Tuesday, May 2, 2017

SHETENI HANA HARAKA

SHETENI HANA HARAKA

Soma ni muhimu....
Mara nyingi watu husumbuliwa na baadhi ya tabia, au kuwa nazo kwa kujua au kutojua_ hasa ni Kiburi, Uvivu, Tamaa ya mwili, tamaa ya macho, Kupenda pesa, maneno mengi, na matumizi mabaya ya fedha... na kushinda katika kila jambo...na kushinda kupanda kiroho. 

Mara nyingi tunashughurika sana na kumurika Miguuni, tunasahau kuwa adui wa miguuni huanzia mbali, kabla ya kufika miguuni. Ukweli ni kwamba mengi yanayotusumbua leo ni matunda tu ya magugu ambayo ibilisi aliyapanda wakati tulipolala, na wakati anapanda ukweli, hakuwa na haraka_ alijua mbegu itaota, kama mwenye shamba asipoamka mapema.
Ulipokuwa unafanya baadhi ya vitu na ukiona ni kawaida, na wakati mwingine mama, ndugu, au rafiki walinyamaza kimya, au wewe mwenyewe uliona kuwa ni kawaida tu, ila leo mti umeota, matunda yanaonekana_ ndipo unashituka. 

siandiki kumsifu shetani, naandika ili kufichua mbinu kubwa ambayo shetani hutumia dhidi ya watumishi na wakristo wengi...hasa kutufanya tusifike mbali.

"Shetani hana haraka..." Ni neno lilibadiri muerekeo mkubwa wa maisha na matendo yangu. Mama yangu katika huduma (Mama Nyagawa) aliniambia, akinisisitiza kuwa **sasa sina kiburi ila napaswa kuwa makini, maana shetani hana haraka, hupanda kiburi leo, akitegemea kesho atavuna

nafikiri alimaanisha kama nilivyoelewa "kuwa napaswa kulinda adui asipande mbegu" ndipo nikakumbuka Yesu alivyosema "lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake" 

Napenda kutazama na kucheza, (mpira wa kikapu),  moja ya wachezaji wa NBA ninaowapenda sana ni Stephen Curry,  naamini ni mchezaji bora hajawahi tokea tangu wakati wa Michael Jordan. 
Siku moja Stephen Curry alifunga gori katikati ya wachezaji na wazuiaji waliobobea na hata kupewa tuzo kama Briant, lakini mchambuzi alipovuta picha kwa karibu akaona Curry amefunga lile gori akiwa amefumba macho, kila mtu alishangaa, kweli kudumbukiza kile kitundu cha kikapu ukiwa umefumba macho!!
Lakini_ Siku ya jana yake, Curry alifanya mazoezi kudumbukiza mpira kwenye kikapu, upande ule aliyotumia kufunga gori mara 77. Fikiri sasa!!
"Stephen Curry alitumia kumbukumbu ya misuri, hakuhitaji macho"

Unapofanya jambo mara kwa mara, mara kwa mara_ kwa kujua au kutokujua,  baadae inaingia kwenye mifupa_ na ikishaingia kwenye mifupa, TABU ndipo huanza. Mtu hujaribu kuacha na kubadirika, akipata matokeo madogo. wazungu huita "Addiction" na wengine hufanya wasijue_ kuwa wanakosea, hata kujihesabia haki, hata wakisikia injili,  mchana watafanya lile lile.
"Mambo mengi ambayo mtu hufanya katika nusu ya pili ya maisha yake, ni yale aliyopanda katika nusu yake ya kwanza"

BADO LIPO TUMAINI
Kama ilivyo jino kwa jino, jicho kwa jicho, Yesu amesema "Kesheni basi... 
Paulo amesema "msimpe ibilisi nafasi" Efeso 4:7
Hakikisha ni nini kinapandwa kwako...
JIBU NI MOJA: Muwahi shetani_ tuwe wajanja kama nyoka na wapole kama ua...Anza kupanda tabia unazotaka

ANZA KUPANDA TABIA UNAZOTAKA
Andika chini VIPI UNATAKA KUWA, Andika kwa peni, na anza Siku hiyo hiyo kufanya mazoezi ya hizo tabia...itachukua mda lakini nakwambia tena ndani ya siku 360 utanipa matokeo...ukifanya hivyo kwa mwaka itakuwa ni tabia yako.

"utapata shida mwanzo, ukifanya na kufanya na kufanya... ila baadae itaingia mifupani... na ikiingia mifupani tu, wewe ni mshindi...

Amka asubuhi saa 10...kuomba
Anza kuomba zaidi ya saa moja kabla ya kulala
Anza kusoma neno saa zaidi ya moja kila siku
Anza kuwa mfadhiri
anza kuhubiri injili kwa mmoja mmoja
anza kutoa sadaka, zaka na shukrani n.k

Anza kuwa unavyoitaka leo_ kama AMIRA inavyoenea taratibu ndani ya ngano na kuiteka ngano yote, ndivyo tabia njema itateka mwili wako wote.
NINI UNATAKA KUWA
Andika chini tabia nzuri zote unazotaka kuwa nazo, Anza leo kuzifanya, itakuaa shida, utaona kushindwa...ila songa mbele "unaposhindwa, usilie kuacha safari, lia kuendelea"

SIKIA NENO MUHIMU
"Haupo una-po-taka KUWA sababu haupo una-vyo-taka KUWA"
Anza kujenga unavyotaka kuwa leo_ Ili baadae uwe unapovyotaka na unapotaka kuwa.
Shetani anapanda tabia kwa siri, sababu anajua wengi hupotea wanapofika juu na kukosa tabia za kuwatunza wabaki juu...
Usikose somo lijalo
Kwa msaada wa Roho mtakatifu 

Ev.Ulenje 
Director CWGM. 
Contact: 0718721848 , imaf2b@gmail.com . 


Monday, April 24, 2017

UBIZE NA MUEREKEO WA KANISA.

BUSY AND WORK...

Bila kupinga tunaishi dunia ya watu bize sana,
asubuhi baba kazini, akifika ni bize, hata mama anayebaki nyumbani pia ni bize_ ameshika kupiga deki, kuosha vyombo, mtoto n.k.

wafanyabiashara na wajasiliamari ni bize...

sasa kuja kwa simu za Smartphone na vipindi vizuri vya TV na siasa kuchukua sehemu kubwa ya maisha; basi ubize umeongezeka_ asubuhi lazima uguse Facebook, na kundi la whatsapp limesema nini, bado hujafika kutazama picha nzuri instagram,  na sentensi fupi twitter...

unaporudi jioni, mama ni kupika,  baba taarifa ya habari, huku anacheza na simu mkononi akicheka na marafiki fb, na whatsapp...

TUMEKUWA BIZE SANA...

MPAKA TUNASAHAU....kuomba, Kusoma neno, kutafakari sheria na hukumu za Mungu, na namna ya kutenda kazi ndani ya ufalme...

Dada mmoja (jina nahifadhi)  nilipomwambia kuna wakati sipokea simu, sijibu sms, wala whatsapp hata kama sms ni nzuri_ Alisema nalinga, LAKINI: Naijua faida ya kutenga masaa ya simu, whatsapp, insta na fb.

***Sasa Siku ya Jumapili si siku ya BWANA TENA, bali ndiyo siku ya KUPUMZIKA...

Hata kanisani tunaomba ibada iishe mapema, ili tukale na kupumzika na familia nyumbani, na kuna rafiki ndiyo siku ya kuja kukusalimu.

huwezi kukataa "NI MAMBO MENGI LEO YANACHUKUA MDA WETU MWINGI, ambao, TUNGETUMIA KUTAFAKARI, KUPANGA NA KUMJUA MUNGU ZAIDI.

- Ni kipi kimechukua mda wako uliokuwa ni mda wamaombi?
- Ni kipi kimechukua mda wako uliokuwa wa kusoma neno
- Ni kipi kimeiba mda wako wa kutafakari
- Ni kipi kimechukua shahuku yako ya kushuhudia

- Ni kipi kimechukua pesa yako ya sadaka na kuchangia injili_ ni vocha au bando...

***Unafikiri ni hekima kusoma neno Dk 30 na kukaa mtandao Saa 1.30 na zaidi....Kuomba lisaa 1, na kukaa mtandaoni usiku Masaa 2. IS NOT FAIR, kweli IS NOT FAIR....

NAAMINI
Ukitazama nyuma kabla huna smartphone kuna vitu ulikuwa hufanyi sasa unafanya
kuna udhaifu ulikuwa huna, sasa unao
kuna dhambi inakutesa na ilikuwa haikutesi
kuna mda unamwibia Mungu...

Tunapokuwa Bize tuangalie TUSIMSAHAU Mungu wetu,
tuangalie TUSITENDE dhambi

YESU aliposema "Upendo wa wengi utapoa, alimaanisha alichosema, na alimaanisha kama alivyosema.

Ujumbe kwa wote_ We must Refocus_
#ChurchBACKtoFocus.

Written by
Ev. Ulenje
Director CWGM

Inspire by the Holy Spirit.
fungua ulenje.blogspot.com kwa masomo zaidi.

Sunday, April 23, 2017

Kanuni Moja MUHIMU, Kumtafuta Mungu Nyakati Hizi.

KUMTAFUTA MUNGU KATIKA NYAKATI HIZI

Kanuni MUHIMU,  Mimi naona ni muhimu sana, kwa kila mtu kuijua na kuiweka moyoni, na kuifanyia kazi.

Nianze na kusema, Mungu alisema kwa wana wa Israel "Mtanitafuta na 'kuniona', mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote" Ye

maana ya "kumtafuta kwa moyo wote" ukiipata, ndiyo mwanzo wa kuanza kumtafuta Mungu kama Mungu anavyotaka, na utakuwa ndiyo mwanzo wa kumpata.

NI KAMA HIVI...
Kijana mmoja akamfata mzee tajiri na kumwambia "nataka kuwa tajiri kama wewe", Yule tajiri akamwambia tuonane kesho saa nne asubuhi ufukweni mwa bahari.
kijana akashangaa " kuna uhusiano gani kati ya kutaka utajiri na kwenda ufukweni"
Tajiri akamsisitiza "unataka utajiri, kesho saa nne asubuhi njoo Ufukweni"
Kesho kijana akafika ufukwe wa bahari akiwa amevaa suti amependeza saa nne asubuhi, Tajiri akamwambia "anza kupiga hatua kuingia ndani ya bahari". Kijana akaanza kupiga hatua, maji yakafika magotini, Maji yakafika mabegani, yakafika mdomoni, tajiri anazidi kumwambia aende. Maji yalipofika puani, anashindwa kuhema, kijana akatoka haraka majini,  akasema "huyu mzee ana kichaa". Mzee akamfata kwa haraka na kumshika kichwa na kumzamisha kichwa ndani ya maji_ Kijana akaanza kuhangaika ajitoe,

maana alikuwa anashindwa kuhema. Tajiri akaendelea kumkandamiza ndani ya maji. kwa mda baada ya kijana kuhangaika sana, akamtoa. Kisha akamuuliza "Je! Unapokuwa ndani ya maji, nini hasa unataka?"
Kijana akajibu "nataka kuhema"
Tajiri akamjibu "Hadi utakapofika wakati wa kutaka utajiri kama unavyotaka kuhema, hapo utakuwa tajiri"

NINI MAANA YAKE...
Tuhamishe hii hadithi kwetu watu wenye fikra tofauti na ulimwengu,  sisi tumeagizwa kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na mengine tutazidishiwa.

neno hili liki-ingia moyoni mwako,  KUMTAKA MUNGU KAMA UNAVYOTAKA PUMZI"

kati ya kitu muhimu sana kwetu ni pumzi, na tunahakikisha hatuipotezi_ na ndiyo HITAJI NAMBA MOJA KWETU.
Unapokuwa ndani ya maji, huwezi kutazama simu, TV, mama, Wala kumsikiliza mjomba, wala mume, au mke ila ni moja tu KUPATA KUHEMA..
Sidhani kama utakumbuka kula, au kuchati, kama unataka unatafuta pumzi, bali unachohitaji ni PUMZI TU.
UKIFIKA kumtaka Mungu namna hiyo_ Kuacha vyote na kushughurika na kumtaka kama unavyohitaji pumzi...
UTAKUWA UMEFIKA KUMTAKA KWA MOYO WOTE.

KANUNI YA PILI: Sema KANUNI namba 1 hata mara saba zaidi, asubuhi na jioni, mpaka uone inajisema yenyewe moyoni, hapo itakuwa imechukua maisha yako yote.
Sema nami
NIKIMTAKA MUNGU SANA KAMA NINAVYOTAKA KUHEMA NITAMPATA ZAIDI.
Ukifika kumtafuta Mungu, na kuona huwezi ishi pasipo Yeye, ukarudia kusema hata ikafika moyoni, itachukua moyo wako wote.
Jina la Bwana Libarikiwe

Contact: 0718721848