Saturday, October 17, 2015

BARAKA TANO ZA PETRO: JANA IMEKWISHA LEO NI SIKU MPYA, KESHO ITAKUWA NJEMA ZAIDI YA LEO.

BARAKA TANO ZA PETRO NA MAANA YA LEO, KESHO NA JANA.

UTANGULIZI
Jana Imekwisha, Leo ni Siku Mpya Kesho Yaweza kuwa Nzuri Zaidi ya Leo.
Huu ni mfulizo wa somo la muhimu sana kwa kila mtu, litakusaidia kutambua uko wapi na unaenda wapi, ni somo lililojaa kanuni za namna ya kuitumia leo yako kwa hekima na kuwa na Kesho nzuri. Somo litakupa kuelewa sehemu ya Mungu katika maisha yako na sehemu yako. Litaondoa maswali mengi kuhusu matumizi ya neema ya Mungu.
Mfululizo huu utamtazama Petro kwa kina: tabia zake, mitazamo yake, ucheshi wake, udhaifu na uimara wake na kutazama namna yote hayo alivyoweza kuyatumia hata kumfanya Yesu kwa neema akampa Baraka Tano na zote zikatimia. Na kutazama namna zinavyohusiana na maisha yetu ya leo na kujenga kesho yetu njema.

Nimetumia miaka mitatu sasa kuandaa somo hili. Na nitakayosema na wewe humu ni rasha rasha tu ya somo lenyewe ambalo lipo jikoni likioikwa zaidi kama kitabu.
Kwa msaada wa Roho mtakatifu mafunuo haya ya muhimu yameandikwa na kupewa uvuvio wa hari ya juu kubadiri maisha yako.
Fatana nami.

Tuanzie hapa, Safari ya kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwa kutumia gari la abiria ni wakati mzuri sana. Ni fanani ya safari maisha, MAISHA YANAENDA KASI SANA, hata kuzidi uwezo wetu wa kuyamudu".
Jinsi gari linavyoenda mbere ndivyo barabara, nyasi za pembezoni mwa barabara na vyote vya nje ya gari utaona vikirudi nyuma, jinsi gari linavyoongeza kasi ndivyo vitu pia vinaongeza kasi ya kurudi nyuma. Pekee huwa napenda kutazama uzuri wa tendo hili, maana jinsi unavyosonga mbere ndivyo unavyokutana na nyasi zingine, miji mingine, barabara nyingine, na wote wanarudi nyuma kwa kasi. Nikiwa mtoto nilifikiri kuwa ni kweri vinarudi nyuma, ila shule na ukubwa ukachangia kujua kuwa kwenda mbele kwa gari ndiko husababisha vionekane kurudi nyuma, ila vyenyewe huwa tunaviacha palepale.

Maisha ni safari, maisha ni safari, maisha ni safari, huu ndiyo msemo niliousikia tangu miaka yangu ya utambuzi wa mema na mabaya. Leo naandika kitabu hiki nikiwa na ufahamu napata nguvu ya kuhoji na kuandika, kama maisha ni safari basi kuna gari la abiria tumepanda, na kama lipo basi lazima litakuwa na lina jina, na kama lipo kweri basi kuna barabara, kuna nyasi tunazoziacha nyuma kila siku, kuna miji na vijiji tunaviacha nyuma, kuna vituo tunaviacha nyuma, kuna watu wanashuka njiani nasi tunaendelea mbere, tunafika pia tunashuka wengine wanaendelea, kuna wakati tunafika hata mwisho wa safari.

Kama ni kweri; maisha ni safari, mda ndiyo kipimo cha safari yetu, kila mtu ana mda amewekewa kuishi, na kikomo cha mda wake ndiyo mwisho wa safari yake inayoitwa maisha, wapi tunaenda, tunaelekea kwenye mafanikio na kushindwa, tunaelekea kwenye furaha au huzuni, tunaelekea kwenye utajiri au umasikini, tunaelekea kwenye kuleta mabadiriko au kukubari mabadiriko, tunaelekea kwenye kuwa mfanyakazi au kuwa muajiri, tunaelekea kuwa muwekezaji au mteja, tunaelekea kuwa mtumwa au mtu huru, tunaelekea kufa unafahamika au hufaamiki, tunaeleka mbinguni au jehanamu.
Basi tulilopanda linaitwa ulimwengu;  ni tofauti na nchi au dunia, hivi ni sayari, lakini ulimwengu ni hari ya uathiri (influence), ni hari ya kitWu, mtu/watu kuwa na nguvu ya kufanya wengine kufanya kitu fulani kwa kupenda au kutopenda,
Hivyo tupo kwenye basi la kila mtu akitafuta nguvu ya kuwa na uwezo wa kuwafanya wengine wafanye anachotaka, ulimwengu umpe anachotaka, apate anachotaka, aishi anavyotaka, aende anapotaka, ale na kuvaa anavyotaka. Ukitazama kwa makini; utaona ni wachache ndani ya gari hili ulimwengu wamefanikiwa kufikia hapo, tunawaita matajiri/mabepari/wawekezaji/wajasiriamari, ila kundi kubwa; mabilioni na mabilioni ya watu bado wapo hawajafanikiwa; bado hawajafanikiwa kupata nguvu hizo, za kufanya unachotaka, kwenda unapotaka, kuwekeza unapotaka, kula unavyotaka, kusoma na kusomesha unapotaka, kufanya starehe unayotaka n.k.

Kumbuka hii ni sehemu ya kwanza wiki ijayo tunaendelea...

"Maisha yanaenda kasi, zaidi hata ya uwezo wetu wa kuyamudu"

Kama gari ni ulimwengu, nyasi, na vingine ambavyo huwa tunaviona vikipita na kurudi nyuma kwa kasi ni nini?. Shetani na dunia haijawahi kuwa na jipya, siku zote ni yale yale, dhambi iliyomwangusha huyu, kesho inamwangusha yule, baada ya miaka kadhaa inamwangusha mwingine, jaribu na changamoto iliyomkumba huyu ndiyo hiyo kesho humkumba yule; nimekuwa mshauri wa watu wa rika tofauti kwa miaka kadhaa sasa, sijawahi sikia tatizo ambalo ni jipya, yote yanafanana, tofauti ni mtu na aina ya watu waliyopatwa basi. Nyasi na miji tunaipita huwa havitembei viko pale pale, gari la mbere na gari la nyuma watazikuta palepale na kuzipita, ukipita jana, leo na kesho utazikuta pale pale, hata zikikatwa, miji na vijiji vitabaki, katika safari hii kila mtu atapitia changamoto, majaribu, vikwazo, na makosa kadhaa. Na yote huwa yanafanana.
Cha ajabu, kwanini watu wanashindwa, yaani aliloshindwa huyu kesho yule naye anashindwa; watu hawataki taarifa na kujifunza.

Mfululizo wa somo hili la BARAKA TANO ZA PETRO ni kukusaidia kujua kanuni za kuwa salama katika safari, kujua kuitumia leo yako vema na namna ya kuandaa na kutumaini kesho yako, na pia kukusaidia kufika salama mahari unapotaka ufike katika safari ya maisha uliyoianza, na  kuwa moja ya kundi dogo lenye nguvu ya kuongoza na kuathiri ulimwengu uende wanapotaka, kufanya zaidi, kushinda adui yako mkubwa ambaye ni mafanikio yako ya sasa, kuishi maisha ya mafanikio na amani ya furaha, kuondokana na utumwa wa pesa.
Daniel aliishi nchi ya utumwa lakini aliifanya Babel iende yeye anakokutaka, akainuliwa na kuwa sehemu ya juu ya maliwali wote wa Babeli na juu ya Uliwali wote wa Babeli. Leo ni zamu yako, tumechoka kuishi kama watumwa katika nchi zetu wenyewe. Tumechoka kuishia katikati ya mafanikio yetu wakati Mungu ametuumba kufanya zaidi ya tuliyofanya.

PETRO MWANAFUNZI WA KIPEKEE
Ni mwanafunzi machachari na mchangamfu, nahisi alikuwa ni mtu muongeaji, mtu wa kucheka na tabasanu mda wote, mwenye siasa kidogo, mcheshi, muoga, mwenye silka kubwa ya uongozi, kiherehere, na mtu ambaye hutochoka kukaa naye, ila utachoka tu kumsikiliza maana anaonekana alikuwa ni bingwa wa kuongea.
Petro katika maisha yake anakuja kupewa baraka tano na Bwana Yesu, ila kuzifikia, kuna kazi ilimbidi afanye, alipitia maisha ya kupatia na kukosea.
Petro hakuwa mwanafunzi aliyekuwa namba moja kwa ukaribu na Kristo lakini alifanikiwa katika kupata baraka nyingi ukisoma vitabu vya injili. Hivyo anatupa fulsa sisi ya kumchambua na kutusaidia kujua tunawezaje kujifunza toka kwake.

MAMBO YA MSINGI KUJUA KUHUSA PETRO
1. Petro alikuwa ni mvuvi, masikini, mwenye dhambi, alikuwa chini ya ukoloni wa Kirumi, na maisha yake aliyatumia kuvu samaki na si kukaa na familia.
2. Petro alikuwa alikuwa ni mtu wa kutochoka kujaribu: mda mwingi alisema linalotoka moyoni kujibu maswali ya Yesu na kuchangia mada za Yesu, kuna wakati akapatia na kuna wakati alikosea, lakini hakuchoka kujaribu tena na tena hata alipozuiwa, hakuacha.
3. Alikuwa muoga, ila aliyejitahidi kuushinda uoga wake, hata wakati aliposhindwa alijaribu tena; aliogopa kusema kuwa yeye ni wa Yesu, kuogopa kupigwa kama Yesu, lakini Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo walipoleta taarifa ya kufufuka kwa Yesu, mitume wengine wakaona ni upuuzi yeye hakusita kuwa wakwanza kwenda kuona bila kujari kuwa alikuwa anaenda kwa mtu aliyemkana, siku waliposhukiwa na Roho Mtakatifu akawa wakwanza kusema kati ya wanafunzi 120 waliyobaki, siku zote alipambana na hofu yake, aibu, na woga wake.
4. Alikuwa tayari kufa kwaajili ya wengine, alikuwa tayari kufa ili tu injili iwafikie na wengine. Alikuwa tayari kupambana ili kumwomo Kristo japo haikuwa sahihi kufanya hivyo. Alikuwa tayari kufika mpaka lango la behewa ya kuhani mkuu kuona Yesu anafanywa nini na makuhani.
5. Petro alikuwa ni mwenye njaa na kiu ya haki: alipoona Eliya na. Musa wanasungumza na Yesu akaona hapa ndipo pa kukaa, akamwambia Yesu "...Bwana Mkubwa, ni vizuri sisi kuwapi hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa na kimoja cha Eliya" hali hajui asemalo. Japo alikuw hajui asemalo lakini alionesha kiu na ufalme wa. Mungu, kiu na kukaa penye dirisha la mbinguni. Na kwa hapo Yesu akambariki.
Petro aliacha vyote na kumfata Yesu, hata alipofanywa kuwa kiongozi wa makanisa yote hapo Uyahudi bado alizidi kuifanya kazi ya Mungu na kuutafuta ufalme wake.
6. Alisimamia anachokiamini kwa gharama yeyote; hata walipomshawishi kuwa aache kulihubiri Jina la Yesu, bado alisimama pamoja na Yohana na kuwaambia "...ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe, maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Mdo 4:19-20
7. Alikuwa mtu wa kutazama leo; Petro hata wakati alipokosea, alichukua kuwa hilo ni kosa la jana, akawa analisahihisha na kusonga mbele, kiukweli Petro alikuwa ni mtu wa kukosea sana, ila alikuwa ni mtu mwenye kutumia sana fulsa. Petro alipoambiwa na Yesu "rudi nyuma ewe shetani" Yoh 18:10, ndiye huyo huyo anakuja kumwambia nipo "tayari kwenda na wewe gerezani" Luka 22:33, Yesu anamwambia utanikana mara tatu, Petro hakusita kwenda naye kwenye maombi, aliposinzia na kuamshwa mara kadhaa, hakusita kunyanyua upanga na kumkata sikio la kuume mtumwa mmoja wapo wa kuhani mkuu, Yesu anamsahihisha, hakukosa kwenda naye mpaka malangoni mwa behewa ya kuhani mkuu, na huko alipomsaliti, pia hakusita kuomba msamaha, na kuwa mwanafunzi wa kwanza kufika kaburini kuhakiki kufufuka kwa Yesu na kuonana na Yesu kati ya wale mitume 12. Siku zote alitazama maadamu ni hai, naweza kusahihisha na nikafanya kitu chema, kikafuta baya la jana na kunifanya kuwa mtu wa muhimu, mafanikio na mwenye kibari.
8. Petro aliwaza chanya siku ziku zote; siku zote alipoona fulsa imetokea, akaishinda hasi na kuweka chanya, alipoona Yesu amesema, ikawa ni fulsa, akaamini inawezekana, alipoambiwa kavue samaki wa kwanza atatoa pesa, japo hakuwa ona, akaamini akaenda, alipoambiwa wokovu kwa mataifa, Wayahudi wengine ilichukua miaka na miaka, lakini yeye aliamini saa hiyo hiyo alipoambiwa na Mungu, aliwaza chanya siku zote, hakutamani kubakiwa na hasi, aliiweka hasi ni ya jana, sasa si wakati uliyopita.
9. Petro aliamini anapohusika Mungu yote yanawezekana: Petro alipoambiwa shusha nyavu, hakuuliza mara mbiri "...kwa neno lako nitashusha nyavu" akashusha, alipoambiwa kavue samaki utapata pesa, haraka akaenda, Roho Mtakatifu alipowashukia, saa hiyo hiyo akaanza kuzungumza kwa ujasiri watu watubu, alipomuona kirema akiomba omba, hakutaka kuambiwa sasa unaweza kuponya, akafanya muujiza.
10. Alikuwa na roho kubwa ya uongozi. Petro alikuwa na roho ya kuongoza, najua kuwa kila mtu ana silka ya uongozi ila Petro alikuwa na roho ya uongozi, hii roho kila mtu huzaliwa nayo, ila ni jukumu la mtu binafsi kuifanya hii roho ichipuke na kufanya kazi. Petro alitamani kila kitu awe kiongozi, kila kitu afanye yeye, kila kitu kiwe sawa, kila kitu kiende inavyohitajika. Na hivyo Yesu akamfanya kuwa kiongozi. Kiongozi ni yule mtu ambaye yuko tayari kujitolea katika mambo yote, na hapa ndipo sehemu kubwa pekee inayomuwezesha mtu kuichipua roho ya uongozi.
11. Petro alikuwa mtu wa mahesabu na mfanya kwa faida. Wakati wote waliponyamaza kuhusu kumfata Yesu, Petro hakukaa kimya akaona aulize. "...tazama tumeacha vyote tukakufata; tutapata nini basi?" Petro hakutaka kufanya kitu kwa kujitoa kisichokuwa na matokeo ya maganikio yanayoitwa faida mbere.

NINI TUNAJIFUNZA...
1. Unaweza toka chini kabisa mpaka kuwa juu kabisa.
2. Usichoke kujaribu uonapo fulsa
3. Kila binaadamu anazaliwa na woga, shinda woga wako.
4. Kubari kufa kwaajili ya wengine, kuiponya nafsi yako ni kuwa tayari kuiuwa nafsi yako kwaajiri ya Kristo na watu wengine
5. Alitafuta kwanza ufalme wa Mungu, na mengine akazidishiwa; alifanya sehemu yake na kumuacha Mungu afanye sehemu yake.
6. Kama unachokimini kiko sawa, simama ulipo, usiyumbe wala kuyimbishwa. "The strongest man is a one who stand alone" Karl Max
7. Usisumbue mda wako kutazama jana, tazama fulsa sa leo, usitazame kushindwa au mafanikio yako ya jana, tazama fulsa za leo na uzitumie kwa nguvu ile ile iliyoko ndani yako, bila kuregea.
8. Hata wakati inahitajika uwaze hasi, au wengine wanawaza hasi, wewe waza chanya. Shinda mawazo hasi.
9. Amini wakati na mahari anapohusika Mungu yote yanawezekana.
10. Chipusha roho ya uongozi kwa kujitolea. Unapowapa watu vitu wanavyohitaji watakupa wewe zaidi ya unavyoviitaji.
11. Kuwa mtu wa mahesabu, hesabu hasara na faida. Unapotoa vyote kuanzisha biashara utapata nini basi, unapotumika usitumike kiuvivu, jitume ukijua faida yako ni kubwa toka kwa Yesu, umempa mtu mda wako kuonana naye, utapata nini basi, umeenda sehemu utapata nini basi. Chochote unachofanya lazima utazame utapata nini basi.

BARAKA TANO ZA PETRO
ngoja tuziorodheshe baraka hizo tano na ukurasa wa mbere tutaona namna alivyofanya kwa sehemu yake kwa uaminifu pasipo kuingilia nafasi ya Mungu, pasipo kumngoja Mungu aje afanye sehemu yake na Mungu akafanya sehemu yake kwa uaminifu na hivyo akafika alipoahidiwa na kutamani kufika.
1. Mvuvi wa watu—Luka 5:10B
2. Mwamba wa kanisa—Math 16:18
3. Mmiliki wa funguo za ufalme wa mbinguni—Math 16:19
4. Muimarishi wa wengine—Luka 22:32
5. Mlisha kondoo—Yoh 21:15


SEHEMU YA TATU
MAANA YA JANA, KESHO NA LEO

Mwaka wa 2009 nikiwa natoka shule ya sekondari ya Kigurunyembe nikiwa na marafiki zangu kadhaa, Mr. Maneno akanyanyua kinywa na kutamka kwa huzuni iliyochanganyika hasira na majuto kwa mbali, akasema "kama isingekuwa yule msichana nisingekuwa nimeferi" tukacheka sana, akanitazama "unajua nilikuwa na akiri sana zaidi hata yako dogo", nikamjibu kwa kebeghi "ndiyo basi tena, neno ningelijua huja mwisho wa safari" alikasirika na kujaribu kunipiga ila hakuweza. Wakati huo mimi tulikuwa tukisubiri kuchaguliwa kwenda elimu ya kidato cha tano, sasa kati ya wanne tulikuwa tukitembea wakati ule ni mimi pekee niliyekuwa na matokeo ya kufauru. Mr Maneno hakuwa anajuta kuferi, ila alikuwa anajuta alichofanya wakati aliokuwa amepewa kusoma akautumia kufurahi na kula anasa na msichana.

Monday, March 3, 2014

WAMNGOJAO BWANA TUTAPAA KAMA TAI (Isaya 40:26-31)


Isaya 40:25-31(31)
Tai ni ndege wa tofauti na ndege wengine kabisa.

SIFA ZA TAI
1.      tai anatembea na tai wenzie
na sio ndege wengine yeyote; sio mwewe wala kunguru
Ø  watu wapenda mafanikio wanatembea na wapenda mafanikio
Ø  watakatifu na watakatifu.
2.      tai anapaa umbari mrefu zaidi ya ndege wengine.
Ø  Mungu ni lazima atupe nguvu za kufanikiwa zaidi ya wengine
Ø  Mafanikio kazini zaidi ya wengine
Ø  Biashara mafanikio na wateja wengi zaidi
Ø  Tenda nyingi zaidi
Ø  Max nyingi zaidi kwa wanafunzi
3.      Tai anatazama umbari mrefu zaidi (kilometa 5 mbere)
na akikiona kitoweo au kitu hukivuta na kuonekana karibu na kukifata mpaka akipate, hata kama vikitokea vizuizi huwa hajari na hupambana mpaka akipate.
Ø  Hata majaribu yajapo 2014 hatutojari bali tunatazama ahadi za Jehova mpaka tutakapozifikia
Ø  Hata kama wakitokea watu kupinga, kazi au mume lakini tunatazama ahadi za Bwana mpaka tuzipate
Ø  Majaribu yajapo tunafumba macho na kuzivuta ahadi za Bwana na kuzitazama hizo tu.
Ø  Lolote na hilo (piga uwa) kupaa kama tai lazima.
4.      Tai hali mizoga bali anakula chakula halisi (kipaya/flesh)
Ø  Tunatafuta taarifa mpya na sio za zamani.
Ø  Hatutotumia vitu vya kale; kuazima au kupewa bali 2014 ni mwaka mpya na mafanikio mapya.
Ø  Sisi sio watu wa kazi za kale
Ø  Sisi sio watu wa asiri tena; ugonjwa na mikosi ya babu ni ya babu sisi tunaanza upya.
5.      Tai anatumia kimbunga au upepo mkali kupumzisha mbawa na kupaa juu zaidi.(upepo mkali unaoambatana na radi, mvua, na ngulumo kali).
Wakati ndege wengine wanajificha kwenye miti na vichaka kuogopa
Ø  Wakati wengine wanalalamika matatizo na shida wewe unatumia majaribu na shida hizo kupaa zaidi angani.
Ø  Tumngojeao Bwana tunatumia dhiki, uchi na adha kupaa juu zaidi kimafanikio.
6.      Tai wanapotaka kukutana (kujenga ndoa).
·         Mwanaume humfata mwanamke juu, mwanamke agunduapo hushuka chini na kuchukua gome au ganda la mti na kupaa nalo juu.
·         Akifika juu analiachia lianguke chini; mwanaume analiata kwa kasi, na jinsi linavyoongeza kasi naye anaongeza kasi; akilipata anarudi nalo juu na kumpa mwanamke.
·         Mwanamke anapaa tena juu zaidi na kuliachia tena; na mwanaume kulifata kama mwanzo na kulirudisha kwa mwanamke
·         Na mwanamke hupaa tena juu
·         Kitendo hiko hufanyika zaidi ya saa moja
·         Mpaka pale mwanamke atakapoona umbari wa kwenda juu unatosha na baada ya kuona mwanaume amefauru mchezo ndipo anakubari.
Ø  Kabla mtu hujakubari urafiki au ukaribu naye mpime kwanza
Ø  Sisi ni wa thamani (tumngojeao Bwana)
Ø  Sisi sio watu wa kawaida
Ø  Sio watu wa chipsi na keki au soda
Ø  Hatupatikani kirahisi
Ø  Ni bidhaa hadimu
Ø  Thamani yetu ni kubwa makazini; wanatuhitaji na wakibaki wao tu mambo yote yanaharibika.
Ø  Dunia yatuhitaji; ndio maana tukiondoka tu na dunia ndio mwisho wa mchezo wake.
Ø  2014 ni kutafutwa kama lulu
7.      Wanashirikiana kwenye uzazi
·         Tai jike anapotaka kuzaa; jike na dume wanashirikiana kutafuta eneo la juu la ncha ya mlima ambapo mnyama na adui hawezi kufika.
·         Mwanaume anaenda kutafuta miba na kuweka sehemu hiyo na kushuka tena chini kuleta magome ya mti kujenga kiota juu ya ile miba
·         Na kushuka tena chini na kuchukua miba na kuweka juu ya yale magome; anashuka tena na kuchukua nyasi na kufunika ile miba
·         Kisha anashuka tena na kuchukua ngozi kufunika zile nyasi
·         Baada ya kumaliza kujenga kibanda anarudi tena chini kuchukua miba mingi zaidi na kufunika kile kiota; kuzuia maadui.
Ø  Mwanaume na wanawake lazima tushirikiane katika kujenga familia; familia tujenge pamoja.
Ø  Kanisa lazima tubebane: muujiza wa mtu upo mikononi mwetu
Ø  Nyumba zetu, familia zetu, maisha yetu ni lazima yalindwe na Damu ya Yesu.
Ø  Wako makini kufanya mambo yao nasi lazima tufanye mambo kwa umakini.
Ø  Baba anafanya jukumu kama kichwa na mama anakaa pembeni na kutia moyo
8.      Wakati wa kufundisha watoto.
·         Mama yao anawatoa kwenye kiota sababu ya uwoga wanarudi tena
·         Hivyo mama yao anatoa ngozi na kubakiza miba- hivyo wanaporudi tena ndani wanakutana na miba wanachomwa na kutokwa na damu
·         Wanashangaa baba na mama yao aliyewapenda sana leo amewageuka na kuwaumiza.
·         Na baadae mama yao anawasukuma pembeni ya ncha ya mlima na kuanza kuruka kwa hofu.
·         Kabla hawajaanguka chini baba yao anatokea na kuwabeba wasianguke na kuwarudisha mlimani
·         Kitendo hiko kinaendelea mpaka wahakikishe wote wanajua kuruka sawa sawa.
Ø  Wanapopatwa na mshangao wa mateso hayo- hapo hapo wanapata maarifa na mbinu mpya za kimaisha na kuishi
Ø  Mungu anakuwekea miba (shida, dhika, uchi na adha na mateso na majaribu) kwa mema; ili upate mafunzo na kukufanya uwe bora zaidi ya sasa.
Ø  Wakati mwingine anafanya kama amekuacha kumbe yupo pembeni akikutazama na kabla hujaanguka anakuja kukubeba
Ø  Tumngojao Bwana mwaka huu ni lazima tubebwe na Jehova katika Jina la YESU.
Ø  Na atakujaribu kwa kila hatua mpaka ufuzu mafunzo yote na kuitwa mkakamavu: ukifuzu level moja anakupeleka level nyingine mpaka uwe umekomaa ndipo anakuacha.
Ø  Tunapaswa kujifunza kutoka kwenye matatizo na sio kuraumu
Ø  Kawaida watu wanaopata mateso, magumu na matatizo magumu na mengi ndio ambao wanatoka na maarifa, hekima na uzoefu zaidi. MFANO DAUDI NA SULEMANI
9.      Tai anaishi miaka mingi zaidi
·         Anaishi miaka 70
·         Lakini kufika miaka hii, anapaswa kufanya uamuzi mgumu katika maisha yake.
·         Akifika miaka 40;
o   Mdomo wake unachoka/unazeeka na kushindwa tena kuchukua mawindo(ukari na uregu wa mdomo unapinda)
o   Kutokana na uzee na uzito wa mabawa, manyoya yanarundikana kifuani na kumfanya kushindwa kuruka.
·         Anabakiwa na maamuzi mawili tu
o   Kufa
o   Au kupitia mateso na maumivu ya siku 150 (miezi 5)
·         Kitendo hiko kitamtaka tai apande juu ya ncha ya mlima kwenye kiota chake na kujipiga kwenye mawe mpaka ncha ya mdomo wake ivunjike yote.
·         Na kukaa akisubiri mpaka ncha ya mdomo iote yote.
·         Baada ya hapo analazimika kutoa manyoya yake yote ya uzeeni mpka abaki pasipo hata na nyoya
·         Baada ya miezi 5 anapata manyoya mapya na kuishi tena miaka 30.
Ø  Anaonesha kwamba wamngojeao Bwana kumbe kumbe tuchakaapo kuna kuzaliwa upya na kufanya upya tena na kuishi miaka mingine zaidi tukiwa na nguvu mpya.
Ø  Ni lazima tukubari kubadirika hata kama mengine yanaumiza; kwenye ufalme wa Mungu
Ø  Kujitoa kwenye matatizo ya kale ni lazima tukubari kupoteza faida za sasa (vya thamani vya sasa) kwaajiri ya baadae
Ø  Tunapaswa kutoa mambo yote ambayo hayana umuhimu kwetu kwa sasa ili kufanyika upya; kwaajiri ya kesho yetu
Ø  Lazima tukubari mateso, majaribu na shida kwaajiri ya baadae
Ø  Wakati fulani twapaswa kutoa tamaduni zetu, tabia, na mazoea fulani ili kuweka tabia na ufahamu mpya
Ø  2014 Bwana anakwenda kurenew maisha yetu na kutupa mapya yenye raha zaidi.
Ø  Maombolezo 3:22
Ø  Ayubu 17:9


THANKS ALMIGHTY GOD, Please my Dear God go and teach your people yourself; but I give all my body to use me as a tools, For Your Glory. In Jesus Name... Amen


                       




                       


                       

  

Wednesday, December 25, 2013

PURPOSE OF PRAYER AND CHRISTMASS


KUSUDI LA MAOMBI NA KRISMASS
Kusudi la Yesu kuzaliwa ilikuwa ni kurudisha utawara wa mwanadamu ulikuwa umeibwa na shetani amba mwanadamu alipewa na Mungu.
Mwanzo 1:26
Mungu anampatia mwanadamu utawara, anawaambia mkataware (Let them have dominion), lakini shetani anakuja kuchukua ule utawara kwa kumkosanisha mwanadamu na Mungu (kuondoa uhusiano wake na Mungu) Ambao ndiyo nguzo kuu ya utawara wake;maana hawezi kutawara pasipo kuwa na utawara na Mungu.
Shetani alipchukua ule utawara toka kwa mwanadamu, ndipo akachukua cheo cha mwanadamu kama mkuu wa ulimwengu huu na yeye kuwa ndiye mkuu wa ulimwengu huu, shetani akaanza kumtawara mwanadamu na kumuamrisha afanye anachokitaka yeye, na mwanadamu hakuweza kujizuia kwake, hata wafalme walimfata, Sauli alikosea, Mussa alikosea, Daudi alikosea, Sulemani alikosea, Yeroboam alikosea na wengine, machafuk, na dhambi zikaingia ulimwenguni, watu kuuwana wa kwa wao na kuuwa wanyama kwa kasi kubwa sana, uzinzi, ufiraji, ubakaji, ukahaba, ushoga na usagaji, wizi, udokozi, vita, unafki na umbea na magmvi ya kila aina.
Mungu akaleta mapigo mawili kwa kuamini wenda mwanadamu akamrudia yeye (sodomo na ghomola, na ile ya Nuhu) lakini mwanadamu akaendelea kutenda maovu kwasababu alikuwa chini ya mkuu wa ulimwengu huu shetani
Ndipo Mungu akasema sitomwangamiza mwanadamu tena, bali nitafanya nae agano jipya, Yeremia 31:31; 32:40
Yesu akazaliwa ili kuunda agano hilo jipya, na kuzaliwa Yesu ni ishara ya agano hilo jipya kama ilivyotabiliwa na nabii Isaya( Isaya 7:14, 9:6)
na ishara hiyo ilikuwa ni utawara; Hivyo Yesu alikuwa ni ishara ya kurejeshwa utawara unaotokana na uhusiano wa mwanadamu na Mungu. 
Yesu alipozaliwa akazaliwa kwa kusudi la kurejesha uhusian huo
ndio maana alipokufa pazia la hekalu(patakatifu pa patakatifu) na hivyo si makuhani tena bali kila mtu ana ruhusa ya kutengeneza uhusiano wake binafsi na Mungu na kupkea utawara ambao baba yetu na mama yetu Adam na Hawa waliupoteza.
na hivy kwa kuzaliwa kwake na kupigwa kwake basi hapo kwanza hatukuwa taifa lakini sasa tu taifa la Mungu, na tumefanyika wafalme na makuhani, watu wa milki ya Mungu (1petro 2:9, Ufunuo 5:10)
na sasa Ufalme wa Mungu si ufalme wa watu tena wa kawaida bali ni ufalme wa wafalme chini ya MFALME WA WAFALME
na si tena watu chini ya Kuhani bali ni ufalme wa makuhani chini ya Kuhani mkuu Yesu. 
Na hivyo utawara wetu umerejea tena.
Yesu akasema nimewapa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka na kazi zote za yule adui,
lakini pia aliwapa mamlaka juu ya pepo wabaya na magonjwa yote (Luka 10:18-19)
na Yesu alipoondoka wanafunzi wa Yesu wakaanza, kuwa na amri dhidi ya pepo, magonjwa, na hata wafu wakafufuliwa na viwete wakatembea, na hiy ni ishara ya kurudishiwa ufalme.
Hivyo krismass ni kurudishiwa uhusiano na utawara ambao Ibirisi aliuchukua kwa Adam na Hawa.
lakini kuupata utwara huu ni lazima uwe mwana mambi, sababu Mungu hawezi kufanya kitu chochote duniani kama Mwanadamu asipoomba na kuruhusu kifanyike kwa njia ya Maombi
Yoh 12:31, yoh 16:11