Roho ni kunena kwa lugha.

- 1 Kor 14:18 - Paulo alimshukuru Mungu sababu alinena kuliko wote wakorintho, ambayo walisifika kwa kunena mpaka kupitiliza, ina maana Paulo aliwe msisitizo sana kunena kwenye maisha yake.


- Na kumbuka Biblia imesema "wakasema kwa lugha" na tena inasema "nikiomba kwa lugha" maana yake kunena kwa lugha kunakuwezesha wakati wowote mahali popote ukawa ukisema na Mungu wako, siyo lazima kwenye maombi, hata wakati unakula, unavaa, unatembea, unapiga stori.

UMUHIMU WA KUNENA KWA LUGHA

Tuone sasa umuhimu wa kunea kwa lugha, kwanini Mungu anataka tunene kwa lugha


1. Kunena kwa Lugha ndiyo ishara ya kwanza mtu akipokea Roho Mtakatifu.

- Mtu akipokea Roho Mtakatifu ishara ya kwanza ni kunena kwa lugha.

- Mdo 2:4 ; tunaona wanafunzi walipojawa na Roho mtakatifu, muujiza wa kwanza haukuwa kuinua kiwete au kuponya kipofu, bali walinena kwa lugha. Siku zote Mungu anacholeta kwanza ujue kinabeba vyote. Mfano katika uumbaji, Mungu alianza na kuumba "Nuru" sababu Nuru inabeba vyote - Mwanzo 1:3. 

- Kwahiyo Mungu alitangulia na Kunena kwa Lugha akiwa na maana Lugha mpya [Marko 16:17] inabeba vyote ambavyo Roho anakuja navyo.

   -  Mdo 10:45, 46 ; Utaona Katika nyumba ya Kornelia, wale watu waliokuja na Petro, Wayahudi walioamini, walijua kuwa mataifa nao wamepokea kipawa cha Roho kama wao walipowasikia wakinena kwa lugha; ina maana ishara ya kuwa mtu amepokea hiki kipawa cha Roho ni Kunena kwa lugha.

  -  Mdo 19:6 ; Utaona Paulo alipowawekea mikono wale wanaume kumi na wawili wa Efeso wapokee Roho Mtakatifu, walipopokea, cha kwanza walinena kwa lugha. 

2. Kunena kwa Lugha ni Njia ya Kuongea na Mungu.

- kunena kwa lugha kunamuwezesha mtu kuongea na Mungu kwa njia ya roho yake 

- 1 Kor 14"2

- kwa maana nyingine Mungu ametupa njia ya kiroho ya kuwasiliana naye kibinafsi, tena moja kwa moja [mazungumzo ya wawili na Mungu].

- Paulo anasema "anasema mambo ya siri" maana yake hakuna anayeelewa zaidi ya roho yako na Mungu, na hata shetani haelewi.

- ndiyo maana shetani anapinga sana kunena kwa lugha sababu anajua haelewi, anajua kuna ushindi mkubwa sana kwa mtu anayeomba kwa lugha.

- Mungu ni roho, na kunena kwa lugha ni kunena katika roho yako - maana yake roho kwa roho ndiyo zaweza kuelewana vizuri zaidi ya mwili kwa roho - Ndiyo maana Paulo anasema "akili hazina matunda [1 Kor 14:14]" 

- Yesu amesema "Mungu ni roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli - Yoh 4"24. Maana yake kumuabudu Bwana kwa kunena, kuomba kwa kunena ni muhimu zaidi [1 Kor 14:15]

- Mungu anataka sana roho yako, sababu inamuelewa zaidi ya mwili wako -  na sababu Roho Mtakatifu anakaa kwenye roho yako, basi Mungu anaelewa zaidi roho yako ikiomba zaidi ya maneno ya akili - Ndiyo maana Paulo alimshukuru Mungu kwa sababu ananena zaidi ya wote.

3. Kunena kwa Lugha Inakusaidia Kuomba kama Mungu atakavyo.

- Kwa sababu unponena ni Roho ambaye anayajua mapenzi ya Mungu - 1 Kor 2:11 anasema "vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu".

- Rum 8:26, 27 - Anasema hatujui kuomba jinsi itupasavyo.

- Maana yake "tunajua kuomba" ila siyo "itupasavyo"

- maana yake naweza omba kwa kiswahili, kwa lugha yangu, ila sitoweza kuomba inipasavyo. 

- Kwanini, Sababu;  ni Roho pekee ndiye anaweza jua mambo ya Mungu, hivyo ni Yeye Roho pekee anaweza kuomba ipasavyo, hata ukapata majibu.

- Kwahiyo kuomba katika roho kunamuwezesha mtu kuomba "impasavyo". siyo tu kuomba kukamilisha ratiba au kuonekana umeomba, maana kufanya isivyopasa wakati mwingine ni sawa na hujafanya.

- Sasa Paulo anasema "udhaifu wetu" ina maana [siku ukikubali huu udhaifu unao, kwamba huwezi kuomba ipasavyo], basi utataka kuomba kwa lugha saa zote, ili usi-miss kuomba ikupasavyo.

- Tena anasema "Yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho" maana yake Mungu anaijua nia ya Roho, maana yake anaanza kutazama nia ya Roho siyo nia yetu tena; ambayo mara nyingi haiwazi sawa sawa na mapenzi ya Mungu, sawa sawa na neno.

- Sasa "Kwanini anatazama nia ya Roho na siyo yako" anasema "Kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu" - maana yake kuna namna Mungu anapenda tuombe.

- Siyo kwamba hatuombi, ila tunaponena kwa Lugha tunaomba kama apendavyo Mungu.

- Nikupe mfano, unaweza ukawa unaomba kuhusu chakula, au kuolewa - kwa maneno utaomba chakula au kuolewa lakini katika roho hujui ya kesho, kunena kunaweza kuondosha nguvu za giza au sababu ambayo inazuia wewe kupata chakula, kunena kutakusaidia kuondoka na yoyote, maana mwenye uhitaji "anaweza kuja mtu ukaona muujiza kumbe siyo" sasa kunena kutamzuia huyo mtu na kuanza kupangua rohoni mpaka kumpata yule sahihi" ndiyo maana tunasema unatamka "siri" maana yake ni rohoni.


linaendelea wiki ijayo....

Kwa msaada wa Roho Mtakatifu

Wako Pastor Ulenje

+255 683 477 827 

Facebook kama Pastor Ulenje Online.


Tuesday, May 2, 2023

ROHO AKIJA ANAMBADIRISHA MTU NA MAISHA YAKE

ROHO MTAKATIFU ANABADIRISHA MTU NA MAISHA.

ROHO NI NANI?

- MUNGU anasema ni Roho yake - Yoel 2"28

- Yesu anakuja kusema Roho Mtakatifu - Yoh 14"26. 

- Ina maana utakatifu upo ndani yake, ndiyo sifa yale kuu [ Roho ni mtakatifu na ana nguvu ya kumfanya mtu kuwa mtakatifu]

○ Rum 15"16, 2 Thes 2:13, 1 Petro 1"2

- Roho anakuja ameonekana anakuja na nguvu - Luka 1"35, Mdo 1"8


ROHO ANABADIRISHA MTU NA MAISHA.

1 SAM 10"6,7

- Roho anakufanya kuwa mtu mwingine, tofauti na yule wa kwanza.

- Unapofanyika mwingine, unapewa uwezo, mamlaka ya kufanya chochote uonavyo vema.

- Kuokoka ni kufanywa upya kabisa, na Roho ndiye anahusika katika kukufanya upya

Tito 3"5 - si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

Yesu alipojiliwa na Roho akawa mwingine.

- Yesu bila Roho alikuwa ni mtu wa kawaida, Sababu Yesu ni alichukua asili yetu, akawa kama mwanadamu.

- Ila ile Roho ndani yake ikamfanya kuwa Mungu yaani Kristo.

- Kilichofanya aseme Yeye na Baba yake ni sawa siyo muonekano wa nje, bali ni ndani.

- Alipojiliwa na Roho akawa mwingine kabisa na kuanza kufanya makubwa.


- 1 Sam 16"13

- Daudi alipojiliwa na Roho akawa mtu mwingine kabisa.

- Ndipo watu wakaanza kumfahamu Daudi, lakini hakuna aliyemjua hapo kwanza.

- Pasipo Roho unaweza tia bidii ila zikawa si kitu sababu unakuwa kama wanadamu wengine. 

- unapofanyika mtu mwingine maisha yako yote yanabadilika, ndiyo maana kila aliyejiwa na Roho maisha yake yanabadilika kuanzia na hapo. Ukisoma mifano ya Yusufu, Musa, Daudi, Sulemani, Nabii Eliya, Yesu Mwenyewe, Wanafunzi wa Yesu, na hata leo tunaona mtu anapofika kiwango cha kujaa Roho maisha yake yanabadilika kabisa na kupata sura mpya.


Ubarikiwe kwa Kusoma

Mimi ni Pastor Ulenje 

Tiktok kama Pastor Ulenje 

Facebook kama Pastor Ulenje Online 

+255 683 477827