Tuesday, November 22, 2022

UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KWA MKRISTO

 KWANINI TUNAMHITAJI ROHO MTAKATIFU?

Somo la Kwanza


Luka 24:45, Mdo 1:4-5

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasitoke mjini mpaka wapokee Roho mtakatifu, maana yake ni muhimu sana kwa Mkristo. Yesu alileta ufalme wa Mungu, na alitaka watu kuingia ndani ya ufalme huo. Wanafunzi walipotaka kujua lini atawaletea ufalme, Yesu anasema kuhusu Roho Mtakatifu.

Yesu anamaanisha ili mfanikiwa ndani ya huu ufalme muhimu sana ni Roho mtakatifu.

  • Utaona kabla Yesu hajafanya chochote kwanza alipata Roho mtakatifu

  • Pia utaona anaawaacha wanafunzi wake, pia anawaambia wasitoke mpaka wapokee Roho

  • Na wanafunzi wake, utaona katika mahubiri yao, cha kwanza kabisa mtu akiokoka ni Roho mtakatifu, na ishara yao kubwa kama mtu amepokelewa na Mungu basi ni kupokea Roho Mtakatifu. Mfano mzuri ni habari ya Kornelio


KWANINI TUNAMHITAJI ROHO MTAKATIFU/ UMUHIMU WA RMT

  • ROHO NI MUHIMU KATIKA WOKOVU WETU.

Tunaokoka kwa njia ya Roho mtakatifu.

  • Yoh 3:5-6 tunazaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho mtakatifu.

Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

  • Tito 3:5 Roho ndiye anayetufanya upya.

si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

Roho ndiye anashuhudia kuwa sisi tu watoto wa Mungu

  • Rum 8:16 ndiye anashuhudia pamoja na roho zetu

Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

Roho ndiye arabuni ya wokovu wetu

  • 2 Kor 1:22 Naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. Arabuni ni ishara ya kitu kijacho. Muhuri ni dhamana au uthibitisho.

naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.

Tunatunza yale mazuri Mungu aliyotupatia kwa Roho Mtakatifu

  • 2 Tim 1:14 Tunalinda ile amana nzuri kwa RMT. Amana ni akiba nzuri au ya thamani. Pasipo Roho utapoteza kila kitu.

Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

Tunamshinda adui kwa Roho Mtakatifu

  • Mdo 1:8 mtapokea nguvu akishawajilia juu yenu RMT. Mfano wa Skewa Mdo 19:14-16. Hawa watu hawakuwa wameokoka, wakatamka jina la Yesu wakijaribu lakini hawakuwa na nguvu.

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

  • Mdo 8:5-7, 5:3-5. Filipo kwa sababu alijaa Roho mtakatifu akashinda nguvu zote za giza, mpaka mganga akasalimu amri.

Tunashinda tamaa za dunia na za mwili kwa RMT

  • Rum 8:13 

kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

Tunakuwa imara katika wokovu kwa sababu ya Roho Mtakatifu

  • Mdo 4:8, 13 walipotikiswa Roho akawapa hekima ya kujibu kwa ujasiri mpaka mafarisayo wenyewe wakashangaa.

Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,

Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Pastor Ulenje

+255 683 477827

MOROGORO, TZ.

Saturday, November 19, 2022

MAANA HALISI YA MAOMBI 01.

Mpaka tumejua maombi ni ‘serious task’ kwetu tulio-amini, Hapo tutaanza kuomba. 


 Yesu anasema tukiomba tusipayuke-payuke.

Kupayuka si maneno mengi, kupayuka ni kurusha maneno pasipo shabaha. haikuwa na maana ya kukataa kuomba kwa sauti, ila usifanye hivyo kwa kuamini kuwa sauti huleta ufanisi wa maombi au ndiyo maombi yanakuwa na matokeo. 

Sauti haileti matokea, sauti ni sauti tu. Bali kuomba bila shabaha, bila imani, bali kutamka maneno mengi tu ukifikiri ndiyo kupata majibu, hiyo ndiyo kupayuka. Bali maombi lazima yawe na shabaha, yawe na matarajio. 

Pasipo matarajio hakuna uhakika, pasipo uhakika hakuna imani, pasipo imani hakuna majibu ya maombi, pasipo majibu ya maombi, maana yake bado hujaomba. 

 Swali kwanini Yesu alisema tusipayuke? 

Yesu alitamani tuombe kwa shabaha. Na hii ndiyo siri ya kuombea jambo la mda mrefu, ng’ang’anizi, lililokufata mda mrefu. Unapoingia kuomba ni muhimu kujua kuwa, hitaji lako Yesu alilijua kabla hata ya hitaji kukufikia (Math 6:8, Zab 139: 16), maana Yeye ndiye aliyeziamuru siku kabla hata hazijaja bado. Ndiyo maana akasema “...Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba”

 Mjumuisho wa maneno yote ya mwanzo ndipo tunapata maana ya maombi. Maombi yana nguvu sana kama yakiombwa kwa shabaha. Yaani kuomba ukiwa na matarajio ya kitu fulani kitokee, na ukaomba mpaka kitokee. 

Majibu ya Mungu ni kama bahari, cha kushangaza wengine wanaenda na vijiko, nenda kwa Mungu na matarajio makubwa, matarajio yasiyo na kizuizi cha kutazama uwezo wako bali uwezo wa Mungu usio na kipimo.

 MAANA YA MAOMBI

Kama Yesu anasema Baba Yetu anajua haja zetu kabla hata hatujaomba, kwanini hayashuki TU!?

 Yesu akasema “Basi ninyi salini hivi; Baba Yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Math 6:9-10). 

 Hivyo tunapoingia kwenye maombi tunaingia kwenye very serious business of God’s Kingdom, kushusha mapenzi ya Mungu ambayo yalishakuwa tayari mbinguni hata kabla siku hizi hazijafika, Mungu alikuwa anakusubiri wewe uyashushe duniani (Muhimu 1Kor 2:9). 

Yesu anawaambia wanafunzi wasalipo, wamwambie MUNGU mapenzi yake yatimizwe, kwanini wakati Mungu si mwanadamu hata a-amuriwe na mtu. 

Hapana “Mungu pasipo mtu hafanyi, na Mtu pasipo Mungu hawezi”. 

Usipotamka nini kitokee duniani Mungu hafanyi bali anasubiri mtu mmoja/wawili/zaidi “aliyeitwa kwa jina lake, ajinyenyekeshe na kuomba, na kumtafuta uso, na kuziacha njia mbaya; basi atasikia toka mbinguni na kuwaamehe dhambi yao, na kuponya nchi yao” (2 Nya 7:14) 

Hivyo; Maombi ni kumruhusu Mungu kuingilia jambo duniani 

Kifupi: Maombi ni kushusha mapenzi ya Mungu duniani.

Usikose Sehemu ya pili ya Somo hili kwenye Blog hii ya ulenje.blogspot.com. 

Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477827

Morogoro, TZ.


Saturday, November 12, 2022

LAZIMA UWE NA SHAHUKU YA KUKUA NA KUONGEZEKA

Bila shahuku ya kukua hakuna mtu aliyewahi kukua.

Shika sana hili_ Wewe ni zaidi ya jinsi ulivyo na unaweza kuwa zaidi ya ulivyo leo.

📌 Kwa Mungu inatakiwa tukue, na Mungu anategemea tukue. Eph 4:13,14

Mungu ametupa nguvu ndani yatu, ikiwa na kazi ya kutufanya tukue. Kuna vitu Mungu hawezi kukupa, ijapokuwa ni vyako, mpaka ukue. Galatia 4:1-7.

Hata chakula, mafanikio, karama, vipawa, nafasi, fulsa na cheo, ambacho Mungu anakupa, kinatokana na ukuaji wako.


MAENEO MUHIMU UNAHITAJI KUKUA NA KUONGEZEKA.


1. Kua kwenye Kuomba

Math 26:40_ Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja.

Yesu alitaka wanafunzi wake wakue katika muda na stamina yao ya kuvumilia usingizi na kuomba.


2. Kukua kwenye kufunga

Math 9:15

Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.

Yesu alimaanisha, siku atakayopaa basi lazima tuanze kuutisha mwili kuacha chakula kwa ajili ya Bwana kwa muda fulani.


3. Kukua kwenye imani

Math 17:16, 19-21

Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.

Yesu alitegemea kwa muda aliokaa na wanafunzi wake, unatosha kukua imani, wakamvunja moyo alipoona kumbe bado wana mashaka hata kutoa pepo. Yesu anategemea kwa muda huo ulio kaa kwenye wokovu, uwe tayari una imani ya kutoa pepo na zaidi.


4. Kukua kwenye Neno.

Ebr 5:12

Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 

Kolosai 1:10 anasema "mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu"

Muda huu inatakiwa uwe tayari unaweza kufundisha siyo tena hata maziwa hujui, weka bidii kusoma neno ili ukue katika maarifa ya Mungu. 


5. Kukua katika kumtumikia Mungu.

Luka 5:10

Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu. 

Mungu anataka ufike hatua ya kuanza kuvua watu.

Yoh 15:16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Mengine yote ni mema, ila kusudi moja la kuokolewa ni ili ukazae matunda, uokoe wengine. "Mungu ametutuma kila sekta ili kuokoa watu kila sekta" huu ndiyo msemo wangu naupenda.


6. Kukua kwenye kiasi.

1 Thes 5:6-8

Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. 

Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 

Chochote fanya kwa kiasi, fanya kwa ratiba, ili ufanye kingine pia.


Mimi ni Pastor Ulenje 

+255 683 477827 

MOROGORO. TZ.

Saturday, April 23, 2022

JUA UNDANI KUHUSU MAISHA YA MILELE

 *** MAISHA YA MILELE NA MWAMINI 


-( 1 Wathesalonike 4:13-18)

-Kwanini tunajifunza maisha ya milele? Ni muhimu sababu mtu ataweza ishi kwa kujizuia (mithali 29-18).

-Mtu anaejua Kuna maisha ya milele ataishi kwa umakini Sana

-MUNGU ametupa maisha ya sasa ili tujiandae na maisha ya milele


- MUNGU ametupa maisha ya sasa ni mchujo na kigezo kikubwa alichoweka ni utii Yani unae mtii ndie BWANA  wako

- Tamaa za shetani ni 

1)Tamaa ya mwili

2)Tamaa ya dunia

3)Kiburi Cha uzima


*Mwanadamu akifa anaenda wapi ??

- katika Agano la kale neno walilopata ni kuzimu (Zaburi 49-14) Yani walio haki na wasio haki wote wanaenda kuzimu ( Zaburi 88-3)

-YESU anakuja kutuonyesha kuwa kule kuzimu walitenganishwa walio haki na wasio haki ( Luka 16-19) YESU anatuletea neno peponi na jehanamu.


-Mtu asiyeokoka akifa anaelekea jehanamu ( Marko 9-45)

-Mwenye haki akifa anaelekea peponi( luka 23-43)

- peponi sio mbingu mpya peponi ni Mahali pa kufarijiwa

-Jehanamu sio Mahali pa mwisho kwa wasio haki Mahali pa mwisho ni kwenye ziwa la moto ( ufunuo 21-13)

- Walio haki wakifa wanaelekea peponi wakisubili pia hukumu kwa matendo ya mwili waliofanya baada ya kuokoka .

- peponi sio Mahali pa mwisho kwa waliokoka Bali ni mbingu mpya ama yerusalem mpya biblia inasema Mahali huko  ni pazuri hamn mfano Kuna Kuna dhahabu Safi Kama bilauri pia Kuna kuta nne ambazo marefu na mapana yake zimefanana kuta zimepambwa na madin Kama zumaridi  ,yakuti nk

- katika yerusalem mpya hutokumbuka maumivu 


* Nini maana ya kufa kwa mwamini ???

-Ni kuondoka toka mwili huu wa batili na kwenda kukaa na BWANA(2 Wakorinto5-6)

- Paulo alitamn kukaa na BWANA (wafilipi 1-21)

-Paulo anasema tuziweke kando zile dhambi zinazotuzuia( waebrania 12-1)


* Unaishi kwa ajili ya Nani???

- MUNGU anasema mbele yenu nimeweka uzima na mauti Ila chagueni uzima ( kumbukumbu la torati 30-19)

-(wafilipi 1-21)

-(warumi 6-21)


* Kiti Cha hukumu Cha KRISTO 

- Kwa walio haki

-wafu watafufuliwa kuungana na walio hai siku ile ya parapanda kuu ( 1wakorinto 15:50-53)

-(warumi 14-10)

-(2 wakorinto 5-10)

- sisi tuliokoka hatutahukumiwa pamoja na wasiokoka sisi tutahukumiwa maisha yetu baada ya kuokoka 

- Paulo anasema wengine kazi zao zitaungua Kama nyasi anasema wataokoka Ila kwa Moto 

 

* Vitu ambavyo tutatolea hesabu 

1)namna gani umeshiriki kuleta watu kwa KRISTO ( Daniel 12-3)

2) kwa habari ya ulimi 

3) kwa habari ya kushindwa dhambi( warumi 6:1-4)


-From pastor ulenje EM

Written by kayombo jr